Watanzania tuhoji; kama maandamano ni haki ya kidemokrasia, kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane Ikulu wakati wa kuapishwa Rais Biden?

Wewe unaweza kumsema mdogo wako kuoa Mke Kicheche wakati Mkeo anajulikana ni Zulia la Wageni?
Mimi mke wangu kuwa kicheche haihalalishi mdogo wangu kuoa mke kicheche kuwa jambo zuri na jambo sahihi.Tunakubaliana kwanza hadi hapo?
 
Mipaka pia ina mipaka - huwezi kuzuia kila kitu cha kisiasa kwa vyama vya upinzani kisifanyike nchini kwa kigezo tu eti demokrasia ina mipaka yake!!
Kwahiyo ww unaona ni sahihi kuwaacha watu waingie na silaha nzito Ikulu kama alivyoeleza bwana Tumbiliwaulaya juu?
 
Kwahiyo ww unaona ni sahihi kuwaacha watu waingie na silaha nzito Ikulu kama alivyoeleza bwana Tumbiliwaulaya juu?
Nani alishawahi kuandamana ama kwenda kwenye mikutano ya hadhara Tanzania akiwa na siraha? Hebu acheni mambo yenu ya kijima!!

Hatuwezi kuruhusu mtu mmoja kufanya anachowaza yeye tu, akumbuke watanzania tupo mil 60 na tuna fikra pia na zinaweza kuwa bora kuliko hata za kwake. Kuua sauti za watu ni dhurma kubwa mno na inakiuka misingi ya demokrasia na haki za binadamu - mwambieni.
 
Sisi na demokrasia yetu tumeshawahi kurugusu waandamanaji wenye silaha kuingia bungeni?
 
Kuna mahali popote umeona serikali ya Marekani ilikataza maandamano?
Umeona tamko lolote la maandamano kupigwa marufuku?
Yaani umelenga hoja nzito sana hata humu JF kuna watu wengi hushabikia maandamano kuwa ni haki yao.
UZITO wa swali lako ndio umeona wanaanza kukujibu utumbo.
HONGERA kwa kuliona hilo.
 
Measures za kujikinga mbona zipo? Kama vile kuvaa barakoa na Social distancing? Wangewaambia wavae barakoa na social distancing kati ya mtu na mtu wanapoandamana
Mkuu mtu akiwa na hasira anaweza asifate hizo measures
 
Nani au chombo gani kilitoa tamko la kukataza maandamano?
Issue ni katiba inatoa uhuru wa kuandamana haijaweka exceptions kuwa kila mwandamanaji mmoja anatakiwa aongozane na askari mmoja!!! hii hesabu yako umeiokota wapi? kuwa waandamanaji wakiwa laki moja na askari wanatakiwa wawe laki moja kuwa kuwe na ratio ya one to one!!! unajuwa nimecheka hili jibu lako umejibu kituko
 
Haki bila mipaka ni vurugu.... na mipaka bila haki ni utumwa.

Wenzetu wana haki lakini wanatambua pia lazima kuwa na mipaka, huku hata hiyo haki ya kuandamana kwa masharti hakuna.
 
Nani au taasisi gani walitoa tamko la kukataza maandamano wakati wa kuapishwa kwa Biden?
swali zuri na ninaona linafaa linafaa kujibiwa na mwanasheria nguli anaeishi ugaibuni tundu lissu
 
Issue ni katiba inatoa uhuru wa kuandamana haijaweka exceptions kuwa kila mwandamanaji mmoja anatakiwa aongozane na askari mmoja!!! hii hesabu yako umeiokota wapi? kuwa waandamanaji wakiwa laki moja na askari wanatakiwa wawe laki moja kuwa kuwe na ratio ya one to one!!! unajuwa nimecheka hili jibu lako umejibu kituko
Weka hicho kifungu tukione....
 
HOJA YAKO N NZURI KWA KIWANGO CHAKO.

HUJATUAMBIA TOKA UCHAGUZI MWAKA JANA MPAKA 20/01/2021 KWANINI WANAACHA NAFASI MUDA MREFU KIASI HICHO? JE HAO WANAOTAKA KUANDAMANA HICHO KIPINDI HAKIKUWATOSHA KUFIKISHA JUMBE ZAO? JE HAPA TANZANIA KUNA SIKU WATU WAMEANDAMANA KWENDA IKULU?
 
