Watanzania tuamke, tuache mazoea ona tunavyoteseka hatua za mwishoni

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Wakati Serikali inatangaza suala la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole (biometric) wengi walipuuzia wakijua ni nguvu ya soda, wakiamini serikali haiko serious.

Pia wapo walioamini kwamba muda ni mrefu hivyo hawakua na haraka yoyote, Waliendelea na majukumu yao mengine japo kuna wakati walipata muda wa ziada kutekeleza jambo hilo,ispokua hawakuona umuhimu wake.

Wapo wengine waliona umuhimu wa kufanya jambo hilo na walilitekeleza mapema sana kukwepa usumbufu huu unaojitokeza kwa sasa.waliwahi mapema. kuweka taarifa zao sahihi sehemu husika,ukiacha wale ambao uhamiaji waliwatilia shaka uraia wao.

Na ifahamike kwamba wengi wameanza kumuelewa Rais Magufuli anamanisha ya kile anachokisema.

Ndio maana baada ya yeye kusajili kwa alama za vidole na kutoa tamko lake la kuongeza siku 20 ,hapo ndipo baadhi yetu tukashituka kujifunika shuka kukiwa kumekucha.

Zipo changamoto mbalimbali upande wa wadau wote kwa maana ya wananchi, NIDA na idara ya uhamiaji katika kutimiza majukumu yao hili sipingani nalo.

Sidhani toka tangazo litoke kama ulikua serious ndani ya miezi mitatu kuweka taarifa zako sahihi uhamiaji na Nida kuhakikisha unasajili laini biometric dhahama hii ingekukuta,japo kuna wengine baadhi si makosa yao bali ni idara husika kukwamisha zoezi hili.
hapa naongelea wale wazee wa kupuuza.

Niwaombe watanzania muda huwa ni mchache siku zote ,hivyo ni muhimu kuutumia accordingly, tusome alama za nyakati hii ni awamu ya tano ,"it walks the talk"

Mwisho niwape pole wale ambao wanahangaikia namba zao za vitambulisho si kwa makusudi yao ,bali ya uzembe wa wengine.

Na Pia niwakumbushe wale wenzangu na mimi kila kisemwacho wao hu ignore ,mwishoni ndio huanza kuchakalika na kutupa lawama huku na kule wakati walipuuza zoezi.

Rais Magufuli kaongeza muda wa kusajili biometric mara mbili,je ataongeza mara ya tatu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ina 'walk the talk' mbona milioni 50 za kila kijiji hatujapata?
 
Kwa taarifa yako hata sisi tuliosajili mapema bado tulipata usumbufu usio wa kawaida, zoezi hilo kwenye kila eneo lililokuwa linafanyika ndani ya wiki mbili, misururu ilikuwa mirefu kiasi kwamba mtu uliweza hata kupoteza siku 2 bila kufanikiwa. Usimtaje rais hapa maana hata yeye alichelewa kujiandikisha, na kama alitaka ajue madhara ya kuchelewa kujiandikisha au hata adha ya zoezi zima, na yeye angefika apange mstari. Kwa ujumla hilo zoezi linaendeshwa kijima mno. Mbona baada ya kupata kitambulisho au namba, huko kwenye makampuni ya simu hakuna huo usumbufu wa kijima?
 
We sema tu umeandika kumsifia Magufuli kwamba "He walks the talk".

Lakini kumbuka watanzania tumezoea michaka michaka ya dizaini hii si katika serikali ya awamu ya tano peke yake na sio kweli kwamba awamu zilizopita zilikuwa haziko serious katika kampeni zake na kwamba eti tulikuwa tunadekezwa.

Kumbuka "mziki" wa mabadiliko ya mfumo wa luninga kutoka analojia kwenda dijiti (huna king'amuzi, hupati habari), usajili wa Line za simu kwa vitambulisho vya mpiga kura au lesini za udereva (huna kitambulisho, huna mawasiliano), lakini kumbuka pia "mziki" wa kuzima simu feki. Hayo yote yalitekelezwa kikamilidu na serikali ya awamu ya nne na wala hakukuwa na "unseriousness" na wananchi tumeshazoea. Wacha tu wazime simu zao.
 
Kwa taarifa yako hata sisi tuliosajili mapema bado tulipata usumbufu usio wa kawaida, zoezi hilo kwenye kila eneo lililokuwa linafanyika ndani ya wiki mbili, misururu ilikuwa mirefu kiasi kwamba mtu uliweza hata kupoteza siku 2 bila kufanikiwa. Usimtaje rais hapa maana hata yeye alichelewa kujiandikisha, na kama alitaka ajue madhara ya kuchelewa kujiandikisha au hata adha ya zoezi zima, na yeye angefika apange mstari. Kwa ujumla hilo zoezi linaendeshwa kijima mno. Mbona baada ya kupata kitambulisho au namba, huko kwenye makampuni ya simu hakuna huo usumbufu wa kijima?
Wapo vijana wanapita hadi bar wanatafuta watu wa kuwasajili. Zoezi hili ni gumu kwa asie na kitambulisho cha taifa tu
 
Wakati Serikali inatangaza suala la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole (biometric) wengi walipuuzia wakijua ni nguvu ya soda, wakiamini serikali haiko serious.

Pia wapo walioamini kwamba muda ni mrefu hivyo hawakua na haraka yoyote, Waliendelea na majukumu yao mengine japo kuna wakati walipata muda wa ziada kutekeleza jambo hilo,ispokua hawakuona umuhimu wake.

Wapo wengine waliona umuhimu wa kufanya jambo hilo na walilitekeleza mapema sana kukwepa usumbufu huu unaojitokeza kwa sasa.waliwahi mapema. kuweka taarifa zao sahihi sehemu husika,ukiacha wale ambao uhamiaji waliwatilia shaka uraia wao.

Na ifahamike kwamba wengi wameanza kumuelewa Rais Magufuli anamanisha ya kile anachokisema.

Ndio maana baada ya yeye kusajili kwa alama za vidole na kutoa tamko lake la kuongeza siku 20 ,hapo ndipo baadhi yetu tukashituka kujifunika shuka kukiwa kumekucha.

Zipo changamoto mbalimbali upande wa wadau wote kwa maana ya wananchi, NIDA na idara ya uhamiaji katika kutimiza majukumu yao hili sipingani nalo.

Sidhani toka tangazo litoke kama ulikua serious ndani ya miezi mitatu kuweka taarifa zako sahihi uhamiaji na Nida kuhakikisha unasajili laini biometric dhahama hii ingekukuta,japo kuna wengine baadhi si makosa yao bali ni idara husika kukwamisha zoezi hili.
hapa naongelea wale wazee wa kupuuza.

Niwaombe watanzania muda huwa ni mchache siku zote ,hivyo ni muhimu kuutumia accordingly, tusome alama za nyakati hii ni awamu ya tano ,"it walks the talk"

Mwisho niwape pole wale ambao wanahangaikia namba zao za vitambulisho si kwa makusudi yao ,bali ya uzembe wa wengine.

Na Pia niwakumbushe wale wenzangu na mimi kila kisemwacho wao hu ignore ,mwishoni ndio huanza kuchakalika na kutupa lawama huku na kule wakati walipuuza zoezi.

Rais Magufuli kaongeza muda wa kusajili biometric mara mbili,je ataongeza mara ya tatu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa faida ya Watanzania anaweza kuongeza na ndio maana anaitwa Rais, ana mamlaka ya kuweza kufanya uamuzi huo akitazama uhalisia,ila mimi naomba asimtumbue mkuu wa NIDA hili zoezi ni zito..najua waliosajili kama wewe mnashangilia kimoyo moyo tufungiwe laini utafikiri kuna mapambano hiyo haitasaidia..Kwa sasa ni swala Mh.Rais, TCRA na NIDA kupima uitikiaji wa watu katika kujisajili, na kutathmini wataamua nini..sisi wananchi tunasubiria..
Tambua usajili utakuwa na asili ya zoezi endelevu maana laini inaweza kufa,siku kupotea,waweza kuhamia TTCL siku yoyote ukaaachana na mtandao usio na GB za kutosha..kitu cha msingi kila Mtanzania ahakikishe anapata kitambulisho chake na kuheshimu taratibu za mawasiliano.
 
Kwa taarifa yako hata sisi tuliosajili mapema bado tulipata usumbufu usio wa kawaida, zoezi hilo kwenye kila eneo lililokuwa linafanyika ndani ya wiki mbili, misururu ilikuwa mirefu kiasi kwamba mtu uliweza hata kupoteza siku 2 bila kufanikiwa. Usimtaje rais hapa maana hata yeye alichelewa kujiandikisha, na kama alitaka ajue madhara ya kuchelewa kujiandikisha au hata adha ya zoezi zima, na yeye angefika apange mstari. Kwa ujumla hilo zoezi linaendeshwa kijima mno. Mbona baada ya kupata kitambulisho au namba, huko kwenye makampuni ya simu hakuna huo usumbufu wa kijima?

Magufuli hakusajili sku ile,magufuli hatumii laini za 32K na hakuna raisi anazitumia izo ni za wananchi! wala magufuli hatumii mitandao ya simu za biashara anaweza kufanya ivo tu kama anataka kujihakikishia kitu flan kwenye hio mitandao! kiukwel

hakuna sehem hakuna changamoto, hata mm nlipata changamoto wkati wa kusajili ila baada ya kupewa muongozo wa apa na pale nlifanikisha, imefika mpaka hatua watu wa usajili wanawafuata watu mitaani kuwasajili watu, sasa ikifungwa ni halali kabisa, siku nlienda kupata namba yangu ya NIDA nlienda na dogo mmoja ambae ndo kaingiza 18 mwaka jana na alipewa fomu kajaza mwezi uliisha alikuja na akapata namba,na akasajili laini yake! kiukwel tumezidi kupuuzia mambo, kwa mtu anaeona umuhimu wa mawasiliano angekua ashamaliza kabla ata ile awamu ya kwanza kuisha, hata kama taarifa zako hazikuonekana ungepewa fomu mpya ujaze, na ungezirudisha mwishowe ungepata namba yako na ungesajili
 
Ok kuwa Magufuli hatumii line hizi za simu za kawia kwangu ni elimu mpya, nashukuru kwa elimu hiyo maana sikuwa na ufahamu wa hilo. Je siku ile alienda kufuata nini na kusema amesajili line yake, au ndio mambo ya kutia hamasa na kuongeza msisitizo?

Ni kweli hakuna sehemu hakuna changamoto, ila hivi vitambulisho vya NIDA sio changamoto tena bali ni uzembe wa hali ya juu. Hayo mambo ya NIDA tumeanza kuyasikia miaka minne nyuma toka enzi za akina Mwaimu. Muda wote huo ni changamoto? Wengi wetu mpaka tunayozungumza hatuna nakala halisi za hivyo vitambulisho zaidi ya namba tulizopata mitandaoni. Yote hayo ya kutopata hata hizi nakala ni changamoto au uzembe tu kwa kichaka cha changamoto. Mfano halisi mimi nilijisajili mwaka jana mwezi wa nne, mpaka leo sijapata nakala ya kitambulisho, je hiyo ni changamoto tena au uzembe?
 
Na mimi nimeandika ugumu upo kwa wasio na NI card.
Haraka haraka haina baraka..zoezi la usajili bado linahitaji hamasa na muda.Kuna watu washakata tamaa na mambo mengi kiasi hawahitaji shinikizo bali nafasi inapokuja na urahisi wa jambo/huduma kufanyika ndio husababisha wao kuitikia zoezi..Huwezi amini kuna watu wazima wengi tu hawajawahi ata kwenda NIDA kujaza fomu na wametulia tu! hamasa bado inahitajika..
 
Mbona sijaona kitu tofauti na kumsifia huyo Mungu wako!?

Nilipoona hapo kwenye "awamu ya tano" nikakupuuza kabisa. Nimejikaza sana kusoma mpaka mwisho!

NIKUELIMISHE: Mpaka muda huu, Bunge lilipaswa kuwa limetunga sheria za usajili wa laini za simu, na wakati huo huo TCRA kupitia waziri mwenye dhamana, ilipaswa kuwa imetunga kanuni husika.

Hatuwezi kuishi kwa hisani za magufuli. Leo akiamka aseme "zima laini zote"; kesho kutwa akiamka kichwa imekaa sawa aseme "nawapa fadhila ya siku kumi zaidi". HAPANA.

Tunalo bunge na tunavyo vyombo vya udhibiti na utoaji huduma. Swala la usajili wa laini za simu sio matakwa au zawadi za Rais.

Mpaka muda huu najiuliza, magufuli anapata wapi mamlaka ya kutoa hisani za kuongeza muda au kuamrisha laini zifungwe?

Yeye ni sultan au ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili zoezi linahitaji muda ,serikali ifanye tathimini ya faida na hasara zake kabla ya kuzifungia line za simu ,utulivu ni muhimu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, bahati mbaya sana hii nchi kila jambo huwa kukurupuka, mamlaka zenyewe zinafanya kazi za hovyo, hawana mifumo ya kurahishsha zoezi, zoezi hili linatakiwa lipewe muda zaidi kwa sababu serikali hii ya ovyo na mambo yake ya hivyo hivyo, kama hawawezi kuongeza miezi sita mingine basi wafunge tu hizo lines, tutakuwa tunatumia simu za kuazima, watu wengi wansumbuliwa kila siku ukienda unaambiwa hivi kesho unaambiwa vile, kiujumla mambo yako ovyoovyo sana, nasikitika kuoona watu wanashabikia eti awamu ya tano as if ndio tumepata uhuru leo, wafnge tu hizo line tusisumbuane hapa, kwanza sio lazima kutumia simu, kama hawataki watu tutumie simu, ama la tutasajiri line za Kenya au Uganda, kila kitu kukurupuka tu.
 
Ilinichukua miaka 6 kupata kitambulisho yaani nilijiandikisha 2012 nikapata mwaka 2018 binafsi sina hamu nao hao jamaa, yaani nilipata mateso makali sana
Utashangaa mtu anashangilia eti serikali ya awamu ya tano !!, wewe miaka 6 unasubiri ID !!
 
Back
Top Bottom