Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 19, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180

  Kwa namna yeyote ile utakayotafsir neno AKILI bado utalifungamanisha na uwezo wa kutambua baya na zuri. Wasomi wanaamini kuwa hakuna mtu anayependa ama kuchagua kufikwa na jambo baya..ni katika tabia za kawaida za binaadamu. Na wasomi wakubwa wakiwemo Socrate wanaamini kuwa kufanya jambo ovu ama baya daima mfanyaji uathirika, na kwa kuwa AKILI za kibinadamu zinakataa mtu kujidhuru ama kujiathiri, kwa mtazamo huo kufanya jambo ovu ni matokeo ya kutokuwa na akili, na neno moja la kukosa akili ni UJINGA..kwa lugha ya Kigeni ni IGNORANCE.

  Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.

  1. Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo siwezi kuzungumzia ujinga wake ila nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.

  Tanzania is exceptional country with extra ordinary countrymen..TUNGEKUWA wajinga tungekubali nchi yetu KUTOTAWALIKA..nchi hii ni ya mfano katika nchi za Afrika, mfano kwa UONGOZI imara, mfano kwa AMANI na UTULIVU, mfano kwa UMOJA wa KITAIFA, mfano kwa kujitoa katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kwa hali na mali, hakuna Nchi yeyote katika Afrika kusini mwa jangwa la sahara ambayo imepiga hatua na kufikia ilipofikia leo ikawa HAIJAPATA msaada wa TANZANIA, kama ipo naomba niambiwe.

  Hivyo mimi binafsi napingana kabisa na WAZO kuwa CCM haijafanya chochote katika ujenzi wa ustawi wa jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla..Marais wa Tanzania kutoka BABA wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka Jakaya Mrisho Kikwete wameendelea kuwa ICON sio tu kwa Tanzania bali kwa DUNIA nzima katika suala zima la Utawala na uongozi uliotukuka, hata leo tuzo mbalimbali za Kimataifa zimeendelea kuelekezwa Tanzania kwa heshima ya utendaji wa kazi zao...ni UJINGA na MJINGA tu ambae anaweza kupaza sauti bila aibu kusema kuwa WATANZANIA ni wajinga...na inatia shaka zaidi pale inapotokea mtu huyo akiwa MTANZANIA.

  Na kama ni kile ninachokiona ni MAHABA kwa Upinzani wa nchi hii, niseme tena mimi nimewahi kuwa Mpinzani wa CCM kwa muda mrefu, its no better kwenye upinzani kuliko hata kwa CCM..Hauwezi kulizungumza suala la UONGOZI BORA kwa upinzani..hauwezi kuzungumzia Suala la kukuza ELIMU kwa wapinzani, hauwezi kuliongelea suala la kukomesha Rushwa kwa Wapinzani wa nchi hii...hauwezi kuwaamini kwa lolote wapinzani wa nchi hii..Ni watu wasiojitambua, wasiojielewa, wasio na misimamo, wanaoyumba na baya zaidi WASIOFIKIRI.

  CCM imeendelea kuwa CHAMA kinachojitathimini na kinachojiimarisha siku hadi siku, sipingi wala sisemi kuwa CCM haijawahi kukosea, haina makosa na haijaaribu katika utawala wake..hapana na nikisema hivyo nitakuwa mnafiki, lakini tunaiona CCM ikijivua gamba katika new style, ikikataa kuwakumbatia mafisadi na kwa mara ya nyingine tena ikipata mgombea BILA RUSHWA, BILA HILA na BILA MTANDAO...hivyo kama PASCO unaamini kuwa CCM ni ile ile, yenye watu wale wale na sera zile zile basi PASCO wewe sio PASCO yule ninayemjua ambae huwa anaandika baada ya kufikiria, it seems contrary to my experience., perhaps U have personally and intentionally decides to do wrong and u seemed to know full well of ur decision.

