Watanzania tuhoji; kama maandamano ni haki ya kidemokrasia, kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane Ikulu wakati wa kuapishwa Rais Biden?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,485
2,000
Wamarekani ndio hujifanya vinara wa kufundisha demokrasia na mojawapo ya haki za kibinadamu na kidemokrasia ni kuandamana kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda Ikulu alikokuwa akiapishwa Rais Biden?

Wao hutuambia kazi ya majeshi sio kuzuia waandamaji ni kuwalinda wanapoandamana.

Na huku kwetu wengine upinzani husema hayahitaji hata kibali kinachotakiwa ni kutaarifu tu polisi.

Sasa kwanini Jeshi la Marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda Ikulu alikoapishwa Joe Biden?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,485
2,000
TABIA ya waandamanaji imeakisi sana tabia ya msamasishaji wao Trump,na hata hivyo na wewe kwa akili yako unaweza ukaruhusu waandamanaji wenye siraha kwenda kuandamana ikuru?
Kumiliki silaha marekani ni haki ya kidemokrasia na kutembea nayo ni haki yake kwa sababu ni ya self defence na kuandamana ni haki ya raia wa marekani walitakiwa waruhusiwe kwa demokasia ambayo wao wenyewe hujifanya vinara wa kuhubiri!!!
 

shamimuodd

JF-Expert Member
Jan 28, 2019
640
1,000
TABIA ya waandamanaji imeakisi sana tabia ya msamasishaji wao Trump,na hata hivyo na wewe kwa akili yako unaweza ukaruhusu waandamanaji wenye siraha kwenda kuandamana ikuru?
Hahaha si wao wanajisema wana demokrasia hahahaha, pimbi kabisa hawa, wanatuletea mamluki sisi waandamane tukizuia nongwa ila pini hao vibaraka wao tumewapiga na bado mpaka akili ikae sawa
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,485
2,000
huna habari ya kwa nini wamefanya hivyo?!? USIPOTOSHE elezea fujo za CAPITOL HILL ndio uhitimishe na hicho kibwagizo chako
Lawama ni kwa askari walitakiwa waandamane na waandamanaji kuhakikisha wanaandamana kwa amani sio kuzuia .Sio kazi ya jeshi kuzuia maandamano kwa demokrasia waliyotufunza wenyewe!!! WANGEWAAMBIA RUKSA KUANDAMANA wakaambatana nao kusindikiza maandamano yao sababu ni haki yao ya kidemokrasia
 

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
274
500
Wamerekani ndio hujifanya vinara wa kufundisha demokrasia na mojawapo ya haki za kibinadamu na kidemokrasia ni kuandamana kwa nini Jeshi la marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda ikulu alikokuwa akiapishwa Raisi Biden?

Wao hutuambia kazi ya majeshi sio kuzuia waandamaji ni kuwalinda wanapoandamana

Na huku kwetu wengine upinzamni husema hayahitaji hata kibali kinachotakiwa ni kutaarifu tu polisi
Sasa kwa nini Jeshi la marekani lilizuia watu wasiandamane kwenda ikulu alikoapishwa Joe Biden?
Yaani umelenga hoja nzito sana hata humu JF kuna watu wengi hushabikia maandamano kuwa ni haki yao.

UZITO wa swali lako ndio umeona wanaanza kukujibu utumbo.

HONGERA kwa kuliona hilo.
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
878
1,000
Lawama ni kwa askari walitakiwa waandamane na waandamanaji kuhakikisha wanaandamana kwa amani sio kuzuia .Sio kazi ya jeshi kuzuia maandamano kwa demokrasia waliyotufunmza wenyewe!!! WANGEWAAMBIA RUKSA KUANDAMANA wakaambatana nao kusindikiza maandamano yao sababu ni haki yao ya kidemokrasia
Wamarekani wako almost milioni200 NATIONAL GUARDS waliokuwa deployed ni kama elfu25 tu so wakijitokeza waandamanaji 100k askari watakuwa na uwezo wa kuambatana nao?!?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,485
2,000
wamarekani wako almost milioni200 NATIONAL GUARDS waliokuwa deployed ni kama elfu25 tu so wakijitokeza waandamanaji 100k askari watakuwa na uwezo wa kuambatana nao?!?
Issue ni katiba inatoa uhuru wa kuandamana haijaweka exceptions kuwa kila mwandamanaji mmoja anatakiwa aongozane na askari mmoja!!! hii hesabu yako umeiokota wapi? kuwa waandamanaji wakiwa laki moja na askari wanatakiwa wawe laki moja kuwa kuwe na ratio ya one to one!!! unajuwa nimecheka hili jibu lako umejibu kituko
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,551
2,000
Sidhani kama sehemu wanaruhusu maandamano yasiyo ya amani. Laiti wiki mbili zilizopita wangeandamana kwa amani wasingezuiliwa. Halafu mkuu YEHODAYA kuna muda unakuja na great threads halafu baadae unakataa.
 

Jinikashkash

JF-Expert Member
Nov 27, 2020
400
1,000
Nadhani Tbccm hawa kukuonyesha wale hawakuwa wandamanaji bali wahuni na wezi waliosababisha vifo vya watu watano.

Sijui kama hata unajua makundi ya Q Anon na Proud Boys yalioandaa fujo zile yana itikadi gani.

Hii huwezi jua kama source yako ya habari ni Uhuru na Mzalendo
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
878
1,000
Issue ni katiba inatoa uhuru wa kuandamana haijaweka exceptions kuwa kila mwandamanaji mmoja anatakiwa aongozane na askari mmoja!!! hii hesabu yako umeiokota wapi? kuwa waandamanaji wakiwa laki moja na askari wanatakiwa wawe laki moja kuwa kuwe na ratio ya one to one!!! unajuwa nimecheka hili jibu lako umejibu kituko
Sina hakika katika hilo kwamba katiba yao haikuweka mashariti ya kuandamana.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
2,993
2,000
Usitake kuhalalisha ushetwani wenu kwa mgongo wa Marekani.

Wale watu hawafanyi vitu kihuni, kishenzi kama serikali ya jiwe.

Jiwe angekuwa US. angekuwa ashafungwa jela kitambo.

Ana makosa lukuki ikiwemo matumizi mabaya ya kiti
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,485
2,000
Sidhani kama sehemu wanaruhusu maandamano yasiyo ya amani. Laiti wiki mbili zilizopita wangeandamana kwa amani wasingezuiliwa. Halafu mkuu YEHODAYA kuna muda unakuja na great threads halafu baadae unakataa.
Ni kazi ya askari kulinda amani kwenye maandamano sio kuzuia hiyo ni kwa mujibu wa demokrasia wanayotufundisha wao .Wao walitakiwa tu kuyalinda wanapoandamana sio kuzuia
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,551
2,000
Ni kazi ya askari kulinda amani kwenye maandamano sio kuzuia hiyo ni kwa mujibu wa demokrasia wanayotufundisha wao .Wao walitakiwa tu kuyalinda wanapoandamana sio kuzuia
Kasome upya ujue tofauti ya maandamano ya amani na vurugu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom