Watanzania tujaribu kuwa na shukrani japo kidogo..

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,318
Kuna mijadala inaendelea kuhusu kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, Wengi wanasema kocha huyu hatufai wengine wanadai hana ubora wa kuifundisha Stars,

Swali ni je hiyo miaka 39 ambayo hatukushiriki Afcon hao makocha walifanya nini Mpaka tuanze kumpa lawama Amunike , ni kipi kinatufanya tushindwe kuheshimu taaluma za watu?

Nini kinatufanya tusiwe na shukrani kwa kocha huyu aliyetuongoza mpaka tukashiriki Afcon baada ya miaka 39 kupita bila kushiriki.

Nani asiyetambua uwezo wa senegal inawachezaji bora na wanaocheza ulaya, Senegal inashika nafasi ya 1 kwa mataifa ya Africa kwenye rank za Fifa inacheza na Tanzania ambayo ni ya 23 na kati ya timu 24 zinazoshiriki Afcon mwaka huu Tanzania imemzidi Burundi pekee,sasa mtu anamlaumu kocha kwa kupoteza mchezo dhidi ya senegal amesahau kuwa wapinzani wetu ni bora zaidi.

Sisi kama watanzania tunatakiwa kujua sisi ni#Underdog kwenye mashindano haya tuache lawama siziso na misingi kikubwa tushiriki kutokana na uwezo wetu tusilazimishe kufanana na wenzetu ambao walishakuwa na mikakati tangu awali na wametuzidi kwa kila kitu katika maendeleo ya mpira wa miguu..

Hapa tulipo mpaka sasa ni mafanikio baada ya kuburuzwa kwa miaka mingi michuano hii kwa sasa iwe njia ya kujipatia uzoefu na kujipanga kwa michuano ya mbeleni sio muda wa kulaumu bali ni muda wa kujipanga..

Amunike wa muda mfupi ni bora kuliko makocha bora hewa ndani ya miaka 39 iliyopita
..
HAPA TULIPOFIKA CHINI YA AMUNIKE NI MAFANIKIO YATUPASA TUWENA SHUKRANI NA SI LAWAMA SISIZOJENGA..

Imeandikwa na #Gluka_de_sports..
 
Tanzania imemuzidi Burundi, nadahani aliyefanya tathimini alikosea. Ukilinganisha mchezo wa Burundi na Nigeria na ule wa Tanzania na Senegal, unaweza kuendelea kuikumbatia hiyo tathmini?

Kama kawaida, ni kitu gani watanzania wanaweza kutembea kifua mbele na kujivunia? Ni kuondoa ukabila miongoni mwao, hakuna lingine!!!!

Huwezi kunenepesha mbuzi siku ya mnada ukapata matokeo mazuri. Tusunirie mvua siku Tz inakutana na Algeria, wengine wako kazini sisi tunaenda kwenye maigizo.
 
Tanzania tunaweza maneno tu tena Kila mtu anajifanya kocha wakati hata timu ya mtaani kwao tu hajawahi ifundisha
 
Mechi ya jana tulizidiwa kila kitu na kila Idara, Boko alilosajiliwa goli la wazi kabisa. Samata hukuonekana kabisa, Boko naye sababu walilazimika kurudi kukaba badala ya kushambulia..

Rafu za kijinga Sana vijana wa taifa stars walikuwa wanacheza, midfield ilikufa kabisa alikosekana mtu wa kuzuia na kuwalisha forwards/strikers mipira, mabeki wetu nao bure kabisa..

Shukrani pekee jana zimfikie kipa wa Stars kwa kucheza kizalendo na kujitoa kwa dhati na kweli kwa nchi yake, magoli yote alofungwa ni uzembe wa mabeki..

Zaidi tumshukuru Mungu walau hatukufungwa goli nyingi, na kwa matokeo ya jana ni wazi stars anaondoka mapema sana maana kwa Algeria na Kenya pia atapigwa tu.

Despite wadhamini na serekali kujitoa kwa michango na mengine bado wachezaji wetu wamekosa morale na ari ya kupambana kwa ajili ya nchi..
1. Viwanja, ikumbukwe wameahidiwa kila mmoja kupewa kiwanja bure endapo watafika walau 8 bora.
2. Vifaa vya ujenzi, mdhamini ASAS alisema wazi atatoa Tani moja ya cement, nondo na mengine kwa kila mchezaji endapo wakafika walau nusu fainali.
3. Fedha, wadhamini wameahidi mamilioni ya pesa.

