Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Jumuiya ya Watanzania kwa ujumla inasahau kwamba lilikuwa kosa la jinai kwa mazungumzo binafsi ya simu kati ya kina Makamba, Nape nk kunaswa na kurekodiwa? Je walikuwa wakipelelezwa na vyombo vya usalama nchini? Kulikuwa na kibali cha Mahakama kwamba simu zao ziwekwe katika vyombo vya kunasa mazungumzo yao?
Na kama Raisi Magufuli ametumia njia haramu ambayo haikubaliki kisheria kunasa mazungumzo binafsi ya simu, yeye ndiye alipaswa kuwa wa kwanza kuwaomba msamaha kina Makamba na Tanzania kwa ujumla.
Ni haramu kisheria na kimaadili kunasa mazungumzo binafsi ya simu ya watu bila kibali au sababu za msingi za kiusalama, lakini inaonekana hili linafanywa na awamu ya tano kwa kawaida na hawaoni kama ni tatizo!
Je, watanzania tuelewe kwamba sasa imefikia serikali ya awamu ya tano imekuwa ikinasa mazungumzo ya viongozi wa kitaifa na watu wengine bila ridhaa zao au amri ya mahakama? Hivi kwa nini Watanzania hatulioni hili bali fikra zote tumezielekeza kwenye tarumbeta zinazopigwa juu ya watu kuomba msamaha kwa raisi? Ukweli ni kwamba serikali yeyote inapofikia hatua ya kuanza kunasa mazungumzo ya simu ya viongozi wa kitaifa, hiyo ni serikali ya kidikteta.
Ni kosa kisheria na katika haki za binadamu kufanya hivyo. Raisi Magufuli atueleze kwa mfano, kwa nini serikali ilikuwa ikinasa mazungumzo ya Makamba akiwa waziri katika serikali? Je alikuwa akipelelezwa? Mahakama ilitoa kibali? Na habar iliyopo na kwa maneno yake mwenyewe, Raisi Magufuli ameenda mbali na hata kueleza hadharani kwamba mbali na mawaziri, anafanya hivi hata kwa majaji, kwamba wanachoongea katika simu au email zao sio siri kwake. Ni kwa nini haya yanafanyika? Katiba yetu inampa Raisi mamlaka hayo?
Na hivyo hivyo mazungumzo ya Kinana na Makamba Junior. Raisi Magufuli atoe maelezo ya kina kwa nini serikali iliona kuna umuhimu wa kuwa wananasa mazungumzo yao ya simu, na kwa kutumia sheria ipi ya usalama, na kama walikuwa washukiwa wa uhaini.
Nawashauri viongozi kutia ndani mawaziri muwe makini sana katika suala la kuongea na simu rasmi zenu maana tumeingiliwa. Tumieni simu ambazo hazijasajiriwa katika majina yenu na ambazo mtawapa namba zake watu mnaowaamini tu, kwa kuwa inaonekana serikali ya awamu ya tano imeamua kufanya mambo kama vile kichaa kapewa rungu.
Haikubaliki kabisa kunasa maongezi ya simu ya watu bila sababu za msingi au amri ya mahakama. Na ni wazi kwamba viongozi wote wa kitaifa pamoja na wastaafu simu zenu zinanaswa, au "kudukuliwa" kama wanavyosema mitaani.