Watanzania tuchague moja, Tanzania kwanza au siasa kwanza

Dorin Kaaya

Member
Sep 18, 2020
15
15
Wana JF,

Nimeandika uzi wa TANZANIA NI BORA KULIKO SIASA

Nimepata reply nyingi na niseme wazi kuwa watu wengi wanaonekana kuichoka amani kwani ndani ya Tanzania wana-reply kwa hasira na chuki.

Leo naomba TUCHAGUE lipi bora, Tanzania kwanza au siasa kwanza. Tukichagua Tanzania kwanza nadhani tutaelewana.

Siasa za dunia na Afrika kwa ujumla zina mengi ila kikinuka ndo unaeza jua umuhimu wa nchi yako kuliko siasa niseme wazi kuwa Mimi naona Tanzania kwanza alafu wanadiaea wajichunge ili Watanzania waendelee na amani Kuna wengine tunajua pakiharibika, hakuna shule, hakuna kazi, hakuna kuoa wa KUOLEWA hakuna furaha.

Watanzania TUCHAGUE Tanzania kwanza au siasa kwanza nakuuliza wewe?
 
Hivo vyote vilishachaguliwa ndio maana vilikuwepo kabla hata wewe hujazaliwa.

Sema tu utandawazi umekuwa kazi mpaka mtoto wa drs la 3 anajua siasa ni nini? Na amani ni nini?

Pia vyote vinategemeana. Huwezi kula nyama wakati huna magego.
 
Kwa sasa watz wote hatupigi hatua kwenda mbele bali tunapiga marktime tuu.

Ili tupige hatua inabidi tutoke kwenye hii comfort zone, we need nea status quo.

Na hamna kuchagua, sio option ya mimi na wewe bali NYAKATI ndio muamuzi wa mambo yote.

Hivi unadhani wale walomuua Yesu walipenda? Hapana. Ni nyakati ndio ziliamua iwe hivyo. Kila jambo lina wakati wake na ukifika hakuna wa kulizuia.

Hivyo wewe usijitese buree, jiandae kwa chochote kitakachoamuliwa na nyakati tulizopo.

NB: Tukisema huwezi pambana na nyakati huu ndio mfano halisi hapa chini. Utafungia media zoooote zisimuoneshe mpinzani wako lakini haitafaa chochote.

IMG-20201016-WA0018.jpg
 
Bila siasa hata Tanzania yenyewe haitakuwa nchi bora, siasa imebeba mfumo wa nchi.
 
Kupitia siasa katika nchi za kidemokrasia hapa ndipo serikali huundwa.

Nchi bila serikali, Serikali bila nchi??

Huwezi Chagua kitu kimoja pekee hapo.
 
Mihemko ndio inawaua vijana

Kikinuka wananyumbulika maporini kama manyumbu

Mbaya zaid toka mambumbumbu wapate laki na nusu ya kununulia tekno huku mitanfaoni hatulali, wanachochea wasichokifahamu

Hawajui watawaponza hata bibi zao wasio na hatia kule kijijini

Wapo wanaosema bora amani itoweke.......

Ndugu zangu msiombee msichokijua

Bora ugali na chumvi kwenye amani kuliko pombe na nyama choma vitani
 
Hivo vyote vilishachaguliwa ndio maana vilikuwepo kabla hata wewe hujazaliwa.

Sema tu utandawazi umekuwa kazi mpaka mtoto wa drs la 3 anajua siasa ni nini? Na amani ni nini?

Pia vyote vinategemeana. Huwezi kula nyama wakati huna magego.
Point bro
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom