Uchaguzi 2020 Watanzania tufungue macho na tujiulize haya kuhusu wagombea wa wapinzani

Mzee mende

Member
May 29, 2020
33
29
TAFAKARI YANGU

Mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Na tayari tuko kwenye kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo kwenye ngazi zote zinazohusika.

Uchaguzi huu ndio jiko la kupika na kuwaivisha viongozi wapya watakaoliendesha gurudumu la uongozi wa taifa letu,ndio watakaobeba mustakabali wa marndeleo katika nyanja mbali mbali yakiwemo ya kiuchumi.

Vyama vyote vikubwa vya CCM, CHADEMA, ACT, CUF na NCCR-Mageuzi vyote vimeweka wagombea wake kwenye nafasi za urais na zile za ubunge na udiwani. Huu ni mwezi wa tisa na leo ni tarehe 13/09/2020 tayari harakati za kampeni zimevuka robo.

Kuna matukio mawili makubwa yanayozaa tafakari katika mchakato huu:

1)Ni kitendo cha mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutangaza nia yake ya kugombea urais Tanzania akiwa nje ya Tanzania (nchini Ubelgiji) kuna maswali mengi kwenye hilo lakini kibwa likiwa ni je, Mgombea huyu anawakilisha Maslahi ya Watanzania?

Na swali hili likaturudisha nyuma, kwa kurejea takwimu za kiongozi huyu mtia nia ya Urais, je akiwa mbunge lini tuliwahi kumsikia akisema lolote juu ya kuinua hali za wananchi kiuchumi, kiafya, kelimu, kibiashara n.k hata tu kwa wananchi wa jimbo lake?

2) Tumekuwa tukifuatilia kampeni za wagombea hawa. Pia tumekua tunafuatilia mapokeo yao kwenye mikutano hiyo, lakini zaidi tumefuatilia hata namna wanavyoripoti habari zao za kampeni ili kuuhabarisha umma.

Kwenye hili la kuuhabarisha umma kuna tafakuri nyingine hapa, na hasa chama cha Chadema kinahusika zaidi, na hoja hapa ni lugha wanayoitumia zaidi kuuhabarisha umma. Tumeona mara nyingi mno uongozi na watoa habari wa chama hiki wakitumia lugha za kigeni kuuhabarisha umma juu ya maoni yao au mapokeo wayapatayo na matarajio wakati wa kampeni na lugha zitumikazo ni Kiingereza na Kiarabu.

Tunajiuliza tena: je, hili ni kwa maslahi ya nani?
Kweli walengwa ni Watanzania wa Ikungi, wale wa Mwandiga, au wale Hai, au labda wa Mbamba bay na Tandahimba? Tunajiuliza zaidi, hasa lengo ni nini? Au ndio zile sauti zisemazo kwamba hawa wametumwa na watu wa huko, na ya kwamba wao ni mawakala tu wa ukoloni? Kwamba mkoloni ndie amewatuma waje kupanda upya mbegu za ukoloni na ubeberu?

3) Kama ilivyoelezwa hapo juu kuwa leo mchakato wa kampeni umeshavuka robo ya ufanyikaji wake toka uanze, lakini nchi ikiwa kwenye joto hilo tunamuona mmoja wa wagombea wa nafasi nyeti kabisa ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Bernad K Membe anasafiri kwenda nchini U.A.E kule Dubai.

Hatujui hasa kilichompeleka ,na yeye au chama chake hakijatamka lolote. Watanzania wana haki ya kujuzwa juu madhumuni ya safari ya mgombea huyu wa Urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo huko Falme za Kiarabu au maslahi ya safari hiyo kwa Tanzania
Je, huko Dubai nako kuna mikutano ya kampeni? Au labda huko kuna ofisi za chama cha ACT-Wazalendo?

Sasa iwapo kiongozi wa namna hii na yule aliyetangaza nia akiwa ughaibuni, wakipewa dhamana ya kuiongoza serikali ya nchi yetu na kukabidhiwa mustakabali wa watu wa taifa hili la Tanzania watakua na uwezo au utayari wa kuyapigania maslahi ya Watanzania? Au watakua ni viongozi wa kusafiri tu kuelekea huko walikotumwa?

Katika uhai wa taifa letu, taifa lenye umri wa miaka 59, moja ya mambo ambayo waasisi wa taifa hili na hasa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mambo tuliyofundishwa, moja ni kuwa gereza baya zaidi na utumwa mbaya zaidi ni ule utumwa au ufungwa wa akili. Je, vyama hivi havijashikiwa akili? Je, hawatumiki kuchonga bara bara ya ukoloni mpya? Je, dhamira yao si kukwamisha harakati za mtanzania kukombolewa kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya na katika nyanja nyingine?

Mungu ametujaalia macho, ametujaalia akili. Tumebarikiwa kuwa na utashi bora kabisa lakini jana yetu tunaifahamu vyema kabisa na taswira ya kesho yetu rais John P. J. Magufuli ameshatuonesha vizuri sana. Tukatae kutumika na tukatae vibaraka na mawakala wa ukoloni.

Alamsiki wana +255
 
Kama unampenda sana Lissu siyo vibaya. Sisi tunamtaka JPM siyo kwa mapenzi baina yetu bali ni kwa mapenzi ya nchi yetu kaonyesha njia kavunja kale kaduara kazamani cha watu kula mema ya nchi na wengine wakitazama
 
Magufuli ndiye raisi wa nchi, na Hussein Mwinyi ndiye raisi wa Zanzibar. Pinga pinga na vibaraka hawana nafasi

(huo ndio ukweli hata kama ni mchungu)
 
Kama unampenda sana lisu siyo vibaya. Sisi tunamtaka JPM siyo kwa mapenzi baina yetu bali ni kwa mapenzi ya nchi yetu kaonyesha njia kavunja kale kaduara kazamani cha watu kula mema ya nchi na wengine wakitazama
Mkuu ukiangalia kwa undani wako watu wanatumika kwa maslahi ya mabeberu. Lakini ipo siku kitaeleweka.
 
Mtajuta kumfahamu Mh.Tundu Lissu. Hakika anawanyoosha vilivyo. Ukweli wote utajulikana mwaka huu. Na uzuri hayupo mwenye uwezo wa kuyajibu makombora anayawatumia.
 
TAFAKARI YANGU

Mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Na tayari tuko kwenye kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo kwenye ngazi zote zinazohusika...
Na tukifumba macho tujiulize hicho chama tawala ambacho kimekuwepo toka uhuru hadi leo ilikuwaje kikafilisi mashirika ya umma, kikaangamiza mashamba na kudunisha kabla ya kubinafsisha migodi?

Tujiulize zaidi kwanini chama hicho kinashangaa umaskini wa nchi na umaskini wa watanzania ilhali chenyewe ndio kinatawala!!!?
 
TAFAKARI YANGU

Mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Na tayari tuko kwenye kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo kwenye ngazi zote zinazohusika...
Asante tunayaheshimu mawazo yako,inapia tuna mitazamo tofauti tofauti ,tunayaona yote natunayachambua natural yafanyia uamuzi nakila mmoja atapata haki take kulingana na alichopanda.
 
Namba hukumalizia mkuu, ila kwakusema ukweli kama kuna mgombea anaongea hoja vizur ni wa CHADEMA. Mh Lisu ukitoa ushabiki wa kisiasa ni mtu mwenye akili ya juu sana.
 
Kama unampenda sana lisu siyo vibaya. Sisi tunamtaka JPM siyo kwa mapenzi baina yetu bali ni kwa mapenzi ya nchi yetu kaonyesha njia kavunja kale kaduara kazamani cha watu kula mema ya nchi na wengine wakitazama

Kwa taarifa yako kila kiongozi ana kundi lake la kula, tena bora hata hao wengine walikula na kuachia wengine kula. Huyu yeye anakula na genge lake, mpaka kufikia kujenga uwanja wa ndege huko kwao.
 
TAFAKARI YANGU

Mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Na tayari tuko kwenye kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo kwenye ngazi zote zinazohusika.

Uchaguzi huu ndio jiko la kupika na kuwaivisha viongozi wapya watakaoliendesha gurudumu la uongozi wa taifa letu,ndio watakaobeba mustakabali wa marndeleo katika nyanja mbali mbali yakiwemo ya kiuchumi.

Vyama vyote vikubwa vya CCM, CHADEMA, ACT, CUF na NCCR-Mageuzi vyote vimeweka wagombea wake kwenye nafasi za urais na zile za ubunge na udiwani. Huu ni mwezi wa tisa na leo ni tarehe 13/09/2020 tayari harakati za kampeni zimevuka robo.

