abdulrahim
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 408
- 286
Namshukuru mungu muumba mbingu na ardhi kwa pumzi niliyonayo mpaka wakati huu! katika kusoma kwangu historia ya nchi yangu pendwa Tanzania Mwl. JK Nyerere alitangaza vitaa kwenye maswala matatu amabyo ni Ujinga, Maradhi na Umasikini...
Kwa bahati mbaya ile vita imepiganwa kwa miongo mingi lakini wale maadui mpaka sasa wanaendelea kuitafuna Tanzania nchi yangu...
Baadae akaongezeka adui mwingine ambaye ni Rushwa..Lakini nae ametuzidi mpaka sasa anaendelea kuitafuna Tanzania yetu...
Kwa upambanuzi yakinifu nilioufanya kwa kuishi kwangu Tanzania na kuwa Mtanzania nimegundua tumeshindwa kupambana na haya yote kwasababu sisi watanzania ni WANAFIKI.
Penye mnafiki ni ngumu baraka ya mungu kufika ila kwakuwa mungu wetu anatupenda na anaitakia mema nchi yetu imeendelea kuwapo.
Raisi mstaafu wa Awamu ya nne alipoingia madarakani aliahidi kuwa atakula sahani moja na Majambazi kwani tulishuhudia wakati anaingia madarakani alikumbana na wimbi la ujambazi.
Task force iliundwa kwa ushirikiano wa vyombo vyetu vyote vya Ulinzi na Usalama na kwakweli ujambazi wa kutumia silaha mpaka kiongozi huyu anaondoka madarakani ni kweli janga hili lilipunguzwa saana mpaka sasa tukawa na vibaka wadogo wadogo wa mapanga(Panya road).
Nimeshuhudia majambazi sugu wengi wakiuliwa tena sio eneo la tukio kwa mfumo wao waliokuwa wanaujua wao.Waliosalimika mpaka sasa wako jela na wale waliobakia mtaani wengine waliikimbia inchi na wengine wakaingia kwenye mfumo mwingine wa maisha..Lakini sikupata sikia watanzania wakipongeza juhudi zile.
Task force ya Ujambazi ilifanikiwa kwasababu kazi yao ilifanywa kuwa weledi mkubwa saana pasipo ingiliwa na Wanasiasa na ndio maana ilikuwa kimya kimya unasikia tu mtaani jambazi fulani kakamatwa baada ya siku kazaa unasikia lile jambazi liko mochwari na file linafungwa amani inatawala.
Lakini sasa vita hizi za sasa, nikianzia na UFISADI, Kiongozi wetu mkuu wa nchi wa sasa Mh. JPM amedhamiria kwa dhati kuhakikisha janga hili linapotea lakini sasa limekutana na adui mwingine ambaye ni UNAFIKI.
Baada ya mafisadi kubanwa wanasiasa hao hao wananza lalamika hali ya maisha imekuwa ngumu ..
Ukweli kabisa mimi ni Mfanyakazi ninayetoka nyumbani 0515hr na kurudi 1730hr kwenda kibaruani kwangu sijaona badiliko la ugumu wa maisha au wepesi hali iko pale pale sema ile pesa ya mtaani(Pesa ya mazabe )imepotea kwa kuminywa kwa mianaya ya ufisadi na ndio maana malalamiko ya hali ngumu ya maisha imekuwa ikisikika kama kelele za daladala kkoo.
Wimbo wa wimbi la madawa ya kulevya TZ haukuanza kuimbwa leo(Waliotajwa woote ama ni Watumiaji/Wasambazaji/Wauzaji/Wamiliki) hakuna aliyetajwa kwa kuonewa(kwasababu mimi si Mnafiki), lakini nashangazwa na aina ya taskforce inayoshughulikia jambo hili. Je ni kweli wamedhamiria kuokoa watanzania dhidi ya madawa ya kulevya kama ilivyofanikiwa kutuokoa kwenye janga la majambazi ya kutumia silaha?
Ninachokiona sasa ni UNAFIKI mkubwaa tena Unafiki wa sasa una timu mbili ambazo zote ni za kinafiki. Timu Ba imeamua kupambana na jambo hili si kwa dhamira ya kuliteketeza bali ni kwa dhamira ya kuonyesha kwamba walijenga bwawa la kuogelea lakini kwa bahati mbaya mvua haikunyesha. Na Timu Be imeamua kuipinga Timu Ba kwakuwa tu Timu Ba inatengeneza njia ya kujiweka mazingira mazuri kwenye ligi..
Mwisho kabisa napenda kumalizia kwamba hizi vita za Ufisadi na Madawa ya Kulevya naomba vishughulikiwe kama ilivyokuwa inashughulikiwa swala la Ujambazi.. Japo nimesikia ile Ant Robbery Task force imeshirikishwa ila sina uhakika kama imepewa baraka kama walivyopewa kwenye Ujambazi. Na pia tujifunze kuachana na unafiki tujitahidi kuwa wakweli zaidi...Mtaani tunasema MWENDA CHOONI ANA HAJA ZAKE!!!!!!