Watanzania sasa tumechoka na Tanesco, tunataka suluhisho la kudumu...

Negative

Member
Dec 26, 2010
17
0
Kwa muda mrefu sasa tatizo la umeme kukatika limekuwa likitokea mara kwa mara na mara nyingi ikiripotiwa kusababishwa na kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, ndugu zangu ikiwa kila mwaka hali hii inajitokeza kwa nini Tanesco wasitafute njia nyingine ya kuwahudumia watanzania? na kama hawawezi kwanini serikali isiruhusu sekta binafsi ikatumia njia mbadala??
Kwa yeyote anayetumia nishati hiyo katika shughuli zake za kila siku bila shaka analitambua hili, hali hii inachosha na inakera, nataka rais atoe tamko juu ya hili, kama hawezi pia aseme tujue kama tutumie kinyesi kuzalisha wenyewe nishati hiyo ama vip...
 
Hata kama waafrika hatuna uwezo wa kujifunza kutokana na historia, hebu tujaribu kufikiri kidogo tu, ni hasara kiasi gani nchi tunaingia kwa saa moja pale ambapo nchi inakuwa gizani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom