Watanzania tuamke tudai katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tuamke tudai katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mwiba, Apr 1, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  KATIBA NI NINI NA VIPI INAVYOTAKIWA IWE

  Katiba………..ni maandiko maalum yanyoweka utaratibu wa namna gani utawala, bunge na mahakama
  zitafanya shughuli zao. Katiba vile vile inaweka namna haki za wananchi zitavyoshughulikiwa na Serikali.  (Tizama Kitabu cha B.R.Atre Legislative Drafting 2nd Edn, pg 200)

  Kwa maana fupi kabisa, Katiba ni makubaliano maalum ya kanuni, utaratibu na mazoea ya chombo fulani yaliyowekwa pamoja na ambayo yanatoa mfumo, muundo na kazi ya chombo hicho. Pale tunapozungumia katiba ya nchi

  Hii inaonesha wazi kuwa Katiba ndio msingi mkuu wa sheria zote, na hakuna chombo kinachoweza kuichezea kwa kuibadilisha ovyo ovyo ila kwa utaratbu maalum uliowekwa. Na ndio maana huko Marekani kesi muhimu ya Marbury vs. Madison ikaamuliwa ya kuwa:

  “…..kwa sababu Katiba ndio sheria kuu ya nchi (kama ilivyo ibara ya VI ya Katiba ya Marekani) na kwa sababu ni mamlaka ya Mahkama kutekelza sheria hizo kwa vitendo, inamaanisha kwamba sheria nyengine za nchi,na hata sheria zinazopitishwa na Bunge (congress) zinaopotofautinana na kifungu chochote cha Katiba, basi sheria hizo zinatoa nafasi kwa Katiba, na sheria hizo lazima ziainishwe na Mahkama zetu kuwa ni batili”.

  Katiba pia inatoa mfumo au utaratibu wa kisheria kwa nchi husika juu ya muundao wa Serikali yake, vyombo vyake vya kisiasa na mahusiano baina ya wananchi na serikali na pia mahusiano baina ya wananchi wenyewe.Katiba ya nchi vile vile ni kama mkataba ambapo wananchi wenyewe na taifa hilo wamekubali kuwa mkataba huo utumike katika kuwaongoza wao na Serikali yao, pamoja na kukubaliana ni namna gani vyombo vya dola vitafanya kazi. Katiba ni lazima iwepo katika nchi ili kukinga matatizo yanayoweza kujitokeza ikiwa kila mwananchi atafuata utaratibu wake, au kila mkondo wa Serikali utafanya wanachokitaka. Katiba ni kanuni maalum ambazo zina lengo la kuiweka jamii pamoja, jamii ambayo itaishi katika mazingira ya amani na utulivu bila ya kuwa na migongano kwa lengo la kuleta maendeleo katika nchi hiyo.

  VIPI KATIBA INATAKIWA IWE ?

  Aliyekuwa Jaji Mkuu wa Marekani Sir. John Marshall, alisema katika kesi maarufu ya Mc. Culloch Vs. Maryland – 4 wheat 316 (US 1819) kwamba Katiba yao ni Katiba ambayo:

  “…………Ina lengo la kushi miaka kadhaa ijayo, na kwa hivyo iwe inaweza kuhimili misukosuko kadhaa ya binaadamu”.

  Lakini ili nisipotoshe maana halisi aliyoielezea Bw. Johm Marshall, yeye alisema kwa lugha ya Kiingereza kuwa:

  “Our constitution ………….is a Constitution intended to endure for ages to come, and consequently to be adapted to the various crises of human affair”

  Sasa basi Katiba yetu ya Tanzania na kwa maana pana Katiba ya nchi nyengine yoyote, ambayo ni sheria mama ya nchi,lazima ilenge huko alikokuona Bw. Jonh Marshall. Inatakiwa iwe inakidhi haja ya mabadiliko ya nchi kisiasa na kiuchumi. Inatakiwa iwe ni nyumbufu (flexible) kukubaliana na ukuwaji wa mabadiliko kadhaa ya taifa husika, na wakati huo huo misingi yake mikuu iwe bado inaongoza taifa hilo na watu wake bila ya kutetereka.

  Katiba nzuri ya nchi, na ambavyo ndivyo inavyotakiwa iwe, ni kama ile aliyoielezea Jaji Sower katika kesi ya Tuffuor v. A. of Ghana – (1980) A.G. 637, 674 kwamba Katiba ya nchi ni chombo ambacho kinakidhi matakwa ya wananchi na kwamba vile vile inaonesha historia yao. Hivyo basi katiba yoyote ile nilazima itizamwE kuwa ni dira, na ni:

  “…………..alama muhimu (land mark) katika kuwaoneshea watu njia ya maendeleo. Ndani yake mna tama na malengo (hopeS and aspirations) kwa kupata maisha mazuri. Katiba ina misingi yake ya sheria (its letter of the law) na ina malengo yake (its spirit). Katiba ndio kichwa cha mikondo mitatu ya utawala ambapo kila mkondo unafanya wajibu wake………..na uwezo wao unatokana na Katiba hiyo, Katiba inaelezea pia namna ya kuibadilisha……..kwa maana hiyo lugha inayotumika katika Katiba ni lazima iwe ina fikiriwa kama ni kitu kinachoishi (living organism) ambacho kinakua na kuendelea……..(capable of growth and development”).
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Jee Katiba zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar zinakidhi yote hayo tuliyelezea, ambayo ni muhimu kuwemo katika Katiba ?
  Jee!, wakati wa kuandikwa Katiba hizi zilipata idhini ya watu wenyewe?. Jee! Katiba hizi zinalinda maslahi ya watu na mfumo wa vyama vingi, au kulinda haki za binaadamu au utawala wa sheria? Yote hayo ni mambo ya kujiuluiza; na ikiwa jibu halioneshi kuwa ni ndio, basi Katiba hizi zitakuwa hazikidhi ule msemo maarufu wa kidemokrasia uliomo ndani ya Katiba wa kwamba ni watu wenyewe ambao wameiandika Katiba yao. Hivyo basi kukosekana kwa mambo hayo kunaonyesha wazi umuhimu wa kuwa na Katiba mpya ili kuwekeza mambo mepya.

  KUNA HAJA YA KUWA NA MABADILIKO YA KATIBA ?

  Kitu cha mwanzo cha kutizama katika utaratibu wa mabadiliko ya Katiba ni kujuwa maeneo ya mabadiliko ya Katiba pamoja na umuhimu wake ili mabadiliko hayo yafanyike vizuri. Malengo yanayotaka kufikiwa lazima yaonekane na yakubalike. Wananchi hawatokubali mabadiliko yoyote ikiwa malengo hayo hayakuainishwa ipasavyo. Kwa hivyo ni lazima kuwe na makubaliano ya Kitaifa katika mabadiliko yoyote yale ya Katiba. Hapa tunasisitiza umuhimu wa kushirikishwa wananchi walio wengi. Suala hapa ni wananchi na si vyama au itikadi za vyama.

  Ulazima wa mabadiliko ni lazima uwe unalazimisha haja hiyo, uwe halali na ukubalike. Wakati wa mabadiliko hayo lazima uwe muafaka na wananchi lazima wakubali kwamba wakati sasa umefika kuwa na mabadiliko. Shauku ya mabadiliko inaweza kuanzishwa na viongozi lakini ni lazima baadae ichanuwe kutoka kwa watu wenyewe kwa nyakati maalum ambazo ni nzuri kwa mabadiliko ya Katiba. Nyakati hizo muafaka ni pamoja na nyakati zinazokuwa zimeiva kwa mambo hayo, ambapo ni mara:

  Baada ya vita ,baada ya mapinduzi ,baada ya muungano wa nchi mbili au zaidi, baada ya mabadiliko ya kisiasa katika nchi,baada ya mabadiliko ya mfumo wa kisiasa kutoka chama kimoja kwenda vyama vingi au baada ya kutoka mfumo wa kijeshi uliopo katika nchi kwenda katika utawala wa kidemokrasia.


  Haya ni miongoni mwa mambo ambayo yanapalilia kwa nguvu kubwa sana sababu za kuwepo au kutungwa kwa Katiba mpya ya nchi kutokana na Katiba iliorithiwa. Nchini Uganda kwa mfano, matayarisho ya Katiba mpya ambayo ingeweza kusahihisha makosa yaliyopita kama walivyodai wanachi ilikuwa ni suala la mwanzo katika ajenda za NRM (National Resistance Movement. Kenya vile vile mabadiliko ya Katiba yalikuwa ni ajenda kubwa wakati wa vyama vingi hadi kufikia kuandikwa kwa rasimu ya Katiba ya Kenya iliojuilikana kwa jina maarufu la Katiba ya Bomas. Afrika ya Kusni nayo walilazimisha kuwa na Katiba mpya baada ya mabadiliko makuhwa ya kisiasa yaliyotokea. Mabadiliko yote hayo yana lengo moja tu, la kuiweka nchi iwe na Katiba ya Kidemokrasia ili vyombo vitavyofanya kazi kwa mujibu wa Katiba hiyo view na ufanisi mzuri wa shughuli za uendeshaji pamoja na kuleta maendeleo ya nchi kwa faida ya watu na nchi husika. Lengo hapa ni lile lile alilolielezea Jaji Sawyer la kuwa na utaratibu mzuri wa utawala wa nchi kwa faida ya nchi na wananchi.

  Ni muhimu kujuwa lengo la mabadiliko hayo ya Katiba pa moja na kujuwa mipaka yake kwa madhumuni ya kuwa na mkakati halisi na njia nzuri za kufanya mabadiliko hayo. Wakati mwengine inaweza ikawa ni muhimu kuifuta Katiba yote na kuiandika upya, lakini wakati mwengine Katiba ya zamani inaweza ikafanyiwa baadhi ya marekebisho na kubakia ile ile. Hata hivyo pale unapokuwa na Katiba ambayo imeshajaa viraka vya mabadiliko basi lazima sasa katiba hiyo ifanyiwe marekebisho kwa kuiandika upya. Hata hivyo katika msingi ya nchi ambazo zimeungana na baadaye kuwa nchi yenye mfumo wa vyama vingi, basi ni vyema Katiba yote ikabadilishwa, kwa maana ya kuzingatia muungano huo pamoja na matakwa ya siasa ya vyama vingi. Hapo tunaweza tukaweka maudhui yetu wenyewe ndani ya Katiba hiyo kwa mujibu wa siasa zetu, utaratibu wetu na mipango yetu tunayohisi yatafaa na kusaidia. Tukifanya hivi tunaweza kujisifia kusema kwamba Katiba yetu ni Katiba yenye mizizi yake nyumbani kwetu (home grown). Wenzetu wa Guyana walifanikiwa kuwa na Katba waliotayarisha wao wenyewe bila ya kutegemea sana kutoka katika Katiba za nchi nyengine. Na Katiba hiyo ilisaidia sana kuijenga Guyana mpya kwa misingi ya ujamaa waliyokuwa wamejiwekea.

  Je WaTanzania tunasubiri nini ? Mfumo wa vyama vingi umeingia miaka kumi na tano iliyopita Sultani CCM amebana kimya ni lazima akurupushwe la si hivyo tutashindwa kujenga hata ukuta maana tunaona mambo yanavyoendeshwa bila ya kuwa kikomo kila siku yanazidi ,Katiba tuliyonayo imezidiwa nguvu na wafuasi wa Sultani CCM lazima ibadilishwe na wakati ni huu hakuna kusubiri tena wala hakuna wa kusema hakuhitajiki KATIBA MPYA anaesema hivyo ni adui wa Taifa hili yeye na mayai yake.
   
 3. M

  MchungajiMakini Senior Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Apr 4, 2008
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sisi wazanzibar tunachoomba ni kudai uzanzibar wetu na wabara warejeshwe makwao pamoja na wahamiaji wengine.
  na kama kwenu bara kuna wzanzibar warejeshwe kwao?

  hiyo katiba mukishaibadilisha hili ndio tunalitaka na sisi.

  kwa kun muungano ya serikali mbili ya muungano na smz.

  munatuumiza jamani
   
 4. Mzee wa oldadai

  Mzee wa oldadai Senior Member

  #4
  Sep 14, 2017
  Joined: Oct 23, 2016
  Messages: 187
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 60
  Wadau wasalam!!

  Nimekaa nimetafakari sana,nikajiuliza mbona wakenya wameweza kudai katiba mpya wakapata,tumehuru ya uchaguzi wakapata,wakapinga matokeo ya Rais Kenyata wakashinda,kwa nini sisi Watanzania tushindwe?
   
 5. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2017
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mlipata nafasi nzuri sana kwenye ile rasimu[ingawa haikuwa perfect] mkaitupilia mbali kwa kuhamishia kwenye uchaguzi kupitia ukawa na kwa sasa sidhani kama ipo kwenye ajenda
   
 6. Lizarazu

  Lizarazu JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2017
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 3,471
  Likes Received: 3,402
  Trophy Points: 280
  Hili suala haliwezi likawezekana hivi hivi tu, linahitaji sacrifice sasa Je, ni nani na nani ambao wako tayari kuweka rehani maisha yao hili katiba mpyaa ipatikane kwa manufaa ya watakao baki na vizazi vijavyo!?
   
 7. Lizarazu

  Lizarazu JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2017
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 3,471
  Likes Received: 3,402
  Trophy Points: 280
  Kwa Tanzania jinsi ilivyo na watanzania wallivyokuwa na roho za kuku, Magufuli akiamua kutawla miaka 40 anaweza tena bila kubughidhiwa.
   
 8. A

  ARDEAN Member

  #8
  Sep 19, 2017
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Vh7Jon
   
 9. mop

  mop JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 744
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 80
  Katiba mpya si kipaumbele cha Watanzania, Watanzania wanahitaji maendeleo na siyo makaratasi eti katiba
   
Loading...