Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 19, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180

  Kwa namna yeyote ile utakayotafsir neno AKILI bado utalifungamanisha na uwezo wa kutambua baya na zuri. Wasomi wanaamini kuwa hakuna mtu anayependa ama kuchagua kufikwa na jambo baya..ni katika tabia za kawaida za binaadamu. Na wasomi wakubwa wakiwemo Socrate wanaamini kuwa kufanya jambo ovu ama baya daima mfanyaji uathirika, na kwa kuwa AKILI za kibinadamu zinakataa mtu kujidhuru ama kujiathiri, kwa mtazamo huo kufanya jambo ovu ni matokeo ya kutokuwa na akili, na neno moja la kukosa akili ni UJINGA..kwa lugha ya Kigeni ni IGNORANCE.

  Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.

  1. Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo siwezi kuzungumzia ujinga wake ila nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.

  Tanzania is exceptional country with extra ordinary countrymen..TUNGEKUWA wajinga tungekubali nchi yetu KUTOTAWALIKA..nchi hii ni ya mfano katika nchi za Afrika, mfano kwa UONGOZI imara, mfano kwa AMANI na UTULIVU, mfano kwa UMOJA wa KITAIFA, mfano kwa kujitoa katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kwa hali na mali, hakuna Nchi yeyote katika Afrika kusini mwa jangwa la sahara ambayo imepiga hatua na kufikia ilipofikia leo ikawa HAIJAPATA msaada wa TANZANIA, kama ipo naomba niambiwe.

  Hivyo mimi binafsi napingana kabisa na WAZO kuwa CCM haijafanya chochote katika ujenzi wa ustawi wa jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla..Marais wa Tanzania kutoka BABA wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka Jakaya Mrisho Kikwete wameendelea kuwa ICON sio tu kwa Tanzania bali kwa DUNIA nzima katika suala zima la Utawala na uongozi uliotukuka, hata leo tuzo mbalimbali za Kimataifa zimeendelea kuelekezwa Tanzania kwa heshima ya utendaji wa kazi zao...ni UJINGA na MJINGA tu ambae anaweza kupaza sauti bila aibu kusema kuwa WATANZANIA ni wajinga...na inatia shaka zaidi pale inapotokea mtu huyo akiwa MTANZANIA.

  Na kama ni kile ninachokiona ni MAHABA kwa Upinzani wa nchi hii, niseme tena mimi nimewahi kuwa Mpinzani wa CCM kwa muda mrefu, its no better kwenye upinzani kuliko hata kwa CCM..Hauwezi kulizungumza suala la UONGOZI BORA kwa upinzani..hauwezi kuzungumzia Suala la kukuza ELIMU kwa wapinzani, hauwezi kuliongelea suala la kukomesha Rushwa kwa Wapinzani wa nchi hii...hauwezi kuwaamini kwa lolote wapinzani wa nchi hii..Ni watu wasiojitambua, wasiojielewa, wasio na misimamo, wanaoyumba na baya zaidi WASIOFIKIRI.

  CCM imeendelea kuwa CHAMA kinachojitathimini na kinachojiimarisha siku hadi siku, sipingi wala sisemi kuwa CCM haijawahi kukosea, haina makosa na haijaaribu katika utawala wake..hapana na nikisema hivyo nitakuwa mnafiki, lakini tunaiona CCM ikijivua gamba katika new style, ikikataa kuwakumbatia mafisadi na kwa mara ya nyingine tena ikipata mgombea BILA RUSHWA, BILA HILA na BILA MTANDAO...hivyo kama PASCO unaamini kuwa CCM ni ile ile, yenye watu wale wale na sera zile zile basi PASCO wewe sio PASCO yule ninayemjua ambae huwa anaandika baada ya kufikiria, it seems contrary to my experience., perhaps U have personally and intentionally decides to do wrong and u seemed to know full well of ur decision.

  Najua unataka tuamini katika UPINZANI basi tusaidie watanzania sisi ambao wewe (mwerevu) unadhani tu wajinga kupindukia, sababu 3 tu za kuamini katika Upinzani..jaribu kutushawishi, kutuita wajinga pekee hakusaidii..tupe HOJA kuwa CCM imechoka na hivyo UPO UPINZANI MBADALA wa kutuvusha baada ya kuiweka CCM pembeni...Mind U nilikuwa MPINZANI, yawezekana kabisa najua hata yale USIYOYAJUA.