Unaweza kutupa tamko lolote la jeshi la Marekani wakikataza maandamano wakati wa kuapishwa kwa Biden?

Unaweza kuweka screenshot au clip yoyote ya tamko la kipuuzi kama hilo kutoka kwa jeshi la Marekani?

Unafahamu jeshi la Marekani ndilo linahusika na ulinzi wakati wa kuapishwa kwa Rais na kilichofanyika ni kuongeza idadi ya wanajeshi tu wakati wa kuapishwa kwa Biden tofauti na Marais wengine?

Kwa sababu wakati wa Trump waliwekwa wanjeshi 8,000 na wakati huu wameongezwa hadi 25,000 wewe hiyo ndio unaita kuzuia maandamano?
Wamarekani ndio hujifanya vinara wa kufundisha demokrasia na mojawapo ya haki za kibinadamu na kidemokrasia ni kuandamana kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda Ikulu alikokuwa akiapishwa Rais Biden?

Wao hutuambia kazi ya majeshi sio kuzuia waandamaji ni kuwalinda wanapoandamana.

Na huku kwetu wengine upinzani husema hayahitaji hata kibali kinachotakiwa ni kutaarifu tu polisi.

Sasa kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda Ikulu alikoapishwa Joe Biden?
 
Wapi ulisoma au kusikia maandamano yamezuiwa nje ya eneo la Capitol Hill analoapishiwa Rais?
Lawama ni kwa askari walitakiwa waandamane na waandamanaji kuhakikisha wanaandamana kwa amani sio kuzuia .Sio kazi ya jeshi kuzuia maandamano kwa demokrasia waliyotufunza wenyewe!!! WANGEWAAMBIA RUKSA KUANDAMANA wakaambatana nao kusindikiza maandamano yao sababu ni haki yao ya kidemokrasia
 
Wamarekani ndio hujifanya vinara wa kufundisha demokrasia na mojawapo ya haki za kibinadamu na kidemokrasia ni kuandamana kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda Ikulu alikokuwa akiapishwa Rais Biden?

Wao hutuambia kazi ya majeshi sio kuzuia waandamaji ni kuwalinda wanapoandamana.

Na huku kwetu wengine upinzani husema hayahitaji hata kibali kinachotakiwa ni kutaarifu tu polisi.

Sasa kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda Ikulu alikoapishwa Joe Biden?
Kwani Marekani wakizuia waandamanaji ndio inaleta uhalali wa Tz kuzuiwa kuandamana?. Non-sense...... Kuandamana kushinikiza watu wasipigwe risasi hadharani bila ya kuwa na RB hadi sasa, kutekwa hovyo, kung'olewa meno/kucha bila ganzi nk inalinganishwa na kuandamana kuelekea Ikulu kwa Joe B?.
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Marekani ni waalimu wetu wa maandamano lakini wazee wa MAGA wamethibitisha ni magangsta kuliko maelezo.

Jamaa wanapata cha 'ARUSHA' kwanza kabla ya kuandamana.
 
Wapi ulisoma au kusikia maandamano yamezuiwa nje ya eneo la Capitol Hill analoapishiwa Rais?
Kwa hiyo ruksa kuruhusu watu kuandamana porini? Kwa hiyo tuanze kuruhusu watu wasiandamane mabarabarani wakaandamane porini huko kusiko na wahusika?

Hata kwetu serikali haiwezi zuia mtu akitaka kuandamana porini
 
Marekani unaruhusiwa kuandamana unavyotaka,ILA USIHARIBU mali au kuingilia wengine uhuru wao
Mbona hiyo hata Tanzania ipo lakini sisi tukifanya wanabweka mfano kuandamana barabarani unazuia uhuru wa watu wengine kutumia barabara kwa shighuli za kujiletea maendeleo nk
 
Unaifahamu Capitol Hill?
Unataka watu wakaandamane ndani ya eneo la bunge?

Back
Top Bottom