Watanzania tuache tabia hii mbaya

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Unakuta Rais au kiongozi anahojiwa mfano na CNN na yeye anajibu kwa kingereza. Huu ni upuuzi, kwani huna lugha nyingine unayo jua? Unatakiwa umjibu kwa lugha yako mama.

Mjibu hata kwa kisukuma hata akitumia miaka miwili kupata tafsiri sawa tu kwani lazima kutumia lugha yao. Sembuse tuna lugha ya kiswahili na bado hatutaki kutumia. Lazima kuonyesha jeuri.

Kuna watu wanajisikia vibaya kutojua kingereza, mbona hujisikii vibaya kuto jua kichina.Mbona wafaransa wanajibu kwa kifaransa au nani alita sheria ya lugha nyingine isitumike kama sio kuendeleza kututawala.

Mara nyingine inaudhi sana, mfano mtu amekimbia mbio mita elfu 10 na ameshinda. kumaliza tuu mwandishi wa BBC huyu hapa, naye anaanza kujikanyaga na kingereza. Umeshinda na bado mtu anataka kukunyanyasa na lugh yake ongea kinyiramba atajua wapi atapata tafsiri.

Kwa viongozi wetu hasa Tanzania. Sio lazima kutumia kingereza hasa kwenye issue za serikali. Kingereza achieni UDSM na UDOM huko madarasani huko juu pigeni kiswahili tena kile cha zenji ndio kizuri.

Kwenye mikutano kama ile ya umoja wa mataifa toa hutuba kwa kiswahili. mbona waarabu na nchi nyingine zinatoa hutuba kwa lugha zao.

Tukifika hapo pa kujitambua hata umaskini utakimbia ipo siku watakuja kutuomba msaada kama wanavyo fanya kwa china.
 
Hoja yako ni ya msingi, lakini hatuwezi kusema ni "tabia mbaya" labda useme mitazamo hasi/ushamba/.....n.k. Tabia mbaya ni kama vile uongo, uzushi, umalaya n.k.
hii bado ni tabia mbaya kujikana uhalisia wako.
 
Unakuta Rais au kiongozi anahojiwa mfano na cnn.. na yeye anajibu kwa kingereza. huu ni upuuzi.

Mimi nikiwa Raisi hata nikikutana na mabalozi nitaongea nao Kiswahili hawawezi kuwa mabalozi nchini kwako halafu wewe mwenyeji ndio uhangaike kuongea nao lugha yao nchini kwako.Kwa nini mimi nijue Lugha yao na sio wao wajue lugha yangu?

Ukienda nchi mfano Ufaransa au china wewe mgeni ndio una kazi kujua lugha zao.Wao hawana mpango na wewe na kilugha chako utajijua.Kuanzia Raisi na viongozi wote unawakuta hawajui kiingereza,kifaransa,wala kiswahili.Wao wanapiga kichina chao kwisha.Anayetaka aje na mkalimani wake kama haelewi.
 
Laiti pia kila kabila lingeng'ang'ana na lugha ya kabila lake kwa mtazamo kama huo sijui hata hichi kiswahili kingekuwa na hali gani hapa Tanzania.
 
Tumkumbuke Philip Nyusi wa Msumbiji alipohutubia Bung la TZ alitumia lugha gani?
 
Lugha ni maelewano kati yako na huyo unae ongea naye.
Sasa kama hamuelewani si balaa hilo.
Mimi naona Uwe BUBU maana ni Lugha inazungumzwa dunia nzima
Bila ya upendoleo.
 
Lugha ni maelewano kati yako na huyo unae ongea naye.
Sasa kama hamuelewani si balaa hilo.
Mimi naona Uwe BUBU maana ni Lugha inazungumzwa dunia nzima
Bila ya upendoleo.
Ndio maana wametengeneza vifaa vya kutafsiri ili kila mtu awe huru kuongea lugha yake
 
Unakuta Rais au kiongozi anahojiwa mfano na cnn.. na yeye anajibu kwa kingereza. huu ni upuuzi. kwani huna lugha nyingine unayo jua? unatakiwa umjibu kwa lugha yako mama. Mjibu hata kwa kisukuma.. hata akitumia miaka miwili kupata tafsiri sawa tuu kwani lazima kutumia lugha yao. Sembuse tuna lugha ya kiswahili na bado hatutaki kutumia. Lazima kuonyesha jeuri.

Kuna watu wanajisikia vibaya kutojua kingereza,mbona hujisikii vibaya kuto jua kichina.

Mbona wafaransa wanajibu kwa kifaransa au nani alita sheria ya lugha nyingine Isitumike kama sio kuendeleza kututawala.

Mara nyingine inaudhi sana .. mfano mtu amekimbia mbio mita elfu 10 na ameshinda. kumaliza tuu mwandishi wa bbc huyu hapa, naye anaanza kujikanyaga na kingereza. Umeshinda , na bado mtu anataka kukunyanyasa na lugh yake.. ongea kinyiramba atajua wapi atapata tafsiri.

Kwa viongozi wetu hasa Tanzania. Sio lazima kutumia kingereza hasa kwenye issue za serikali. Kingereza achieni udsm na udom huko madarasani.. huko juu pigeni kiswahili tena kile cha zenji ndio kizuri..

Kwenye mikutano kama ile ya umoja wa mataifa toa hutuba kwa kiswahili. mbona waarabu na nchi nyingine zinatoa hutuba kwa lugha zao.

Tukifika hapo pa kujitambua hata umaskini utakimbia.. ipo siku watakuja kutuomba msaada kama wanavyo fanya kwa china..
 
Huoni wana wa UKAWA wanvyo neng'eneka humu kwamba Magu hajui kinhereza?
 
mkuu nimependa sana huu mtizamo wako. ningekuwa nakujua ningekuja japo kuchumbia binti yako ili nichote maarifa vizuri na kwa ukaribu zaidi.
 
Huoni wana wa UKAWA wanvyo neng'eneka humu kwamba Magu hajui kinhereza?

Huyu Magufuli atakuwa anaugua mgonjwa wa ukoloni mamboleo tu. kwa nini basi hazungumzi kwa lugha ya kiswahili tu! Sasa hio tuisheni ya lugha ya kikoloni anayochukua ya nini lakini?
 
Back
Top Bottom