  Najua unataka tuamini katika UPINZANI basi tusaidie watanzania sisi ambao wewe (mwerevu) unadhani tu wajinga kupindukia, sababu 3 tu za kuamini katika Upinzani..jaribu kutushawishi, kutuita wajinga pekee hakusaidii..tupe HOJA kuwa CCM imechoka na hivyo UPO UPINZANI MBADALA wa kutuvusha baada ya kuiweka CCM pembeni...Mind U nilikuwa MPINZANI, yawezekana kabisa najua hata yale USIYOYAJUA.

  Ndio tarehe 25th October 2015, tutaichagua tena CCM, tena kwa kishindo KIKUU, lakini kamwe hatuchagui kwa UJINGA..,tunazo akili, tunajua BAYA na ZURI kwetu, na hivyo..TUMEKUSIKIA, TUMETAFAKARI na TUMESHAAMUA kuwa MAGUFULI ndio Rais wetu wa AWAMU ya TANO..

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CCM.

   
 2. p

  peter muta Senior Member

  #81
  Sep 19, 2015
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukawa oyeeeeee
   
 3. Mkinga Wa Milimani

  Mkinga Wa Milimani Member

  #82
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kubali ukatae CCM hamna jipya na zungumia wewe usijumulishe watanzania wote, maana nami nimtanzania ila ninamawazo tofauti na CCM.

  Pili usilazimishie mawazo kuwa watz lazima wawe ccm, ukiwa hivyo wewe utakuwa mjinga wa neno DEMOCRASIA unatakiwa kueleweshwa.
   
 4. A

  Abel Ndundulu JF-Expert Member

  #83
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 754
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lowassa,mpango mzima!CCM ageni kwa amani!
   
 5. Ndikwega

  Ndikwega JF-Expert Member

  #84
  Sep 19, 2015
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 4,602
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Huyu ma.l.a.... Andhani tuna muda wa iujadili upuuzi wake, kura tulishaamua ktayari bado muda tu uwadie. Lowassa for presidency.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #85
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,821
  Trophy Points: 280

  kwa kuanzia kwanza natanguliza samahani kwa haya nitakayosema, mimi ni dhaifu, na kwako wewe Juliana Shonza, mimi hoi!, sina la kusema!, hata ukiniambia condition ni kumtosa ENL na kumchagua JPM, nakubali!.

  Kwa mtu kuukubali udhaifu wake kwenye kadamnasi ya watu nayo ni strength!, naomba kukiri kuwa mimi ni binadamu na nina strengths na weaknesses zangu, miongoni mwa strengths zangu, ni kusema ukweli daima no matter what, na uzuri wa ukweli, siku zote, ndio utakaosimama mpaka mwisho, na miongoni mwa ukweli mchungu kabisa kumeza, ni kwa mtu yoyote mwenye akili zake timamu, anayejua uchumi wa dunia, anayejua tulipopata uhuru sisi Tanzania tulikuwa na rasilimali gani, na kujinganisha na wenzetu tuliopata nao uhuru walikua na rasimali gani, halafu leo miaka 54 baada ya uhuru, tunajiangalia sisi Tanzania tuko wapi, na wenzetu wako wapi, ukijiuliza tatizo ni nini, na ukajua kuwa ni CCM, then, utakubaliana na mimi, kamwe hakuna mtu yeyote mwenye akili zake timamu, anaweza kuichagua tena CCM unless ni ignorant.

  Na baada ya hayo, naomba kukumbushia udhaifu wangu, kwako kiukweli nakupendaga sana tuu wewe mtoto kuliko unavyojijua!.

  Kati ya wanaokupenda humu jf, siko mimi pekee yangu, tuko wengi!, bali hata jamaa huyu, namfahamu pia anakupenda sana!, ile siku ulipotimulia Chadema, alikulilia sana! na uzi humu alikupandishia!.
  Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...


