Watanzania polepole wanaanza kujenga misuli ya kukataa uonevu!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru kuna kila dalili kwamba Watanzania wameanza kujenga misuli ya kukataa kuonewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na Serikali iliyoko madarakani. Ikumbukwe Watanzania hawakuwahi kupitia uonevu, unyanyasasaji au ukandamizaji wa aina yoyote kabla na baada ya uhuru zaidi ya Biashara ya Utumwa na utawala wa Kikoloni ambao haukuwa na unyanysaji kama uliokuwa ukifanyika kwa ndugu zetu wa nchi nyingi za Africa hasa Kusini mwa Afrika kama SA, Zimbabwe, Angola, Mocambique,Namibia n.k.

Tanzania tulibahatikam kupewa Uhuru na mkolone kwenye kisahani. Hakukuwa na mapambano ya dhati ya kuingia msituni kama wenzetu wa Kusini walivyopambana. Kwa mantiki hiyo Watz wakawa wamebweteka baada ya kujitawala bila kumwaga damu. Mwaasisi na Baba wa Taifa hili J.K. Nyerere(rip) hakutaka kutumia mabavu au vurugu kuwaletea Watz uhuru. Hivo basi hata baada ya Uhuru Mwalimu alitamani kudumisha Amani, Upendo, Umoja na Mshikamano huku akiwasaidia nchi za Kiafrika nao wajitawale ingawa ni kwa mtutu.

Mwalimu alishatuacha tangu 1999 na akaiacha nchi hii ikiwa na Amani yake,Upendo wake, Umoja wake na Mshikamano wake. Mwaka kesho 2019 Tanzania itakuwa inatimiza miongo 2 bila ya Mwalimu na hali aliyoacha ni kwa sasa ni kinyume kabisa. Chama alichokiasisi Baba wa Taifa CCM, leo kimegeuka kuwa ni Chama cha kikaburu na kijinasibu kwa kuvunja misingi ya Ubinadamu kwa kiwangi cha hali ya juu. Watanzania kwa sasa kila kona wamejaa hofu, mashaka na wasiwasi. Hwajuia kesho kutatokea nini. Vyama vya Upinzani Tanzania kwa sasa viinapigwa vita kila kona na kuna kila dalili ya kutaka kuua na kufuta kabisa kitu kinachoitwa mfumo wa Vyama Vingi kama Katiba inavyoelekeza.

Utawala wa awamu ya 5 umeingia na sera za ajabu za kupambana na vyama vya siasa kana kwamba ni Maadui wa Chama Tawala CCM na Serikali yake. Kinachoonekana kwa sasa ni Utawala wa hila, unafiki,ujanjaujanja na ulaghai wa kuwazubaisha na kuwafanya Watanzania kuwa ni wajinga na wasio jitambua. Kwamba Serikali inawa hadaa Watanzania kuwa inajenga Viwanda kwa hiyo haitaki kusumbuliwa na Vyama vya Upinzani. Kwamba Serikali inawanunua au kuwatia hofu Wabunge na Madiwani wa Upinzani ili WAHAMIE CCM na wakihamia CCM wana andaliwa mazingira ya KUSHINDA KWA NAMNA YOYOTE ILE HATA KAMA NI KUMWAGA DAMU...Haya tumeyaona juzi Kinondoni na Siha.Kwamba CCM, Serikali, Polisi na TISS walipanga lazima Wagimbea wao washinde kwa vyovyote. Dunia imeshuhudia Masanduku ya Kura yakiporwa na kurudishwa mchana kweupe chini ya mtutu wa Bunduki.

Tumeshuhudia Wapinzani wakinyimwa barua za viapo vya Mawakala na hata waliopewa walizuiwa kuingia kwenye vituo kwa wakati!!Sababu ni kuhakikisha CCM inashinda.Pamoja na Wapinzani kulalalmika kwa TUME/NEC na Msimamizi wa Uchaguzi ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Hii ilipangwa kwamba kwa hali kama hiyo lazima Upinzani ungehamanika kwa vovyote na kuchukua jukumu la kwenda kudai barua za viapo..!! Hapo ndipo Polisi walipataka ili wapate nafasi ya kutumia SILAHA ZA MOTO(LIVE BULLETS) kuwamaliza wapinzani kwa risasi halafu mwisho wa siku wao wanageuziwa kibao cha kusababisha vurugu na kukiuka sheria ati ya Vyama vya siasa na hivo basi MSAJILI AANDAE UTARATIBU WA KUIFUTA CHADEMA...!!!

