Watanzania tuchukue tahadhari ya Corona. Jirani zetu Kenya hali ni tete haspitali zimezidiwa wagonjwa

Tunakumbushana tu hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mikusanyiko ya kila aina na majirani wa nchi jirani wanavuka mipaka kuja kuhani msiba huu mkubwa tulionao.

Tafadhali tuchukue tahadhari wenzetu Kenya hali ni tete.

Zaidi soma > Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa Corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua

Kwa hiyo unataka kumaanisha kuwa Wageni waliokuja ndiyo wanaweza kuileta hapa .... meaning that kwa sasa haipo!? SERIOUSLY!!
 
Tunakumbushana tu hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mikusanyiko ya kila aina na majirani wa nchi jirani wanavuka mipaka kuja kuhani msiba huu mkubwa tulionao.

Tafadhali tuchukue tahadhari wenzetu Kenya hali ni tete.

Zaidi soma > Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa Corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua

Tahadhari tulishachukua zamani na hatujawahi kukaa bila tahadhari. Ila usitupangie tahadhari inayoshinikizwa na mabeberu, wanaoifanyia biashara corona!! Usituambie habari ya Pima, Pima ,Pima!! Usituambie habari ya chanjo iliyopatikana kwa utaratibu wa mwendo kasi!! Usituambie habari ya barakoa za nje. Usituambie habari za lockdown!
Tahadhari yetu kama nchi huru ni: 1. Kumtanguliza Mungu kwa maombi ya kufunga. Hilo lishafanyika. 2. Kupiga nyungu! 3. Kunawa mikono mara kwa mara 4. Kula chakula bora chenye virutubisho vyote. Yote hayo watanzania tunayafanya!
 
Hivi hujawahi kushangaa? Rais wa Marekani (na viongozi wengine wa ulaya) alishapata chanjo ya corona mapema tu. Kwa kawaida wiki mbili baada ya chanjo mtu anapaswa kuwa na Kinga ya uhakika. Lakini huyu Biden pamoja na Kinga ya chanjo huwa anashinda na barakoa! Kama umechanjwa kwa nini uvae tena barakoa?? Jibu ni kwamba chanjo haiamini!! Sasa mabeberu wanataka kupiga pesa kwenye chanjo ambayo hata wenyewe hawaiamini kama inaweza kuwakinga.
 
Shujaa wa Afrika anaagwa bila watu kuvaa barakoa kwa sababu kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari nyingine wakati wa kumuaga shujaa wa Afrika ni kumkosea adabu.
 
Baada ya purukushani za huu msiba tutegemee watu wengi kulazwa mahospitalini kwa changamoto ya upumuaji - tatizo litakalotusumbua watanzania ni kuidharau COVID-19.
 
corona ni mabeberu wanatupiga vita. hamna big issue hapo. wanataka wauze chanjo na dawa zao.
 
Hivi hajawahi kushangaa? Rais wa Marekani (na viongozi wengine wa ulaya) alishapata chanjo ya corona mapema tu. Kwa kawaida wiki mbili baada ya chanjo mtu anapaswa kuwa na Kinga ya uhakika. Lakini huyu Biden pamoja na Kinga ya chanjo huwa anashinda na barakoa! Kama umechanjwa kwa nini uvae tena barakoa?? Jibu ni kwamba chanjo haiamini!! Sasa mabeberu wanataka kupiga pesa kwenye chanjo.
 
Back
Top Bottom