Watanzania sasa wameanza kuelewa Serikali ya wanyonge ni serikali ya namna gani

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,904
Watanzania wengi sasa wanaanza kuona, wengi walikua wamevaa miwani ya mbao hapo kabla ila sasa mbao zimeoza wameanza kuona na kujua serikali ya wanyonge ni serikali ya namna gani.

Serikali ya wanyonge ambayo imejaa majigambo, serikali inayonunua ndege cash money young money, inajenga miundombinu mikubwa, imejenga hospitali 67 na kadhalika na kadhalika haiwezi kuwaokoa wala kuwasaidia wanyonge kwenye majanga.

Janga la Corona(covid-19 au kwa kiswahili tatizo la upumuaji) limekuja kuiumbua serikali ya wanyonge ambayo ilikua inajigamba ina pesa za kulisha nchi miezi 5 wakati wa dharula kumbe hakuna hata 100.

Serikali ya wanyonge inazuia shughuli za kijamii kama mazishi lakini inaruhusu shughuli za bar, clubs, mikusanyiko mingine yenye lengo la kibiashara ili angalau ipate hela. Kwamba mkienda kuzika mtaambukizana ugonjwa aa matatizo ya kupumua ila mkiwa bar mnakunywa hamuwezi kuambukizana. Imeacha shughuli za ibada ziendelee kwa sababu wanatafta huruma kwa viongozi wa dini watafuna sadaka.

Watu wanajiuliza mbona serikali ya wanyonge ya dona kantri mbona inajali sana pesa badala ya utu, jibu ni moja tu serikali ya wayonge ndani ya dona kantri haina uwezo wa kuendesha nchi wakati huu wa ugonjwa wa matatizo ya upumuaji aka covid-19.

Nchi kama Rwanda na Uganda wakati huu wa ugonjwa wa upumuaji aka covid-19 wameonyesha wanaweza kuendesha nchi zao kwa miezi kadhaa ya dharula na pesa ipo ila sio dona kantri.

Majigambo ya viongozi wa serikali ya wanyonge ni debe tupu linalipiga kelele ndani hakuna kitu. Dona kantri sasa tuunakua sembe kantri.
 
Gambino,
Pole in advance kwa namna watakavyokushukia.Naunga mkono mtazamo wako,hii serikali ya wanyonge inaongopa ile mbaya.Kwa kawaida mwenye fedha utamfahamu kwa matendo/matumizi.Asiye nazo sasa,hujaza wallet karatasi/matambara mabovu ili ionekane ana pochi Nene kumbe geresha.

Hawaajiri,hawapandishi vyeo,mishahara tangia JK,hakuna OC maofisini,wanakopa mikopo mikubwa ndani na nje halafu wajiite wana fedha cash?

Tumetekwa na hatuwezi kujinasua iwapo hatutashikamana.Maadui wanatumia vema kanuni ya Divide & Rule,Mara sasa ni NCCR,majuzi ilikuwa ACT Wazalendo na kabla kidogo CUF ya Professor.Tuwe makini!!!
 
Halafu jamaa kajifungia "CHATLE" toka kabla ya pasaka, mpaka leo. Tunamlipa mshahara kutoka kwenye kodi zetu, ila hataki kufanya kazi.

Yupo bussy kuchat na Gerson, waambie watanzania wachape kazi na wasali. Ye mbona hataki kurudi dodoma au dar akafanye kazi?
 
Mnashindana kuanzisha threads 100 kwa siku, mnasahau 98% ya hao watanzania wala hawapo mitandaoni. Ukipewa LIKES 78 kama utabahatika utajiona umepata sapoti ya watanzania kumbe wala hata haijafika 30% ya walio JF. Baada ya uchaguzi October lete mrejesho wa hao wanyonge walioielewa serikali hii ya namna gani.
 
Jmc06, dunia imo viganjani mwa watu sasa hivi.
Kama mitandao isingekuwa na madhara mkuu wenu na serikali yake wasingekuwa wanakesha kuwatafuta watumiaji wa mitandao, au kutaka kuifunga.
Tumia akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
98% ya watanzania hawako mtandaoni?
Ni karibu nchi nzima haiko mtandaoni. Huu ni uwongo wa kiwango cha lami.
Siku izi smart phone zimefika hadi vijijini huko ndani ndani.

Huyu anawaza kama yule kiongozi wa malaika,wanawachukulia Watanzania ni wajinga sana.Usiwaamshe waliolala,tuendelee kuelimishana kupitia mitandao maana ujumbe unawafikia wengi.
 
Mnashindana kuanzisha threads 100 kwa siku, mnasahau 98% ya hao watanzania wala hawapo mitandaoni. Ukipewa LIKES 78 kama utabahatika utajiona umepata sapoti ya watanzania kumbe wala hata haijafika 30% ya walio JF. Baada ya uchaguzi October lete mrejesho wa hao wanyonge walioielewa serikali hii ya namna gani.
Msimu huu wa Corona ya mwaka 2019 watu wengi wana Viswaswadu simu janja wengi wameuza hali ngumu.Hata yangu ipo hatarini kuuzwa.
 
Ameshindwa hata kubaki ofisini aongoze mapambano kweli hatuna mtu kipindi hiki.
 
Mnashindana kuanzisha threads 100 kwa siku, mnasahau 98% ya hao watanzania wala hawapo mitandaoni. Ukipewa LIKES 78 kama utabahatika utajiona umepata sapoti ya watanzania kumbe wala hata haijafika 30% ya walio JF. Baada ya uchaguzi October lete mrejesho wa hao wanyonge walioielewa serikali hii ya namna gani.
Unawaza uchaguzi tu, dalili za kukosa hoja.

Unafikiri CCM wanashinda uchaguzi kwa sababu ya kupendwa, waambie wakubali iwepo tume huru ya uchaguzi kama hawajakaa saa tano ya asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini wanajitahidi jamani, kwenye ile akiba yetu ya 5.3 mil. USD wametoa kiasi fulani cha hela na kununua ventilator moja kwa ajili ya hospitali ya Corona ya Amana.
Kwa hiyo watakaougua Corona na ku- develop complications za kupumua, msijali, kuna ventilator moja tu inawasubiri Amana.
 
Halafu jamaa kajifungia "CHATLE" toka kabla ya pasaka, mpaka leo. Tunamlipa mshahara kutoka kwenye kodi zetu, ila hataki kufanya kazi.

Yupo bussy kuchat na Gerson, waambie watanzania wachape kazi na wasali. Ye mbona hataki kurudi dodoma au dar akafanye kazi?
Hataki kufanya?,wale makatibu wakuu wa wizara walioapishwa majuzi ULIWAAPISHA WEWE?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom