#COVID19 Watanzania tuache uzushi dhidi ya chanjo ya COVID -19, Je mchango wetu ni upi katika kukabiliana na hili janga?

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,454
2,115
Mlipuko virusi vya korona mwishoni mwa mwaka 2019 umebadili kabisa mifumo ya maisha duniani. Ugonjwa huu umesabababisha athari kubwa sana katika kila sekta pamoja na kugharimu maisha ya watu. Nikutokana na athari hizo ndiposa wataalamu wengi wamekuwa wakisumbua vichwa kutafuta suluhisho ili kuokoa maisha ya watu. Shirika la afya duniani na mamlaka za madawa zimekuwa zikifuatilia kwa karibu gunduzi za chanjo mbalimbali na kuziidhinisha zile zilizoonekana faafu kwa matumizi ya binadamu na mpaka sasa chanjo mbalimbali zimeshaidhinishwa na kuleta matumaini kiasi yakutokomeza janga hili duniani.

Wakati mataifa makubwa yakipambana kutafuta suluhisho la janga hili la kiulimwengu hali nitofauti katika mataifa madogo. Kumekuwepo na baadhi ya watu wanaohusisha chanjo za Corona na kile kinachozungumzwa katika biblia "ufunuo wa Yohana na chapa ya mnyama 666. Huo ni uzushi mkubwa kwani matumizi ya chanjo yamekuwepo tangu karne ya 16 na hii sio chanjo ya kwanza kugunduliwa. Hata hivyo kile kinachozungumzwa katika ufunuo ni chapa iwekwayo katika paji la uso au katika bega, je chanjo yafaa kuwekwa katika paji? Biblia inafafanua zaidi kuwa hesabu yenyewe ni yakibinadamu, je katika chanjo kuna namba 666? Sitaingia sana kulichambua hili lakini wenye imani hii wanapaswa kujua chapa ya mnyama nikinyume cha chapa ya Mungu.

Chanjo ya corona nilengo la wazungu kuwauwa wa Afrika, huu ni uzushi mwingine mkubwa unaoendelea kushamiri miongoni mwa watu fulani wenye nia ya kupotosha. Swali dogo la kujiuliza je kufa kwetu au kuishi kwetu ni kupi kutawapa faida zaidi? nafikiri uzushi huu au kuendekeza hoja hii ni ukosefu wa maarifa unaovuka mipaka. Ni miaka 60 tangu tumepata uhuru, tunazo taasisi za elimu na afya zenye waalamu wa ndani, je kupitia wao wanashindwa kubaini athari zozote zitakazo onekana katika chanjo hizo?

Rai yangu nikwamba tuungane kwa pamoja kutafuta suluhisho la tatizo hili, tunao wataalamu na vyuo vikubwa vinavyoweza kutoa chochote tukamaliza hili tatizo kuliko kutegea mataifa makubwa huku tukiwa na hofu ya kuuawa na wazungu.

MWISHO "Tusikubali kurithisha ugonjwa huu kwa vizazi vijavyo''.
 
Back
Top Bottom