Watanzania siyo wajinga sana.

Mtukudzi

Member
Nov 14, 2013
91
400
Hivi majimbo ambayo wagombea wa upinzani walishinda kwenye uchaguzi mkuu 2015 na kisha wakajiunga CCM hapakuwepo wagombea wa CCM? Kama CCM ilikuwa na wagombea, wapinzani waliwezaje kushinda? Walishinda kihalali?
Kwa ninayoyaona kwenye clip ya maazimisho ya siku ya wanawake huko Geita nakubali kuwa watanzania siyo wajinga sana bwana.
Yajayo yanatafakarisha!
 
Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
388
500

Kumbe wewe ulimsikia vizuri kama nilivyomsikia mimi. Alisema "Watanzania sio wajinga sana," na sio kama watu wengi wanavyosema humu JF kwa kuliondoa hilo neno "sana" ambala linapotosha maana nzima ya ujumbe wa mkuu. Ni hivi...mkuu ana amini kwamba Watanzania ni wajinga, ila sio sana. Yaani Watanzania tuna ujinga fulani ambao ndio mpaka leo unaendelea kukiweka chama chake madarakani. Enyi Watanzania wenzangu tuamkeni na kuidhihirishia CCM kwamba sisi sio wajinga kabisaa inapokuja kwenye masuala ya kubaini ukweli wa tamthilia za serikali hii iliyopoteza muelekeo. Tunahitaji majibu ya sio tu suala ya MO, bali pia Lissu, Saanane, Gwanda, na wahanga wengine wa utawala huu...

Narudia tena, sisi sio wajinga kabisaa kushindwa kung'amua michezo hii ya kitoto!
 
Essien jr

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
583
1,000
mwenge&Aman na utulivu tunayodanganywa ndio inawafanya Watz walio wengi kuwa wajinga nakuamini Tanzania haiwezi kuendelea bila chama chakavuu kilichoshindwa kuwatoa ktk ombwe kubwa la umasikini na ujinga unaoongezeka kila inapoitwa leo. Binafsi naamini Watz tu-wajinga mfano mzuri nikilichotokea Kusini suala la korosho. Mali yako anakuja mnunuzi ananunua akiona amekosa soko anairudisha imeharibika na unaopikea? Huu si ujinga au ujinga mpk uweje?
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
tupia hiyo clip tuone
.Idadi ya wana chama wa ccm ni wazee na inazidi pungua,huwezi kuta Kijana anaeyechakalika akashabikia ccm zaidi ya kula kulala,mama wa nyumbani, Kila Kijana ni against ccm yote haya chanzo ni ccm kujitenga na kushindwa kutatua shida za watz.Kutegemea dola kumeshindwa kuikoa KANU na vyama kongwe vingi vilifutika sababu ya kutegemea dola badala ya kutegemea wananchi.
 
Attachments

  • Screenshot_2019-03-09-07-09-29.png
    File size
    984.7 KB
    Views
    22

TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
mwenge&Aman na utulivu tunayodanganywa ndio inawafanya Watz walio wengi kuwa wajinga nakuamini Tanzania haiwezi kuendelea bila chama chakavuu kilichoshindwa kuwatoa ktk ombwe kubwa la umasikini na ujinga unaoongezeka kila inapoitwa leo. Binafsi naamini Watz tu-wajinga mfano mzuri nikilichotokea Kusini suala la korosho. Mali yako anakuja mnunuzi ananunua akiona amekosa soko anairudisha imeharibika na unaopikea? Huu si ujinga au ujinga mpk uweje?

Ujinga na umasikini ndio msingi mkuu wa ccm na katu huwezi tenganisha umasikini, ujinga na ccm Fanya research thus wakisema waboreshe elimu yaani kufuta ujinga ndio itakuwa mwisho wao.Kama umetembea nchi nyingi sisi ni masikini na wajinga sana
 
Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
5,617
2,000
Sio wajinga sana, ni wajinga kiasi. So mjinga Wa kwanza na mjinga wa mwisho nani mjinga zaidi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom