Watanzania tuache kutaharuki: Nchi yetu ina uzoefu wa mema na machungu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Naamini masaa haya 24 yataamua na Watanzania wataweza kujua au kujuzwa kinachoendelea kuhusu afya ya Rais Magufuli. Mwanadamu ameumbwa kuishi na ameumbwa kufa. Katika haya mawili kuna kucheka na kulia, kuzaa na kuzaliwa, kuugua na kupona na magonjwa na afya.

Afya ya Rais ni jambo kubwa na zito na si jambo la kutolea tetesi ah kutangaza au kushadadia uvumi. Inasikitisha sana kuona watu ambao wanatajwa kama viongozi kufanya jambo hili kama nafasi fulani ya kufurahia au kushabikia. Kiongozi na mtu mzima anapaswa kupima sana kauli na maneno yenye kuweza kuleta au kufanya watu wataharuki.

Ni vizuri kujua kwa uhakika kabisa kuwa nchi yetu ina uwezo wa kutosha kuhimili habari mbaya kuhusu afya ya Raisi. Ni muhimu pia kujua kuwa Kuna taratibu za kikatiba zinazopaswa kufuatwa endapo mambo yoyote yanayoweza kusababisha Raisi ashindwe kuendelea na madaraka (ikiwemo ugonjwa, afya ya akili au mauti). Kama lolote linatokea Watanzania watajulishwa baada ya taratibu site kukamilisha na SIYO MAPEMA kabla ya hapo.

Hivyo basi, nawasihi na kuwaasa Watanzania wenzangu kutuliza mioyo na kusubiria taarifa rasmi (iwe mbaya, ya afueni, au nzuri) na tusieneze na kuongeza chumvi, limau na pilipili. Tumwombe Mungu kuwa lolote liwalo Taifa letu litapita salama na kuwa mwisho wa siku sote tutakuwa tumejiuliza maswali na tumejifunza kwa Yote.

Tusiishi kwa hofu na tetesi. Vyovyote vile ukweli utajulikana, tutulie na Tuache taratibu ziendelee. Kukiwa nabla kujulishwa tutajulishwa Nina uhakika Kuna watu wazima na wakongwe na wenye busara. Vijana wengi wametuangusha leo; inasikitisha.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Wabariki Watanzania Wote.

NDANI YA MASAA 24
Yaani, sijui nisemeje. Najua mamilioni ya Watanzania wanaomuunga mkono Rais Magufuli wamekata furaha na amani. Wamekwazwa na taharuki iliyosabahishwa jana. Lolote ambalo lilitokea halikuwa kubwa wala la kutisha ila liliongezwa chumvi hadi ikapitiliza. Tumemuona Rais katika siha njema na tuendelee kumuombea. Kama nilichosema awali Sisi ni Taifa lililokomaa sasa na tuna uwezo wa kuhimili vishindo vyovyote. Tumepitia Vita, ajali, vifo na magonjwa ya kila namna. Tutaweza kuhimili jambo lolote. Tuwe waangalifu kwa habari zinazohusu mambo mazito hasa kama haya. Long Live John Magufuli, Long Live Tanzania! Aluta Continua!
 
Kwani ile barua ya uteuzi hukuiona mwenzetu? Sie tunajua ni mzima kabisa na Jana kafanya uteuzi na utumbuaji, hofu yako ni nini? Nyie ndio mnaijaza jamii taharuki maana msigwa alipost barua za kutumbua nyie mmekazana na upupu wenu.
 
Mkuu, umeandika vyema sana. Sisi ni binadamu, na duniani tunapita tu. Kwa yeyote miongoni mwetu lolote lile linaweza kumtokea liwe jema ama baya kutokana na mitazamo yetu. Ni vyema tusubiri habari zilizo rasmi tena kupitia vyanzo vya uhakika.
 
Tuliishtukia ile mkuu.msigwa huwa ni kimbelembele mno kutupa updates za ikulu,
Kinachowapa hofu zaidi wananchi kuona ukimya wa msigwa,hata kusimama na kukanusha hakufanya hivyo,hapo ndio sintofahamu ilipozidi
Kwani ile barua ya uteuzi hukuiona mwenzetu? Sie tunajua ni mzima kabisa na Jana kafanya uteuzi na utumbuaji, hofu yako ni nini? Nyie ndio mnaijaza jamii yaharuki maana msigwa alipost barua za kutumbua nyie mmekazana na upupu wenu.
 
Back
Top Bottom