Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua Magufuli ndio ajaye

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 19, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180

  Kwa namna yeyote ile utakayotafsir neno AKILI bado utalifungamanisha na uwezo wa kutambua baya na zuri. Wasomi wanaamini kuwa hakuna mtu anayependa ama kuchagua kufikwa na jambo baya..ni katika tabia za kawaida za binaadamu. Na wasomi wakubwa wakiwemo Socrate wanaamini kuwa kufanya jambo ovu ama baya daima mfanyaji uathirika, na kwa kuwa AKILI za kibinadamu zinakataa mtu kujidhuru ama kujiathiri, kwa mtazamo huo kufanya jambo ovu ni matokeo ya kutokuwa na akili, na neno moja la kukosa akili ni UJINGA..kwa lugha ya Kigeni ni IGNORANCE.

  Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.

  1. Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo siwezi kuzungumzia ujinga wake ila nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.

  Tanzania is exceptional country with extra ordinary countrymen..TUNGEKUWA wajinga tungekubali nchi yetu KUTOTAWALIKA..nchi hii ni ya mfano katika nchi za Afrika, mfano kwa UONGOZI imara, mfano kwa AMANI na UTULIVU, mfano kwa UMOJA wa KITAIFA, mfano kwa kujitoa katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kwa hali na mali, hakuna Nchi yeyote katika Afrika kusini mwa jangwa la sahara ambayo imepiga hatua na kufikia ilipofikia leo ikawa HAIJAPATA msaada wa TANZANIA, kama ipo naomba niambiwe.

  Hivyo mimi binafsi napingana kabisa na WAZO kuwa CCM haijafanya chochote katika ujenzi wa ustawi wa jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla..Marais wa Tanzania kutoka BABA wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka Jakaya Mrisho Kikwete wameendelea kuwa ICON sio tu kwa Tanzania bali kwa DUNIA nzima katika suala zima la Utawala na uongozi uliotukuka, hata leo tuzo mbalimbali za Kimataifa zimeendelea kuelekezwa Tanzania kwa heshima ya utendaji wa kazi zao...ni UJINGA na MJINGA tu ambae anaweza kupaza sauti bila aibu kusema kuwa WATANZANIA ni wajinga...na inatia shaka zaidi pale inapotokea mtu huyo akiwa MTANZANIA.

  Na kama ni kile ninachokiona ni MAHABA kwa Upinzani wa nchi hii, niseme tena mimi nimewahi kuwa Mpinzani wa CCM kwa muda mrefu, its no better kwenye upinzani kuliko hata kwa CCM..Hauwezi kulizungumza suala la UONGOZI BORA kwa upinzani..hauwezi kuzungumzia Suala la kukuza ELIMU kwa wapinzani, hauwezi kuliongelea suala la kukomesha Rushwa kwa Wapinzani wa nchi hii...hauwezi kuwaamini kwa lolote wapinzani wa nchi hii..Ni watu wasiojitambua, wasiojielewa, wasio na misimamo, wanaoyumba na baya zaidi WASIOFIKIRI.

  CCM imeendelea kuwa CHAMA kinachojitathimini na kinachojiimarisha siku hadi siku, sipingi wala sisemi kuwa CCM haijawahi kukosea, haina makosa na haijaaribu katika utawala wake..hapana na nikisema hivyo nitakuwa mnafiki, lakini tunaiona CCM ikijivua gamba katika new style, ikikataa kuwakumbatia mafisadi na kwa mara ya nyingine tena ikipata mgombea BILA RUSHWA, BILA HILA na BILA MTANDAO...hivyo kama PASCO unaamini kuwa CCM ni ile ile, yenye watu wale wale na sera zile zile basi PASCO wewe sio PASCO yule ninayemjua ambae huwa anaandika baada ya kufikiria, it seems contrary to my experience., perhaps U have personally and intentionally decides to do wrong and u seemed to know full well of ur decision.

  Najua unataka tuamini katika UPINZANI basi tusaidie watanzania sisi ambao wewe (mwerevu) unadhani tu wajinga kupindukia, sababu 3 tu za kuamini katika Upinzani..jaribu kutushawishi, kutuita wajinga pekee hakusaidii..tupe HOJA kuwa CCM imechoka na hivyo UPO UPINZANI MBADALA wa kutuvusha baada ya kuiweka CCM pembeni...Mind U nilikuwa MPINZANI, yawezekana kabisa najua hata yale USIYOYAJUA.

  Ndio tarehe 25th October 2015, tutaichagua tena CCM, tena kwa kishindo KIKUU, lakini kamwe hatuchagui kwa UJINGA..,tunazo akili, tunajua BAYA na ZURI kwetu, na hivyo..TUMEKUSIKIA, TUMETAFAKARI na TUMESHAAMUA kuwa MAGUFULI ndio Rais wetu wa AWAMU ya TANO..

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CCM.

   
 2. C

  Cool Runnings JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2015
  Joined: Feb 4, 2013
  Messages: 278
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mods, peleka hii kule kwenye thread ya Pasco tafadhali!!!
   
 3. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 13,109
  Likes Received: 16,845
  Trophy Points: 280
  huwa hauaminiki.habari zako zote ni huongo.

  swissme
   
 4. Ndalama

  Ndalama JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 8,192
  Likes Received: 5,143
  Trophy Points: 280
  Unashindana na promotor wa "Mama ongea na Mwanao"? wanakupita kama umesimama, kwi kwi kwiiii
   
 5. a

  aiai654 JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,860
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Njaa mbaya sana. Lowassa oyessss
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,194
  Likes Received: 647
  Trophy Points: 280
  Mungu hata siku moja hawezi kuibariki ccm
   
 7. mceglon

  mceglon Senior Member

  #7
  Sep 19, 2015
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mbana watu hawa iitikia hii au ndo hawataki kusikia maswala ya ccm mi napita tu hahah 👏👏👏👏✌✌✌✌✌
   
 8. wepson

  wepson JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 31, 2014
  Messages: 702
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Hawa sijui ndio wale akina haraka haraka sijui polepole wanajikanyagaaa kwa vitu vya kuunga kuunga na super gluo usitafute uwingi sema ww utampigia magufuli hakuna atakaye kushangaa
  hapa ni lowasaaa kwenda kwenye mabadiliko ya kweli
   
 9. b

  brightoni Member

  #9
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 86
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  We we nawachache mtaipigia ccm mimi nakundi kubwa tutaipigia chadema ramani ya cdm ilikuwa bungeni bwana
   
 10. malkiamrembo

  malkiamrembo JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 29, 2015
  Messages: 317
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Iili kukuthibitishia kauli zako ni uongo angalia kila anaekuja kupost au kukujibu hakuungi mkono na kwa kusema kweli hii thread haiwezi kukaa muda itakosa wachangiaji pole kwa kutusemea tuliowengi tupo na mabadilikooooo....
  Najua ni mmoja wao lkn lowassa ndiye rais wetu
   
 11. Zagazaga

  Zagazaga JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  njaa yako mbaya kabisa...nilidhani unatoa sababu za kwa nn tuichague ccm kumbe porojo tu...kwa taarifa yenu hamna anayewaelewa hata kidogo...hizo ukizotaja sifa za kijinga za chama chako...sifa za kuweka heshima bar wakati nyumbani watoto hawajala...hizo tuzo za rais wako zimesaidia vp kuboresha maisha ya watanzania!?leo tu wamarekani wamegoma kutoa msaada kwa serikali yako ya ccmm kisa rushwa...bado unataka tuwape tena!?!?mimk nashukuru Mungu watanzania wameshaamka wanajua wameibiwa vya kutosha na sasa wanataka waanze upya!!..ccm ingetimiza japo robo ya ahadi zake sasa hv wala wasingekua wanaumiza kichwa na kampeni..we endelea kuaminibuna akili nyingi..na sisi tulio malofa ambao ni wengi tutawaonyesha ulofa wetu ktk ubora wake...cccm out.. yes i said it
   
 12. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 7,435
  Likes Received: 4,474
  Trophy Points: 280
  Lakini dada Juliana Shonza unachopinga kwa Pasco ni kuita watanzania wanaoichagua ccm wajinga! Hapohapo unasema wapinzani ni wajinga!! Tafuta uwiano hapo,nani mjinga?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. m

  mkezwag JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  kwangu Mimi ccm no.na watanzania wote wanaojari future ya watoto wetu na Tanzania yetu nawashauri kusema no kwa ccm
   
 14. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,707
  Likes Received: 5,590
  Trophy Points: 280
  Lowassaaaaaaaa.... mabadilikoooooo..

  Muuza tundu wa CCM ktk ubora wake...Juliana..!!

  Umekomaaaa kama una kwashiakor...!!!


  Lowassa ni Rais tayari...!!!
   
 15. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 7,435
  Likes Received: 4,474
  Trophy Points: 280
  Sawa dada,tumekusikia,tumekuelewa,tumetafakari na tumeamua CCM NO!!!!
   
 16. p

  princeanuu Member

  #16
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 4, 2015
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowasa juuu
   
 17. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 24,559
  Likes Received: 16,656
  Trophy Points: 280
  WATANZANIA SIO WAJINGA, TUMESHAAMUA, tunasubiri kwenda taifa sherehe ya kumuapisha JPM, bhaaas!
   
 18. kababu

  kababu JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 14, 2013
  Messages: 1,535
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaan
   

  Attached Files:

 19. More Tiz

  More Tiz JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 28, 2013
  Messages: 2,234
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Juliana uandishi wako ni mzuri. Lakini unaposema CCM sio ile ile unaimanisha kupingana na wimbo wa CCM unaopigwa katika kampeni ukisema CCM ni ile ile watu ni wale wale..........

  Pia unaposema inapingana na mafisadi unaimanisha ndani ya CCM hakuna mafisadi? Je hao wanaendelea kunadiwa na magufuli Hali ya kuwa Wana kashifa sio mafisadi.?

  Unaposema CCM haijapata mgombea kwa Rushwa Hali ya kuwa mgombea anatoa maneno katika kampeni yakionyesha ni Rushwa, yakiwa ni ya kuponda na kushangaa utendaji uliopita, ukiwa unatoa vitisho vya machafuko kama ya Libya (bear in mind Tanzania tunafanya uchaguzi sio mapinduzi - au Libya nao walienda Kwenye uchaguzi na wakamuuwa Sadamu (magufuli, 2015). Je huyu mgombea anafahamu kweli anayoyaongea?

  Hata hivyo Magufuli anaonekana kama ni mgombea binafsi kwani katika mabango yake hayaonyeshi yeye yuko chama gani? Yanasomeka chagua magufuli bila nembo yeyote ya chama chake. Hiyo inaonyesha yeye mwenyewe hataki kuhusishwa na nembo za chama ndio maana kutengeneza ya kwake
   
 20. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2015
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,956
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ulikaa wapi na sisi waTanzania kuamua haya...mbona sikumbuki?

  UKAWA for state house
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...