Kuna matukio mawili makubwa yanayozaa tafakari katika mchakato huu:

1)Ni kitendo cha mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutangaza nia yake ya kugombea urais Tanzania akiwa nje ya Tanzania (nchini Ubelgiji) kuna maswali mengi kwenye hilo lakini kibwa likiwa ni je, Mgombea huyu anawakilisha Maslahi ya Watanzania?

Na swali hili likaturudisha nyuma, kwa kurejea takwimu za kiongozi huyu mtia nia ya Urais, je akiwa mbunge lini tuliwahi kumsikia akisema lolote juu ya kuinua hali za wananchi kiuchumi, kiafya, kelimu, kibiashara n.k hata tu kwa wananchi wa jimbo lake?

2) Tumekuwa tukifuatilia kampeni za wagombea hawa. Pia tumekua tunafuatilia mapokeo yao kwenye mikutano hiyo, lakini zaidi tumefuatilia hata namna wanavyoripoti habari zao za kampeni ili kuuhabarisha umma.

Kwenye hili la kuuhabarisha umma kuna tafakuri nyingine hapa, na hasa chama cha Chadema kinahusika zaidi, na hoja hapa ni lugha wanayoitumia zaidi kuuhabarisha umma. Tumeona mara nyingi mno uongozi na watoa habari wa chama hiki wakitumia lugha za kigeni kuuhabarisha umma juu ya maoni yao au mapokeo wayapatayo na matarajio wakati wa kampeni na lugha zitumikazo ni Kiingereza na Kiarabu.

Tunajiuliza tena: je, hili ni kwa maslahi ya nani?
Kweli walengwa ni Watanzania wa Ikungi, wale wa Mwandiga, au wale Hai, au labda wa Mbamba bay na Tandahimba? Tunajiuliza zaidi, hasa lengo ni nini? Au ndio zile sauti zisemazo kwamba hawa wametumwa na watu wa huko, na ya kwamba wao ni mawakala tu wa ukoloni? Kwamba mkoloni ndie amewatuma waje kupanda upya mbegu za ukoloni na ubeberu?

3) Kama ilivyoelezwa hapo juu kuwa leo mchakato wa kampeni umeshavuka robo ya ufanyikaji wake toka uanze, lakini nchi ikiwa kwenye joto hilo tunamuona mmoja wa wagombea wa nafasi nyeti kabisa ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Bernad K Membe anasafiri kwenda nchini U.A.E kule Dubai.

Hatujui hasa kilichompeleka ,na yeye au chama chake hakijatamka lolote. Watanzania wana haki ya kujuzwa juu madhumuni ya safari ya mgombea huyu wa Urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo huko Falme za Kiarabu au maslahi ya safari hiyo kwa Tanzania
Je, huko Dubai nako kuna mikutano ya kampeni? Au labda huko kuna ofisi za chama cha ACT-Wazalendo?

Sasa iwapo kiongozi wa namna hii na yule aliyetangaza nia akiwa ughaibuni, wakipewa dhamana ya kuiongoza serikali ya nchi yetu na kukabidhiwa mustakabali wa watu wa taifa hili la Tanzania watakua na uwezo au utayari wa kuyapigania maslahi ya Watanzania? Au watakua ni viongozi wa kusafiri tu kuelekea huko walikotumwa?

Katika uhai wa taifa letu, taifa lenye umri wa miaka 59, moja ya mambo ambayo waasisi wa taifa hili na hasa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mambo tuliyofundishwa, moja ni kuwa gereza baya zaidi na utumwa mbaya zaidi ni ule utumwa au ufungwa wa akili. Je, vyama hivi havijashikiwa akili? Je, hawatumiki kuchonga bara bara ya ukoloni mpya? Je, dhamira yao si kukwamisha harakati za mtanzania kukombolewa kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya na katika nyanja nyingine?

Mungu ametujaalia macho, ametujaalia akili. Tumebarikiwa kuwa na utashi bora kabisa lakini jana yetu tunaifahamu vyema kabisa na taswira ya kesho yetu rais John P. J. Magufuli ameshatuonesha vizuri sana. Tukatae kutumika na tukatae vibaraka na mawakala wa ukoloni.

Alamsiki wana +255
Andiko zuri na mwenye akili ameelewa. Yote yanayofanywa na Hawa jamaa ni wameshanuswa na mabeberu...
 
hatutaki serikali ya mjomba na mpwa wake
 
Back
Top Bottom