Watanzania sio wajinga kiasi hicho na uvumilivu una mwisho


Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Messages
2,481
Likes
416
Points
180
Mzalendo80

Mzalendo80

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2010
2,481 416 180
Ndugu Watanzania Huwa sipatikumuelewa kabisa Huyu Fisadi King Kikwete kung'ang'ania madaraka wakati hawezi kuongoza nchi. Hebu nisaidie kutafakari maana nawaonea huruha watanzania wa hali ya chini jinsi wataosulubika tena kwa 5yrs ya Kifisadi na manyanyaso:thinking:
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,390
Likes
464
Points
180
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,390 464 180
Na alivyo na roho ya visasi am sure kuna watu watapotea humu kimya kimyaaaaaaaaaa
 
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
2,973
Likes
1,383
Points
280
Age
50
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
2,973 1,383 280
Kila mahali Watanzania wanasema walimpigia Dk Slaa Kura

Watanzania sio wajinga kiasi hicho.

Watanzania ni wavumilivu ila kwa hali hii ya UBABE wa CCM na NEC Watanzania wako Tayari kwa lolote.

Hata wabunge wetu kama Regia Mtema, Fred Mpendazoe ....... n.k wameporwa ushindi.

Ufisadi wa kutisha, nchi inateketea kwa umasikini.

Rasilimali zinaporwa kwa faida za vigogo na Familia zao.

Akaunti za TANAPA na NGorongoro zimesafishwa, Madini yameporwa. Watanzania tuseme NOOOO

Usalama wa T ni kwa ajili ya Vigogo???
 
G

Gurtu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2010
Messages
1,210
Likes
10
Points
135
G

Gurtu

JF-Expert Member
Joined May 15, 2010
1,210 10 135
Nimeambiwa na wakala mmoja katika jimbo la Babati vijijini kuwa mara ya kwanza msimamizi wa kura katika jimbo hilo aliposoma matokeo yaliendana na yale yaliyoko katika nakala za mawakala toka katika ngazi ya kata. Matokeo hayo yalionyesha kuwa mgombea wa NCCR aliongoza kwa kura kama 800 na kumzidi mgombea wa CCM kwa kura hizo. Baada ya hapo msimamizi akaacha kumtangaza mshindi na huku yeye akihangaika kupiga simu nje kwa muda mrefu. Katika kata mojawapo inayoitwa Mwada mgombea wa NCCR alikuwa anaongoza kwa kura kama 1993.

Hatimaye msimamizi akaanza kusoma matokeo kwa mara ya pili hadi alipofikia kata ya Mwada akitaja kuwa mgombea wa NCCR ana kura 993 (pungufu ya kura 1,000 tofauti na mwanzoni). Hizo kura 1,000 zikaongezwa kwa mgombea wa CHADEMA. Alipotaja kura za kata ya Mwada na kuonyesha tofauti na zile zilizoko katika nakala za mawakala ndipo mgombea ubunge kupitia NCCR akahoji mbona hizo kura ni tofauti na zilizoko katika nakala za fomu za matokeo toka kwa mawakala. Msimamizi akamwambia mgombea kuwa asiingiliwe na kama mtu ana malalamiko aende mahakamani. Hatimaye mgombea wa NCCR akazidiwa na mgombea wa CCM kwa kura kama 200. Mshindi akawa mgombea wa CCM.

Hali hii inayojionyesha Tanzania ambayo ni kdhulumu haki za wananchi ya kuchagua viongozi wanaowataka ni hatari kwa mustakabali wa taifa. Mapinduzi ya Ufaransa 1789 ya mwaka yalisababishwa na vitu kama hivi. Wakati huo kule Ufaransa tabaka la watu wa chini liliishi maisha yanayokatisha tamaa wakati wengine wekiishi peponi. Ilifikia hadi watu wanaandama mjini kulalamikia uhaba wa mikate lakini Malkia anasema kwamba watu watumie keki. Eti watu wakose mikate lakini badala yake watumie keki?

Baada ya matokeo ya Babati vijijini kutangazwa watu wengi niliokutana nao wanalalamika eti hawatapiga kura tena. Mimi niliwaambia kuwa kukata tamaa siyo suluhisho la tatizo. Yale matumaini madogo watu waliyokuwa nayo yameondolewa lakini Watanzania tusikate tamaa.
 
P

panchilossi

Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
16
Likes
0
Points
0
P

panchilossi

Member
Joined Nov 2, 2010
16 0 0
Kuna namna moja tu watanzania tunatakiwa kufanya, tuungane kama Baba yetu alivyotufundisha ,kuwa na umoja na kufocus na malengo tuliyojiwekea na Mungu ameshaona jitihada zetu kwamba tunahitaji mabadiliko ya kweli na yeye atafanya
 
C

Challenger M

Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
81
Likes
0
Points
13
C

Challenger M

Member
Joined Oct 31, 2010
81 0 13
kaka hata kama ana visasi kumbuka maandiko damu ya mtu kimwagika inaendelea kumlilia huyo mtu kumbuka ya kaini na abel. Kwanza utawala wake mwisho 2015.
 

Forum statistics

Threads 1,236,309
Members 475,050
Posts 29,253,708