  Ndio tarehe 25th October 2015, tutaichagua tena CCM, tena kwa kishindo KIKUU, lakini kamwe hatuchagui kwa UJINGA..,tunazo akili, tunajua BAYA na ZURI kwetu, na hivyo..TUMEKUSIKIA, TUMETAFAKARI na TUMESHAAMUA kuwa MAGUFULI ndio Rais wetu wa AWAMU ya TANO..

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CCM.

   
 2. J

  Juliana Shonza Verified User

  #61
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Hii ndio CCM mpya ninayoizungumza yenye viongozi hawa..

  https://youtu.be/bSG2TBeCS_A
   
 3. J

  Juliana Shonza Verified User

  #62
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Ndio WATANZANIA wana hasira na CCM..ni kweli lakini hilo halitoshi kuwafanya ninyi ni bora kuliko CCM, na kama tutapima hasira za watanzania, basi CCM wana ahueni kuliko wapinzani..

  Pamoja na changamoto zilizowakabili CCM bado ni Chama imara na bora kuliko wapinzani..
   
 4. Rawasha

  Rawasha JF-Expert Member

  #63
  Sep 19, 2015
  Joined: Oct 1, 2014
  Messages: 447
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Wanaiangusha ccm ni kama wewe.makamba.mwigulu.nape na wenye akili za hivo wakidhani ccm inaweza fanya chochote kibaya na bado ipendwe na wananchi. Mungu kawapiga upofu muende nao mpaka shimoni.
  Hata mnunue tv na redio zote na mchane mabango EL na UKAWA wapo moyoni mwa watanzania tayari. Hanma la kufanya.
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #64
  Sep 19, 2015
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,598
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kama ndivyo, basi nadhani mimi si mTanzania...sababu nimemua Lowassa ndio Rais wangu, na si Magufuli.
   
 6. dist111

  dist111 JF-Expert Member

  #65
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 3,035
  Likes Received: 1,376
  Trophy Points: 280
  Wanachoamini wana UKAWA na upinzani kwa ujumla n kuwa nchi inaweza chukuliwa bila maandalizi
  Kwa mtindo huu wa zimamoto hakuna cha kutegemea kutoka UKAWA, yaan wamerudi nyuma zaidi kuliko nilivotarajia
   
 7. Nkanaga

  Nkanaga JF-Expert Member

  #66
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 656
  Likes Received: 490
  Trophy Points: 80
  Ujue Nyie wachache mnaji-contradict wenyewe, wenzio makao makuu, wafikiriao (naamini kuliko wewe) wamejiridhisha kuwa CCM imechoka na haiuzi tena! thats why wakapanga bajeti ya kutendeneza mabango yanayomnadi Mgombea binafsi john pombe, naye kwa kujua ccm kimefariki, hakinadi chama, badala yake anakishangaa kwa namna kilivyotufikisha hapa! Juliana Shonza naamini ulipitia madarasa kadhaa, yatendee haki basi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. C

  Chosen generation JF-Expert Member

  #67
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 13, 2014
  Messages: 4,479
  Likes Received: 3,802
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo sisi tusiomkubali huyo mgombea wenu sio Watanzania? Neno "Watanzania ni general sana" instead tumia "Wafuasi wa ccm." Kwa maana Watanzania ambao sio "wafuasi wa chama chochote" wameamua kuchagua mabadiliko, wameamua kumchagua Lowasa. Otherwise nikubaliane na mdau mmoja hapo juu aliposema "kuhamia kwako ccm, kumekuondolea akili, na sasa hata akina Wema Sepetu ni bora kuliko wewe huko." Chadema ulikuwa Kiongozi wa kitaifa wa chama kwa upande wa vijana. Who knows kama isingekuwa tamaa & usaliti sasa hivi huenda ungekuwa kiongozi wa Bawacha ... Acheni tamaa za kijinga nyie vijana.
   
 9. Charles Dotter

  Charles Dotter JF-Expert Member

  #68
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 16, 2015
  Messages: 894
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 80
  sijawahi kuona mtu anashambuliwa kama huyu dada.
  ushauri wangu kwako...
  bora kwa kipindi hiki ukakaa kimya na uangalie mchakato wakampeni unaendaje, i hope utaufanyia kazi ushauri wangu...maana hakuna alieonyesha kukuelewa na ninahisi wengi wakiona jina lako na thread yaklo hawasoomi coz tayari wana negative attitude toward your post...
  kipindi hiki ni cha ukawa ngojera baadae
   
 10. Mudawote

  Mudawote JF-Expert Member

  #69
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 10, 2013
  Messages: 5,710
  Likes Received: 4,189
  Trophy Points: 280
  Mjingaa wewe lowasa ni mwizi, fisadi na ni bubu hawezi kuwa rais!
   
 11. Mudawote

  Mudawote JF-Expert Member

  #70
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 10, 2013
  Messages: 5,710
  Likes Received: 4,189
  Trophy Points: 280
  Ukawa ni mashetani na wanaompinga wote ni mashetani wasubiri hukumu yao 25/10. Huyo lowasa lazima afungwe
   
 12. Charles Dotter

  Charles Dotter JF-Expert Member

  #71
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 16, 2015
  Messages: 894
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 80
  ndugu yangu kipindi hiki cha uchaguzi kuvumiliana ni kitu cha muhimu sana, sio lazima watu wote wapende kitu kimoja, nadhani si vyema kuwaita masheteni....hii itakuwa haina tija kwa jamii. samahani mvumiliane jamani.....huo ndo ushauri wangu...ninaimani baada ya 25 oct. iwe lowassa au magufuli watanzania wote watakubali nakuendelea na maisha


   
 13. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #72
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 9,096
  Likes Received: 10,227
  Trophy Points: 280
  shonzaaaaa!!! mbona unalialiaa????
   
 14. Root

  Root JF-Expert Member

  #73
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,945
  Likes Received: 13,807
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu mtatumia kila mbinu... polisi wenu wameamua wacheze fair game maana wameona mnaondoka...
  NEC nao wamemaliza goli la mkono..... mkitusumbua Redcard twawapa kabla ya uchaguzi
   
 15. j

  jaxborn kasanya JF-Expert Member

  #74
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 10, 2015
  Messages: 299
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  sema umeamua na kakura kako kamoja pus ww mie Lowasa juba
   
 16. kmbwembwe

  kmbwembwe JF-Expert Member

  #75
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,465
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  nina mashaka na wewe 'huongo' ndio nini?
   
 17. Jp Omuga

  Jp Omuga JF-Expert Member

  #76
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 2,783
  Likes Received: 939
  Trophy Points: 280
  Kuna Watanzania wengi sana kwa sasa wamebadilika si wajinga tena... Na ili kuthibitisha hilo wanataka mabadiliko..!!
  Ila wapo wajinga wachache ndani ya ccm kama huyu mleta uzi ambao wanafikiri kuwa ccm yenye ahadi zile zile itawafikisha kwenye mabadiliko na Tanzania ya Magufuli...!!
   
 18. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #77
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,975
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Sio watanzania. Sena wewe. Watanzania wa leo waneamua lowasa
   
 19. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #78
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 24,559
  Likes Received: 16,656
  Trophy Points: 280
  Ishu sio kuishabikia sisiemu, ishu ni kukataa kufanywa mjinga na watu wanaosema kitu kumbe HAWAMAANISHI. Kama zimo kichwani utakuwa umenielewa.
   
 20. MAGALEMWA

  MAGALEMWA JF-Expert Member

  #79
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 8, 2015
  Messages: 4,215
  Likes Received: 2,429
  Trophy Points: 280
  Watanzania sio wajinga ila wewe ni MJINGA; HUSIKII, HUTAFAKARI na umeamua UCHIZI UKUTAWALE
   
 21. tungwilege

  tungwilege Senior Member

  #80
  Sep 19, 2015
  Joined: May 15, 2015
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ww ndio umeamua,usinisee mm,mm ni lowasa ndio ajae
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...