  Tuachane na jamaa yangu huyo anavyokupenda, turejee kwangu, ulipopandisha uzi huu,Vijana wa CHADEMA wana uwezo mdogo sana - Page 6

  nilikueleza hivi

  Nakutakia Jumamo
  si njema sweety...
  Pa
  sco
   
 7. kayaman

  kayaman JF-Expert Member

  #86
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 3, 2013
  Messages: 3,012
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  shonza nasikia uliolewaga hizi habari ni kweli?
  na zile kampeni za kitanda kwa kitanda sikuhizi umeacha? au jamaa atavumilia tu!
  lowassa rais
   
 8. s

  sensor JF-Expert Member

  #87
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 27, 2015
  Messages: 2,472
  Likes Received: 835
  Trophy Points: 280
  Afungwe akiwa Rais au coz huku uraiani tu mmeshindwa hata kumbambikia hata kesi ya kuku sasà sijui mtamfunga lini ?

  Vijana wa IT bana!!!
  Ze fieldmarshal anawadanganya haswa.

  Angalia msiende kumuuwa Saddam wa Kuwait coz mnatumika vibaya sana.
  Mbele nyuma kote mnatumika
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #88
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,821
  Trophy Points: 280

  Mkuu Jay One, heshima ni kitu cha bure! acha kutukana watu! na sio vizuri kumuita hivi mwenzako, kuwa "anauza", nijuavyo mimi wanachama wa chama kimoja huwa hawafanyi biashara na hawauziani, bali hupeana tuu kwa upendo, kugaiyana kwa hiyana, au kutoa huduma za kibinaadamu kwa viongozi wao kama wajibu, kwa sababu, wengine wao, that is the only thing they can do best, hivyo kupeana kwa kusaidina tuu tena kwa ridhaa zao wenyewe ili kupata kitu, kama ubunge a viti maalum au hata bure bure tuu bila mategemeo yoyote kwa lengo la kufurahishana, kufurahiana na kupeana raha tuu, unless kama una ushahidi kuwa huyu Mhe. (Mtarajiwa) Juliana Shonza, alipokuwa Chadema aliuza, then hata sasa yuko huko CCM nako atauza!, lakini kama akiwa Chadema alitoa bure, then hata sasa huko CCM, atatoa bure!, unless kama una ushahidi wowote wa huyu dada kujihusisha kufanya biashara hiyo, then please, futa hii kauli yako ya kumuita, dada wa watu na mbunge mtarajiwa kuwa ni "Muuza tundu wa CCM", ni ya udhalilishaji, na inatuudhi sisi tunao mpendaga sana tuu huyu mdada!.

  Paskali

  cc. Jay One,
   
 10. J

  Juliana Shonza Verified User

  #89
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Kuhusu utetezi wako ulioendelea nao kwa JAY ONE, nilishakutumia salamu za shukrani kama nitakavyozinukuu hapa chini, kwa kweli wewe ni mwema sana, muungwana sana na hakika unapaswa kushukuriwa...shukran.
  Ama kuhusu msisitizo wako kuwa tukijilinganisha na nchi zingine ambazo zilipata uhuru katika miaka hiyo takriban 50 iliyopita kuwa wengi wamepiga hatua katika maendeleo, lazima ufanye comparison ya workload yetu na wao katika miaka hiyo 50...tumefanya nini interm of African Liberation which is the true factor kwa ku-slow down kwetu katika kupata Maendeleo ya haraka..

  Mwalimu had a vision, right and true Pan Africanism mentality ambapo Tanzania ilitumia resource zake nyingi on the interest of African Liberation believing kuwa if one amongst African nations remain colonized then we are all colonized, and we full utilize our resources to stand that fact..unfortunately leo wametokea watu ambao wewe ni mfano wao who are completely brainwashed and demonstrated high level of schism faction, self centered ego on their heart and mind fundamentally..ambao wanadhani tumepoteza bure nguvu zetu kufanya hayo na kwamba wao ni vinara wa kukosoa BLINDLY..

