Watanzania TANESCO Inakufa Wakati Wateja Wapo Wa Kumwaga?

Ngo

JF-Expert Member
May 25, 2010
284
51
Inasikitisha Kwakweli Katiaka Ulimwengu wa sasa pale Demand ya Service ni Kubwa ila hamna Supply. Nimezungukia Tanesco Mpaka Nimechoka, ni Mwezi wa Nane huu hawa jamaa wanajisuasua tu kuniwekea Umeme kwenye Kibanda changu kwa sababu tu hawana Materials. Nikajiuliza, katika dunia hii ambako makampuni mengi yanatafuta markets kwa bidhaa na services, Kwa Tanesco Sivyo. Kama ndo siasa kutawala uendeshaji wa Makampuni yetu tutafika Watanzania au ndo kulaaniwa kwenyewe huku ambako watu wanakosa maadili katika Uongozi?
 
watu wakiacha kuchakachua hizo mita nyumbani watapata mapato ya kutosha au kila nyumba ikiwa na luku itapunguza uchakachuaji
 
Nafurahi kwamba mjadala umetambua kwamba sote ni wakosa - Serikali (mikataba mibovu, Wizara nyeti kutolipia umeme), Shirika (ufuatiliaji mbovu) na sisi raia (tunaoiba umeme).

Shirika hilo kama litapata faida basi ni kwa maajabu ya Mungu.
 
Tatizo ni Tanesco kutoendeshwa kibiashara - inaendeshwa kama shirika la umma! Hii inatoa mwanya kwa wateja fulani tu kulipia huduma ya umeme na wateja fulani kutolipia umeme. Kwa staili hii shirika haliwezi kutengeneza faida. Dawa ni kuruhusu ushindani kwa kuruhusu makampuni mengine kutoa huduma za umeme katika maeneo mengine tofauti na sasa ambapo Tanesco wanahodhi huduma ya umeme. Hii itawezekana baada ya wadaiwa sugu (ikiwemo serikali) kuilipa Tanesco madai ya nyuma na kudhibiti wizi wa umeme. Nchi za wenzetu huduma ya umeme hutolewa na makampuni tofauti kwenye maeneo tofauti - hii inaweza kuwapa changamoto Tanesco kuboresha huduma.
 
Back
Top Bottom