Watanzania tufunge mkanda, kipindi kigumu zaidi kinakuja

Hilo liko wazi mkuu.
Kuna watu wanashangilia sana ila wote tutapata tabu na shida haitachagua mtu.
Watumishi wa umma mjipange, hususan walimu, askari na kada zingine ambazo hazina maslahi nje ya mshahara nawambia mjipange lijalo litawafurahisha sana.

Graduates ambao mmejiingiza kwenye siasa hamna connection yoyote aisee mjipange itafika hatua hata ugali hamtaweza kununua, mtahama mjini mrudi vijijini kwenu.
Wasanii mliounga mkono juhudi mjipange, mnaishi kwa kutegemea kuimba na show za hapa na pale, mjipange nawambia
Itabidi watu wajikombe sana na kulamba miguu ya wanene ili miradi yao itimie...
 
Kipindi cha mateso kwa watanzania chaja. Mwenye kupuuza na apuuze.

Wafanyakazi hawataongezewa mishahara, wakiongezwa, wataongezewa karatasi lakini siyo fedha.

Shilingi itadidimia kwa kasi, na fedha ya kigeni haitapatikana mikononi mwa mwananchi. Na kutokana na upungufu wake, kuipata itakuwa kwa kuomba, na ukikutwa nayo, itakuwa ni hatia.


Elimu itadorora kwa kukosa funding. Installment ya pili ya fedha ya elimu toka WB haitapatikana kama ilivyotarajiwa.

Haitazidi miaka miwili, inflation itakua na kufikia double digits, na kuzifanya bidhaa zinazotoka nje ya nchi kutonunulika.

Watanzania wengi wenye uwezo kifedha na hata baadhi ya wasio na uwezo mkubwa, watatapakaa mataifa jirani kutafuta maisha.

Hakutakuwa na uwekezaji kutoka nje, na wawekezaji wa nje na ndani waliopo, watazidi kuondoka, na kusababisha tatizo kubwa la ajira. Kutokana na tatizo kubwa la ajira, hata watakaokuwa kwenye ajira, maslahi yao yatakuwa duni kupindukia.

Wafanyakazi pekee watakaoonekana ni muhimu kuliko wote ni Polisi, wanajeshi, magereza na wasiojulikana. Hawa watatumika vilivyo katika kuzima sauti yoyote itakayotaka isikike dhidi ya mtawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moderator naomba comment hii muiweka hapo juu kwenye huu uzi kwa lengo la kuboresha hii mada.
 
Back
Top Bottom