  Kama unadhani ELIMU yako iliyokupa kiburi cha kuona Watanzania wote ni mataahira ndio msingi wa Maendeleo ambayo Mwalimu and the rest walifikiria then U are wrong..U are as IGNORANT better than any of Us..Arrogance is ignorance with an attitude..
   
 11. r

  ray jay JF-Expert Member

  #90
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 974
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  Ndoto zingine ni ajabu sana...
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #91
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,448
  Likes Received: 26,318
  Trophy Points: 280
  Kwanza nitoe onyo kwako Pasco kuwa pamoja na kauli yako kuwa huwa "unampendaga" huyo mhe.Mtarajiwa hilo nakuomba weka pembeni kwa vile kuna mtu amempenda zaidi, ingawa namuona ame 'like' statement yako ya kumzimikia na kumsifu kuwa ni chuma.
  ImageUploadedByJamiiForums1442694713.986244.jpg
  Turudi kwenye mada, nimepata mashaka sana na uelewa wa huyu bibie ambaye amepata kuwa makamu wa mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema tena taifa ja sasa msemaji mkubwa wa mambo mengi ya CCM.
  Katika mada yake amesema " Hakuna nchi yeyote ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara iliyopata maendeleo bila ya msaada wa Tanzania". Jamani hebu nisaidieni labda mie ndio sifahamu. Hivi nchi za kusini ya jangwa la Sahara ni zipi? Tukishazijua tuanze kuangalia mafanikio yao na msaada wa Tanzania kwao ni upi. Tukumbuke kasema NCHI ZOTE. Pasco mwokoe "umpendaye" kwa kutusaidia (kunisaidia) kupata huo ufafanuzi kidogo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #92
  Sep 20, 2015
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,895
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Umeshajifungua?
   
 14. A

  Abel Ndundulu JF-Expert Member

  #93
  Sep 20, 2015
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 754
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ukweli unauma saaana,ndiyo unauma kuliko kipigo!!!TOROKA UJE!!
   
 15. w

  wesiko324 New Member

  #94
  Sep 20, 2015
  Joined: Aug 22, 2015
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawaoni hao kazi yao kupiga kelele tu
   
 16. kson m

  kson m JF-Expert Member

  #95
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 24, 2014
  Messages: 5,511
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Hilo gamba limekaririshwa.kwa kumsaidia nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara ni nchi zote zilizopo kusini mwa msitari wa latitudo 15°s.hizi ni pamoja na liberia,ghana,togo,cameroon,gabon,congo,DRC,CAR,benin,sudan,ethiopia,uganda,kenya,rwanda,burundi,malawi,madagasca,angola,zambia,na africa kusini, kwa uchache.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. kson m

  kson m JF-Expert Member

  #96
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 24, 2014
  Messages: 5,511
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Others are:senegal,guinea bissau,guinea,siera leon,burkinafaso,nigeria,ethiopia,eritrea,djibout,somalia,malawimozambique,zimbabwenamibia,botswana etc.
   
 18. Egnecious

  Egnecious JF-Expert Member

  #97
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 8, 2015
  Messages: 743
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 80
  ushindi ccm upo watu wanaipenda na wataichagua hata watukane vip hapakazitu
  20150920045525.jpg

  20150920045509.jpg
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #98
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,448
  Likes Received: 26,318
  Trophy Points: 280
  Ndicho hicho nilitaka atuambie Maendeleo ya nchi hizo yamechangiwa vipi na Tanzania? MTU anaponiambia ana degree na ni mwanasiasa halafu anasema hivyo napata mashaka na elimu yake, angesema Lusinde sawa
   
 20. mweusi asili

  mweusi asili JF-Expert Member

  #99
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 11, 2014
  Messages: 492
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  chini ya ccm Tanzania tunajivunia umasikini
   
 21. Gefu

  Gefu JF-Expert Member

  #100
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 6,960
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  ....kwa kauli hii bibi umedhihirisha ni mji..ngaaa tu...
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...