Watanzania tuache hizi hulka zetu: Si dili. Watanzania tunaangamia. Taifa linaangamia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tuache hizi hulka zetu: Si dili. Watanzania tunaangamia. Taifa linaangamia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gobret, Jul 3, 2011.

 1. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa la Watz ni ukosefu wa elimu, umasikini wa mawazo kwa wenye elimu. Maana ni vigumu sana kumtofautisha msomi na asiyesoma. Msomi ananena na kutenda sawa sawa na asiyepata nafasi hiyo. Tena bora huyu asiye na elimu darasa. Wasomi wamekaa kimya wanatetea vibarua yao. Nchi inaliwa na wachache. Nchi haina ndege lakini raisi ana ndege ya kufanya omba omba kila kukicha.

  Sijui niseme hili ni kosa la Mkapa maana ndiye aliyenunua hii ndege na yeye hakutumia na hakuwa omba omba. Sasa huyu ****** ndiyo kaona dili kweli. Akitembeza pua na bakuli. Anaikamua nchi kama kupe. Ndege ya nini ya raisi kwa nchi masikini? Watz. wamekaa kimya, Nchi ipo gizani. Wanachapa usingizi. Vyuo vikuu, vyuo vya kati, shule za sekondari nk kazi za taaluma haziendi kwa maana umeme ni tatizo.

  Tunapitisha siku ziende. Wapinzani nao hawayaoni matatizo ya watanzania. Sijui mpaka waambiwe ndiyo wachangamke. Wanafunzi wa vyuo vikuu kama watoto wasio na serikali, maana serikali haiwajali kabisa. Hawapati haki zao stahili. Na wao wamekaa kimya kuhusu suala la umeme, wamekazania fedha zao. Ndio lkn vipi kuhusu elimu wanayokosa???????? Kwa kukosa umeme? Siku hizi walimu wa vyuo vikuu na kati wamerudi kwenye enzi za kufundisha kwa chaki. Maana Mungu kama katulaani vile.

  Lkn kumbe ni sisi wenyewe. Hatuwawajibisha hawa viongozi ambao ni mizigo kwa ustawi wa Taifa la Tz. Tunawapa kura tena lukuki, kwa nini wasitutukane? Tuamkeni, Taifa linaangamia. Kila mtu kwa nafasi yake. Tusijali maslahi binafsi. Tutetee ustawi wa Taifa letu.

  Achana na Raisi na mke omba omba kama Matonya. Bora wakahamia Dodoma ili waungane na akina Matonya huko. Hatuoni faida ya kuwa na rais mbabaishaji wa aina hii. Mawaziri kama wahudumu wa baa vile. Watz kama wateja wao. Nchi inanuka rushwa kila kona. Wabunge kama machokoraa vile. Kazi kupiga makofi na kudai posho. Hakuna wa kusimamia haki.

  Angalia maendeleo ya mikoa fulani fulani ambapo CCM imekita mizizi. Watu wake ni omba omba, wanatembeza bakuli barabarani kama m/kiti wao. Hawana haya.

  Viongozi wa dini nao kama hawaamini vile ktk imani yao. Mara waseme Mungu katuchagulia huyu jamaa. Ni chaguo lake asilani. Hah! Nao wameshtuka. Wameingia mkenge. Sasa wanajutia, toba kila kukicha, Mungu naye hatakikuwasikiliza. Maana wamelitumia vibaya jina la Mungu kwa maslahi yao binafsi.

  Nyerere baba yetu; naye alituahidi kuwa atatuombea kwa Mungu. Sasa hata yeye katusahau. Maana kuna kila sababu ya kutusahau. Watz tumeacha ile misingi mizuri aliyoijenga na badala yake tunajali maslahi binafsi. Yeye alipigania haki, amani na upendo. Leo chuki, mifarakano ghilba nk ndio misimamo yetu.

  Tutasema nini kuhusu umasikini wetu? Jibu: (1)..................................(2).................................(3).............................
   
 2. M

  Mbayuwayu2008 Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watz. huwajui vizuri. Baadhi yao ni kama kondoo wa Maasai. Hawaoni mbele wala nyuma. KAzi yao kutia tick kwenye kisanduku cha CCM wakati wa kupiga kura. Mabadiliko ya kweli huanza na mtu mhusika. Usitegemee mabadiliko kama tunataka yaanze kwa wengine.

  Kuna sumu nyingi pandikizi za CCM. Na sasa tunajutia na tutajuta kweli. Kweli tuna raisi safi sana. Bingwa wa kuharibu majina mazuri ya watz. Hii hali ya kuona omba omba ni dili sijui imeanzia wapi. Risi bingwa wa omba omba na Watz wenyewe wamegeuka omba omba. Tutafika?

  We, sijui nani vile (Gobret) hapo ulipo na wewe omba omba tu. Usinibishie nakuona. Na mimi omba omba. Sote tu omba omba. Nani yupo salama?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuhusu kuombaomba mzee Ben nae alikuwa akiomba,aliwaita NCHI WAHISAN.......labda ndege ndio hakuitumia........nawahurumia sana wanafunz,kwani wanasoma kwa shida
   
Loading...