Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 19, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180

  Kwa namna yeyote ile utakayotafsir neno AKILI bado utalifungamanisha na uwezo wa kutambua baya na zuri. Wasomi wanaamini kuwa hakuna mtu anayependa ama kuchagua kufikwa na jambo baya..ni katika tabia za kawaida za binaadamu. Na wasomi wakubwa wakiwemo Socrate wanaamini kuwa kufanya jambo ovu ama baya daima mfanyaji uathirika, na kwa kuwa AKILI za kibinadamu zinakataa mtu kujidhuru ama kujiathiri, kwa mtazamo huo kufanya jambo ovu ni matokeo ya kutokuwa na akili, na neno moja la kukosa akili ni UJINGA..kwa lugha ya Kigeni ni IGNORANCE.

  Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.

  1. Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo siwezi kuzungumzia ujinga wake ila nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.

  Tanzania is exceptional country with extra ordinary countrymen..TUNGEKUWA wajinga tungekubali nchi yetu KUTOTAWALIKA..nchi hii ni ya mfano katika nchi za Afrika, mfano kwa UONGOZI imara, mfano kwa AMANI na UTULIVU, mfano kwa UMOJA wa KITAIFA, mfano kwa kujitoa katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kwa hali na mali, hakuna Nchi yeyote katika Afrika kusini mwa jangwa la sahara ambayo imepiga hatua na kufikia ilipofikia leo ikawa HAIJAPATA msaada wa TANZANIA, kama ipo naomba niambiwe.

  Hivyo mimi binafsi napingana kabisa na WAZO kuwa CCM haijafanya chochote katika ujenzi wa ustawi wa jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla..Marais wa Tanzania kutoka BABA wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka Jakaya Mrisho Kikwete wameendelea kuwa ICON sio tu kwa Tanzania bali kwa DUNIA nzima katika suala zima la Utawala na uongozi uliotukuka, hata leo tuzo mbalimbali za Kimataifa zimeendelea kuelekezwa Tanzania kwa heshima ya utendaji wa kazi zao...ni UJINGA na MJINGA tu ambae anaweza kupaza sauti bila aibu kusema kuwa WATANZANIA ni wajinga...na inatia shaka zaidi pale inapotokea mtu huyo akiwa MTANZANIA.

  Na kama ni kile ninachokiona ni MAHABA kwa Upinzani wa nchi hii, niseme tena mimi nimewahi kuwa Mpinzani wa CCM kwa muda mrefu, its no better kwenye upinzani kuliko hata kwa CCM..Hauwezi kulizungumza suala la UONGOZI BORA kwa upinzani..hauwezi kuzungumzia Suala la kukuza ELIMU kwa wapinzani, hauwezi kuliongelea suala la kukomesha Rushwa kwa Wapinzani wa nchi hii...hauwezi kuwaamini kwa lolote wapinzani wa nchi hii..Ni watu wasiojitambua, wasiojielewa, wasio na misimamo, wanaoyumba na baya zaidi WASIOFIKIRI.

  CCM imeendelea kuwa CHAMA kinachojitathimini na kinachojiimarisha siku hadi siku, sipingi wala sisemi kuwa CCM haijawahi kukosea, haina makosa na haijaaribu katika utawala wake..hapana na nikisema hivyo nitakuwa mnafiki, lakini tunaiona CCM ikijivua gamba katika new style, ikikataa kuwakumbatia mafisadi na kwa mara ya nyingine tena ikipata mgombea BILA RUSHWA, BILA HILA na BILA MTANDAO...hivyo kama PASCO unaamini kuwa CCM ni ile ile, yenye watu wale wale na sera zile zile basi PASCO wewe sio PASCO yule ninayemjua ambae huwa anaandika baada ya kufikiria, it seems contrary to my experience., perhaps U have personally and intentionally decides to do wrong and u seemed to know full well of ur decision.

  Najua unataka tuamini katika UPINZANI basi tusaidie watanzania sisi ambao wewe (mwerevu) unadhani tu wajinga kupindukia, sababu 3 tu za kuamini katika Upinzani..jaribu kutushawishi, kutuita wajinga pekee hakusaidii..tupe HOJA kuwa CCM imechoka na hivyo UPO UPINZANI MBADALA wa kutuvusha baada ya kuiweka CCM pembeni...Mind U nilikuwa MPINZANI, yawezekana kabisa najua hata yale USIYOYAJUA.

  Ndio tarehe 25th October 2015, tutaichagua tena CCM, tena kwa kishindo KIKUU, lakini kamwe hatuchagui kwa UJINGA..,tunazo akili, tunajua BAYA na ZURI kwetu, na hivyo..TUMEKUSIKIA, TUMETAFAKARI na TUMESHAAMUA kuwa MAGUFULI ndio Rais wetu wa AWAMU ya TANO..

