Cheef Baroka
JF-Expert Member
- Apr 28, 2019
- 491
- 1,000
Pole sana kak.. nahisi hii ni baada yakutambulishwa MAKAMBO badala ya Fundi Banda .Wakati mwingine kuna ujinga na upumbavu unaletwa na mihemko hasa ya wachambuzi wa michezo ambao mimi sijawahi kuwaekewa kabisa hapa nchini.
Hizi sifa za Banda ni kama zimetiwa chumvi mno. Kama kweli angekuwa na uwezo unaoimbwa leo, kwa nini vilabu tajiri vya Ulaya, Uarabuni, South Afrika hawajamuona? Tuacheni kuwa obsessed na mchezaji mmoja kwa sifa za kizushi zilizopitiliza.
Miqueison alikuwa mchezaji bora sana binafsi nadiriki kusema ni moja ya wachezaji adimu sana kwenye soka.
Lakini hawa wachambuzi wanaotuhadaa na Banda.. Banda ..walimuona wa kawaida sana.Hata walipokuwa wakitaja wachezaji wao bora ilikuwa nadra kusikia akitajwa.Leo hii anahitajika na club tajiri inayoujua mpira.Baada ya yeye kwenda ndipo utasikia sifa zinamimika sana.
Watanzania tumekuwa wapumbavu sana linapokuja suala la soka.
Kuna timu inasajili mwonekano wa kimpira na si uwezo wa kucheza.Wakiona mchezaji anatengeneza nywele tu iwe bleach au dreads anasajiliwa kwa sifa zote.Mwisho wa siku wanakuja kulia na tff.
Tuacheni maneno maneno,hasa ninyi wachambuzi maandazi.Kama mlikuwa hamumuelewi Miqueison mnawezaje kuelewa mchezaji mzuri?
Nyie msioelewa ubora wa Morrison mnawezaje kuona mchezaji mzuri?
Nyie mnaobeza wachezaji kama Chama,Bwalya,Mugalu,Boko,na wengine wengi wa Simba mnawezaje kuona wachezaji wazuri?
Nyie mlioshindwa kuona intellect ya Carlinno mnawezaje kuona mchezaji bora?
Nyie mnaoona Ninja ni beki bora tunawaaminije kuwa mnajua kuona vipaji vya wachezaji bora?