Watanzania tudumishe uungwana na utashi wetu

Makame

JF-Expert Member
Jan 3, 2008
512
60
UCHAGUZI MKUU 2010.

1. Zoezi hilo limekamilika, ikiwemo matokeo ya Rais, Wabunge na Madiwani. Kwa upande wa Zanzibar, Rais wa Awamu ya 7 ashaapa.

2. MADAI YA KUCHELEWA MATOKEO NA KUCHAKACHULIWA. Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu Kiravu ametolea ufafanuzi. Ikumbukwe kuwa wasimamizi wa uchaguzi walikuwa na hadi siku mbili za kuwasilisha majibu TUME kisheria. Hivyo, hapakuwa na ucheleweshaji; bali elimu ya kiraia haikuwa ya kutosha.

3.MADAI YA KUCHAKACHULIWA yalianza tokea kipindi cha kampeni; huku uchochezi kwa Watanzania ukifanyika kuwaandaa kufanya fujo kwa madai ya machakachuzi.

4. KUKUBALI MATOKEO. Kwa kuwa uchaguzi ushakamilika, hapana budi

(a) Wagombea kukubali matokeo. Penye uchaguzi, ni mgombea moja ndio atapata kiti; wengine hawana budi kuheshimu maamuzi ya kura za wananchi. Ni Usataarabu wa kisiasa kwa wagombea kukubali matokeo.

(b) Observers washatoa maoni kuwa Uchaguzi ulikuwa wa Huru na Haki; basi tuwachane na ushabiki wa kisiasa na tujinasue na 'kuwa brainwashed'; let us look ahead and build our nation. kuna maisha baada ya uchaguzi.

(c) Kwa wenye reservation, watumie taratibu zilizopo kuziwasilisha reservation zao. Suala la vurugu zilizofanyika Ubungo na Mwanza zilizopelekea kujeruhiwa watu pamoja na mali sio ustaarabu wa watanzania. Aidha tuungane kuwapa pole ndugu zetu wa CHADEMA kule kigoma kwa kupigwa na mabomu ya machozi ofisini kwao.

(d) Tuwapongeze Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri ila tuwahimize wawe makini zaidi kukabiliana na uchafuzi wa amani kama ule uliotokea mwanza
 
Mi naona wewe akili yako haija kaa sawa.. nyinyi ndio mtakao buruzwa hadi mwisho..
Mimi sikatai kuwa Kikwete ameshinda,, kiukweli ameshinda lakini haya mambo yamezidi hivi unajua walicho kifanya Jimbo la Geita? au na wewe ni NEC mumeshiriki katika kuchakachua,, uchakachuzi umefanyika bwana tusikatae,,
 
RAJAB KIRAVU KATOA MAELEZO JANA KUHUSU GEITA.

Vyombo vyote vya habari vimefafanua.

Hakuna hoja ya uchakachuzi, it was human error and the NEC rectified the error; but clarrified the observation.

nawasilisha
 
Back
Top Bottom