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CCM.

   
 2. A

  Abel Ndundulu JF-Expert Member

  #101
  Sep 20, 2015
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 754
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pole sana Juliana Shonza.Nimekuwa nikikufuatilia sana katika safari yako ya Kisiasa.Nakiri kuna wakati nilitaka binti yangu afuate nyayo zako.Ila ulipopotoka na kuwa mjasiliatumbo ndio nikakuona hauna maana kabisa.Kwa sasa anayekufahamu anajua umebeba nembo ya usaliti na kutokuaminika.Hata unayoandika yanaakisi hilo.Nakuahidi CCM itakabidhi nyaraka za uanzishwaji wake kwa msajili baada ya Uchaguzi.Itakuwa imekufa na haitasimama tena!
   
 3. kson m

  kson m JF-Expert Member

  #102
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 24, 2014
  Messages: 5,511
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Nasikia degree zipo mpaka za chini ya kitovu!!!
   
 4. ngomai

  ngomai Member

  #103
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 9, 2014
  Messages: 43
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  He is right, no room for opposition for the mean time to be honest
   
 5. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #104
  Sep 20, 2015
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,614
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Huyu kubwa jinga yupo!
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #105
  Sep 21, 2015
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,598
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wanawake dizaini ya 'mirupo' utawajua tu....
   
 7. J

  Juliana Shonza Verified User

  #106
  Sep 21, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Irrelevant fact to the fact on issue..
   
 8. Sungurawembe

  Sungurawembe JF-Expert Member

  #107
  Sep 21, 2015
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 414
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kapambane katika majukwaa maana umekaribishwa na sasa unataka kuwa msemaji wakati hicho chama ni cha wenyewe. Jitahidi uonekane maana viti maalum si mchezo unaweza tupwa nje
   
 9. r

  realleonia JF-Expert Member

  #108
  Sep 21, 2015
  Joined: May 25, 2013
  Messages: 346
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  juliana toka lini mtoto wa kike asikubalike kwao? mmeharibu kwenu mbozi na mwenzio mwampamba mmesahau pesa na mali mlizokuwa mkichangiwa na watu maskini pale MLOWO mbozi leo hii kwa tamaa zenu mpo ccm mnafikiri mtapona na laana hii ktk siasa nendeni mkatubu ndio mtuandikie hizo ngonjera zenu.
   
 10. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #109
  Sep 21, 2015
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,007
  Likes Received: 947
  Trophy Points: 280
  Pasco ndio mwenye njaa ya Lowasa toka yuko CCM. Yeye ni Lowasa tuu chai, lunch na dinner!Ni kweli tumekusikia na tumekuelewa lakini tunakwenda kumchagua Rais, sio kibaraka wa mabeberu, Ikulu sio pango la wezi!"Hapa kazi tu"
   
 11. A

  Abel Ndundulu JF-Expert Member

  #110
  Sep 21, 2015
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 754
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Message sent and delivered...I wish you all the best!!
   
 12. USSR

  USSR JF-Expert Member

  #111
  Sep 21, 2015
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 1,143
  Likes Received: 908
  Trophy Points: 280
  juliana umesema ukweli na wote tuseme amina
   
 13. m

  marikiti JF-Expert Member

  #112
  Sep 21, 2015
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 2,715
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi wajinga ni wachache kuliko waadilifu
   
 14. M

  Mwembebasha JF-Expert Member

  #113
  Sep 21, 2015
  Joined: Dec 27, 2013
  Messages: 1,427
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dah mrembo upo?? Ina maana ushapotea kisiasa mama?? Kweli siasa mbaya...
   
 15. mtumiaji

  mtumiaji Senior Member

  #114
  Sep 21, 2015
  Joined: Apr 6, 2013
  Messages: 106
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  we itetee sisiem wenyewe wanapiga ma 10% matumbo hayooo, we unabaki na "hapa kazi tu"

  wanasema " LET GOD LOVE CRAZY PEOPLE, IT IS HE WHO MAKES THEM"

  I'm out.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #115
  Oct 8, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,624
  Likes Received: 23,785
  Trophy Points: 280
  Kiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.

  Karibu Boss, Mheshimiwa saba, Bi Juliana Shonza.

  Paskali.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #116
  Oct 8, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,624
  Likes Received: 23,785
  Trophy Points: 280
  Kiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.

  Karibu Boss, Mheshimiwa saba, Bi Juliana Shonza.

  Paskali.
   
 18. ndue

  ndue Member

  #117
  Oct 10, 2017
  Joined: Mar 22, 2016
  Messages: 17
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  Inaonesha ni jinsi gani mnavyohofia uchaguzi 2020 ,ccm mmelikoroga lazma mlinywe, nyang'au nyie
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...