Uchaguzi 2020 Watanzania tuisikilize hii sauti ya Mungu "Huyu ni Mwanangu Mpendwa Mpeni Kura Zenu"

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
568
1,562
Hii ni sauti inayonisumbua kila kukicha ya Mungu Ikiniambia Huyu Ni Mwanangu Mpendwa Nimpe Kura yangu.

Naamini ni sauti inayokusumbua pia wewe Mtanzania ikijurudirudia na kukusii uitii kua " Huyu alie Hai leo ni Mwanake Mpendwa na Tumpe Kura Zetu"

Tanzania itapona tu kwa Kuitii Sauiti Hii ya Mungu.

Wewe Ulisikia wapi Mtu kupigwa Risasi zaidi ya Thelatha na akapona kama hii sio ni Makusudi ya Mungu.

Wewe Ulisikia Wapi Mtu kujaza Nyomi ka lote bila kusaidiwa na Media wala Wasanii kama hili sio kusudi la Mungu.

Wewe Ulisikia wapi Sehemu Raisi wa Nchi alipozomewa lakini Mpinzani wake akashangiliwa kama hii si Ishara ya Mungu kudhihilisha Mtu aliemchagua.

Watanzania tutapataje kupona tusiposikia Wito Huu Mkuu kutoka kwa Mungu ukitutaka kumchagua Mja wake Tundu Antipadi Lissu.
 
Njoo nikupeleke kwa mganga wa risasi. Inaelekea TAL alikuwa mchanga au ameshakiuka baadhi ya masharti ndo maana zikampata vile. Wewe hujiulizi kwa nini dreva wake hakupatwa na risasi hata moja?
 
Mungu akitaka kuuangusha utawala wa kidhalimu, hua anatumia vizazi vyao wenyewe.

Kuna mifano mingi, ila mmoja kwa dini zote;

Mtume Mosses (Nabii Mussa A.S) alilelewa na farau wa misri, ndani ya familia na ndani ya kasri lake. Kipindi ambacho farau aliambiwa na waganga wake kwamba kuna mtoto wa kiume amezaliwa kuja kumaliza maisha yake na kuuangamiza utawala wake milele.

Baada ya kuambiwa tu, aliamua kuwachinja watoto wote waliozaliwa na wanaozaliwa wote wa kiume, na akawaacha watoto wa kike.

Ila Mtume Mosses (Nabii Mussa A.S) alizaliwa, na mungu kuonesha uwezo wake, alifanya alelewe ndani ya kasri la farau mpaka akakua. Alikwepeshwa na yale mauwaji ya watoto wa kiume maelfu kwa maelfu. Kisha ahadi ikatimia ya kumuangamiza farau kupitia kwake.

Tuje TANZAGIZA;

Tanzania, wameuliwa, wamefungwa, wameonewa na kupotea watu wengi sana kwa hofu ya kuja kuangamiza utawala wa kifarau (CCM), kina Ben Saanane, Azory Gwanda na kadhalika. Ila kuna mmoja tu ambae ameshindikana, Tundu Lissu. Sijui inaashiria nini hasa wana bodi.
 
Magufuli anapigwa na Mungu.

Huwez kua Mtawala unayefumbia haki mateso, mauaji.

Kwenye historia ya Biblia Hamna kiongozi wa aina ya Magufuli aliyetusua.
 
Hakika hii nyomi, ni muujiza mkuu wa Mungu aliye hai...........

Tunapaswa watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa, tuitii sauti hiyo ya Mungu, kwa kumchagua huyu shujaa, ambaye naamini ameletwa kwa makusudi maalum, ili aje alikomboe Taifa hili kutoka kwenye mikono ya madhalimu hawa wa CCM
 
Back
Top Bottom