Sielewi bado pamoja na vyote hivi, bado vijana wameshindwa kujitoa. Amunike kipanga timu mbovu kabisa, na alipoingia Ulimwengu walau mchezo kidogo ukabadilika.

Jana nimeumia Sana,
 
ili kupata taifa star.wale wachezaji simba na yanga achana nao kabisa na cheki vipaji ambavyo hatutaki hata kuvijua lakini ni balaa.kwa hali hii
 
Tanzania imemuzidi Burundi, nadahani aliyefanya tathimini alikosea. Ukilinganisha mchezo wa Burundi na Nigeria na ule wa Tanzania na Senegal, unaweza kuendelea kuikumbatia hiyo tathmini?

Kama kawaida, ni kitu gani watanzania wanaweza kutembea kifua mbele na kujivunia? Ni kuondoa ukabila miongoni mwao, hakuna lingine!!!!

Huwezi kunenepesha mbuzi siku ya mnada ukapata matokeo mazuri. Tusunirie mvua siku Tz inakutana na Algeria, wengine wako kazini sisi tunaenda kwenye maigizo.
Huna taaluma hiyo ya uchambuzi wa soka...kwa kauli hii bado unaonekana hujatambua mchango wa kocha...kaa kwenye mada halafu maana unayumbishwa na mentality za kizamani sana ,cha msingi soka linahitaji mchakato mpaka kuja kufikia hatua kubwa, sasa kwa mpira waliocheza vijana jana wameonyesha ukomavu na uthubutu kwenye kucheza mpira bora...kumbuka wapinzani senegal wameshakua kwenye hii michuano mara nyingi sana na uzoefu pia wanao....kwa Taifa star wanahitji pongezi katika kuwatia moyo...tusubiri mechi zijazo...kama tumeweza shiriki sahivi ni sehemu pia ya kujenga uzoefu na kujiamini.
 
Kati ya ujinga ambao huwa siukubali ni huu wa kuaminishana eti tutafungwa kisa timu fulani wachezaji wake wanacheza ulaya.Kwa maana hiyo na sisi tusubiri mpaka kikosi kizima kicheze ulaya ndio tufanikiwe na hiyo itakuwa lini? Kama sio kwamba tutasubiri Sana.

Wazambia 2010 walichukua ndoo ya CAF mbele ya Ivory coast iliyokuwa na kikosi Cha wachezaji wa ulaya tena timu kubwa Kama Arsenal, Chelsea,Man City etc

Taifa stars pumbafu kabisa timu haiwezi kupiga hata pasi tano za uhakika eti inashiriki Afcon.
 
Hii timu inaendeshwa kisiasa na kina BASHITE, ni lazima itafeli tu, hata hatua ya makundi haiingii.
 
Hebu acheni utani, vijana jana Taifa star jana wameifanya senegal waonekane wamecheza chini ya kiwango...vijana wamekaba na kucheza pass..kasoro pale mbele tu,sasa kwa kiwango waliocheza senagal jana wangekutana na timu kama uganda wasingefurukuta,so far vijana wetu wameonyesha mpira mzuri,cha kufanaya marekebisho ni foward ili tusiwe tunapiga pass tu na kukaba angalau tutafute na magoli
 
Kwani mpaka tunakwenda afcon tulishinda. Mechi ngapi chini ya Amunike...
Pia usisahau kwenda kwetu Afcon ni kwa hisani ya uganda

Kufungwa sio shida angalia burundi na namibia wamefungwa lakini wameonyesha wana nini katika timu.. Kocha kashindwa kufundisha timu hata kupiga pasi.
 
Chini ya mdenish paulsen tulikuw tunacheza mpira mzuri sana
Tanzania hata aje kocha zidane bado tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu. Tuige Uganda wamejenga timu yao kwa miaka 4 mfulilizo, Tanzania kila match maingizo mapya ya wachezaji. Timu haiwezi kuwa na muunganiko na maelewano kila siku tutaendelea kurukaruka kama taifa tuje na mpango wa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom