Watanzania tuache unafiki, tuwajibike Kama tunataka kukabiliana na COVID 19

Just Distinctions

JF-Expert Member
May 5, 2016
2,690
5,315
Habari wa wakati huu wakuu, tangu janga hili la Corona litukumbe Tanzania kama ilivyo nchi zingine duniani kote kumekuwa na maoni mbalimbali ya watu wakitaka hatua madhubuti zichukuliwe ili kukabiliana na janga hili ikiwamo kuzuia mikusanyiko na misongamano isiyo ya lazima, kufunga shughuli zote ambazo zinahusisha muingiliano wa watu mbalimbali kama shule, kuweka vifaa vya kujikinga na kupunguza maambukizi, na wengine wakaenda mbali zaidi kuwe na zuio la kutotoka ndani kabisa ili kupunguza kusambaa kwa gonjwa hili la hatari.

Baadhi ya hatua zimechukuliwa na serikali kama ambavyo imetangazwa na wote tumeshuhudia kama kusimamisha michezo, kufunga vyuo na shule n.k na baadhi ya hatua pia bado serikali haijafanya hivyo kama kuweka zuio la kutotoka majumbani kama nchi jirani.

Kitu kinachonishangaza ni kuwa Watanzania elimu ya corona tumeipata na njia za kujikinga tunazijua lakini kwa nini kila kitu tulaumu serikali? wewe unajua corona inasambaa baki nyumbani!, ila sasa asilimia ya watu wengi hata humu jamii forum wanasisitiza serikali iweke "lockdown" ilihali wao bado wanafanya mizunguko na wanaenda mjini kama kawaida.

Kujikinga na kuzuia maambukizi kunaanza na wewe, ikiwa wewe hutaki kufanya hivyo mpaka serikali ikulazimishe huo ndio unafiki tunaouzungumza, lockdown inapaswa ianze na wewe kukaa nyumbani na familia yako. sio kulalamika kwenye mitandao ya kijamii serikali iweke zuio ilhali wewe ndio bingwa wa kufanya mizunguko hapa mjini.

Kuwajibika ni kwa wewe kuchukua hatua stahiki sio mpaka ulazimishwe ndio iwe na mashiko inapaswa ujilazimu wewe mwenyewe. inashangaza wale wanaopigania serikali iweke zuio la kubaki majumbani ndio tunapishana nao kila siku mijini sasa mna tofauti gani na wale wasiotaka liwepo hilo zuio?

Mwisho ningependa kuwasihi waTanzania wenzangu, tuchukue tahadhari kwa kujikinga na gonjwa hili na pia tutumie muda huu ambao bado shughuli za kiuchumi hazijasimama kuweka akiba ya fedha na vingine vya muhimu kadri vile inavyowezekana ili kujipanga kwa yote yajayo kwani tuendako changamoto zitazidi kuongezeka. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari kweli, nikipita barabarani naona wengi walioko kwenye usafiri binafsi wamevaa mask, japo unakuta mtu yuko peke yake ndani ya gari; but wakina sisi kwenye daladala utakuta hakuna hata mmoja aliyevaa mask, japo wote tunajua Corona ipo na mbinu za kujikinga tunazifahamu.

Inawezekana Corona imekuja kupunguza idadi ya wajinga duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka sana, uko wanakoenda wenye magari ndo penye hatari ya ilo gonjwa
Hatari kweli, nikipita barabarani naona wengi walioko kwenye usafiri binafsi wamevaa mask, japo unakuta mtu yuko peke yake ndani ya gari; but wakina sisi kwenye daladala utakuta hakuna hata mmoja aliyevaa mask, japo wote tunajua Corona ipo na mbinu za kujikinga tunazifahamu.

Inawezekana Corona imekuja kupunguza idadi ya wajinga duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah imenibidi nicheke japo inasikitisha sana ila ndio ukweli tulionao, watanzania hatujali tunachukulia poa sana kila kitu kuna watu mpaka hawaamini kama corona ni tishio wanaona ugonjwa flani wa kawaida sana.
Hatari kweli, nikipita barabarani naona wengi walioko kwenye usafiri binafsi wamevaa mask, japo unakuta mtu yuko peke yake ndani ya gari; but wakina sisi kwenye daladala utakuta hakuna hata mmoja aliyevaa mask, japo wote tunajua Corona ipo na mbinu za kujikinga tunazifahamu.

Inawezekana Corona imekuja kupunguza idadi ya wajinga duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app

aim for the stars
 
Back
Top Bottom