Watanzania tuache maneno hakuna mgao bali ni maboresho ya vituo vya kupoozea Umeme

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
612
1,045
Shirika kubwa kama Tanesco ni sehemu ya miundombinu ya kimkakati yaani national Infrustructure strategy.

Jukumu la Serikali ni kuhakikisha miundombinu hii inalindwa na kutunzwa vizuri zaidi.

Kulindwa kwa Shirika Kama Tanesco tunahakikisha kuna utimamu critical national infrustructure yaani miundombinu, vifaa, rasilimali watu, taarifa au information, mitandao yake na taratibu zinavofanya kazi na kufanya nchi iendeshwe kiufanisi.

Unyeti wa shirika kama Tanesco kwa nchi unahitaji watu timamu sana ambao wanaweza kutoa update ya kweli pale panapohitajika mawazo sahihi ya kuboresha miundombinu kwa tuliokuwa chini ya Shirika tunafahamu kwa more than six year shirika halikuwahi kutenga bajeti kuboresha miundombinu yake hela zote zilipelekwa hazina na kupangiwa matumizi mengine.

Umeme hauna longolongo jambo la kwanza Umeme uwake mengine baadaye... lakini unaweza vipi kuwasha Umeme pasipokuwa na miundombinu thabiti.

Umeme hauhitaji propaganda sababu zinapoanguka nguzo za Umeme, haitajiki Waziri kuja kwenye eneo la tukio tunahitaji mafundi wafike na kurekebisha.

Marekebisho yanayofanyika sasa ni kuleta umeme wa uhakika hatujawahi kuwa na masaa mengi ya kukatika kwa Umeme lakini imelazimika kuwa hivyo sababu ya kupunguza siku ya mgao.

Ni kweli tunapenda umeme uwake lakini vipi upande wa maboresho kwenye vituo vya kupoozea Umeme, nguzo na nyaya chakavu...? Tuondoe siasa kwenye mambo ya msingi kama Umeme si kila kitu tunaona kuwa ni uzembe maboresho haya yamekuja wakati sahihi.

Naimani serikali haiwezi kupuuzia miundombinu ya kimkakati kwa kushindwa kuifanyia maboresho.

Hakuna nchi iliyo tayari kuona miundombinu ya kimkakati ikifanyiwa hujuma na kunyamaza.! Suala la kusema kuna Biashara ya Jenereta ni utoto wa hali ya juu.

Vyanzo vyetu vya uzalishaji vinafahamika Rais Samia amekwishatoa maagizo nchi haipo tayari kuingia mkataba na kampuni yoyote ya kufua Umeme nchi.

Watanzania acheni maneno kwenye Umeme kabisa tufahamu priority number moja ni taa kuwaka. It’s not a soft power issue mara nyingi.

1. Keep the lights on
2. Update people on hiccups hili linafanyika wakati huu.
3. Then PR ni ya mwisho if necessary!

Thank you...!!!
 
Acha basi kuleta maneno ya longo longo?. Ni Mgao.

Mauzo ya Generators yameongezeka mno. Kwa wanaofanya Biashaya inayohitaji umeme tayari wameshaanza kununua generator . Wewe kaa kijiweni upige pambio.
 
Wakati wakirekebisha vituo vya kupooza umeme baadhi ya maeneo siyatakosa umeme?
Au neno mgao unalitafsiri vipi?
Mamlaka inasema kutakua na mgao mchana ila hatutakua gizani wewe mleta mada unaposema hakuna mgao kumbe hiyo inaitwaje?
Tuiite wengine kuwa na umeme na wengine kutokua nao?
Hizo ndio longolongo. Kubali kwamba nimgao unaotokana na maboresho kwa nchi nzima
 
More than six years shirika halijawahi kutenga pesa za kuboresha miundo mbinu..interesting!

Wacha tukupuuze tu
 
Kwahiyo wewe unabishana na taarifa ya waziri alietangaza "kutakuwa na mgao"

Mbona watu mna akili za ajabu sana
 
Unataka kutuaminisha kuwa hizo mitambo hazikuwahi kufanyiwa service kipindi chote cha miaka mitano ya Hayati mwenda zake?

Mbona hapakuwa na mgao au kipindi hicho hadi mitambo ya umeme ilikuwa inamuogopa mwenda zake mpaka isihitaji regular services.
 
Hapo mwanzo alikuwepo" kufanyiwa service " naye akamzaa "matengenezo" naye akamzaa "maboresho",naye akamzaa "uwekaji wa mitambo mipya"
 
Soma kwanza kichwa si housing ya Meno. Kwamba chadema watakuja na Umeme wa powerbank...?

January unakuwaga mjinga sana, unadhani ukitetea huu uhuni mnaofanya kwa kuweka maneno ya kiingereza ndio utaonekana unaongea hoja ya maana? Muhuni mkubwa ww.
 
Watanzania acheni maneno kwenye Umeme kabisa tufahamu priority number moja ni taa kuwaka. It’s not a soft power issue mara nyingi

Tumezoea kuwasha mishumaa na vibatari umeme wenu mkikata!! Priority ya wananchi ni umeme wa kuwezesha viwanda vizalishe ama sivyo kutatokea uhaba wa bidhaa na hivyo bei kupanda na kutuumiza wanannchi!!! TANESCO kwa kukata kata umeme ndio mnachochea mfumuko wa bei nchini!!!
 
Back
Top Bottom