Polisi waliomwua Mwanafunzi Acqulina Akwilini hivi sasa wanakula bia tu wala hawana shaka maana wanajua kabisa mpira wanao CHADEMA na lazima waucheze na wafungwe magali...!!
Leo hii Wapinzani na Asasi za kutetea Haki za Binadamu wanaiambia Serikali kuwa Uchaguzi haukuwa Huru na Haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji mwingi wa Haki za Binadamu na utumiaji wa Nguvu za Polisi uliopitiliza na hivyo Katiba kuna lazima sasa kurejea kwenye Mchakato wa Katiba Mpya, Serikali wanasema KATIBA MPYA SIYO KIPA UMBELE CHAO wanataka KWANZA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI....!!??Kweli?

Ni Serikali ya wendawazimu tu ndiyo inaweza kuwaza na kuongea lugha za kifedhuli kama hizi. Kiongozi mwenye hekima, busara na uweledi hawezi kudai ati KATIBA siyo MUHIMU ila MAENDELEO ndiyo muhimu....???Unawezaje kuwaletea Watu maendeleo katika mazingira ya yasiyo na Amani?? Maendeleo yanapatikanaje katika mazingira ya ubabe,ukoloni mamboleo na Ubaguzi unaovuka mipaka??EU na Marekani wamepiga kelele katika hili....Lakini Waziri wetu wa Foreign Affairs anajibu kwa hoja nyepesi za mtu aliyelewa madaraka....Kwamba kwanini leo EU na US wanalalamikia ukandamizaji wa Demokrasia ilhali wakti wa MAUAJI YA KIBITI walikaa kimya??Hii ni akili ya ajabu sana. Kwamba sasa UN,EU au US waanze kufanya kazi ya kuifundisha Serikali kulinda raia wake. Maana yake ni kwaba kunapotokea tukio la watu kuuawa au kupotezwa na WATU WASIOJULIKANA basi lazima UN, EU, US na Jumuia za Kimataifa zipige kelele....!!!Je, hiyo itakuwa ni Seikali ya aina gani inayosubiri kila kitu kuambiwa ndiyo igutuke...???Hii ni aibu ya karne kwa kweli.

Marehemu Muamar Ghadaffy alikuwa akiwapa Wananchi wa LIBYA kila kitu bure. Ukimaliza Chuo Kikuu hujapata hata ajira unaanza kulipwa Mshahara, unapewa Nyumba unakaa bure, ukitaka kuoa unalipiwa mahari na gharama zote za Harusi. Lakini hawa watu hawakuwa na Uhuru ndani ya nchi yao...!!Polepole walianza kuchoka na mfumo wa maisha hayo ya kupewa kila kitu bure lakini hawana Amani,Uhuru na Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa. Kilichotokea baada ya hapo leo ni Historia. Serikali ya CCM inacheza mchezo wa Muamar Ghaddafy....na kadri siku zinavyosonga mbele Watanzania wanaanza kubadilika na kuwa kama Walibya.....!!Huwezi kuwa-fool watu kwa Sera ya Viwanda, Flyovers, Bombadier, SGR and the like iliwahali umewabana mpaka pumzi ya mwisho...!! Hii ni sawa na mtu anajaza upepo kwenye futuza lililojaa upepo tayari lakini unaendelea kushindilia tu.....mwisho wake ni mpasuko kama bomu....!!
 
Subiri uharo wa Lumumba

Lumumba najua hawana hoja katika hili. Sisi tulio Wazalendo wa nchi hii tunawaambia ukweli na uwazi kungali mapema ili wachague kusuka au kunyoa.....!
Lazima wajue kuwa katika haya maovu wanayowafanyia baadhi ya Watz kuna kitu wanakiumba bila kujua na siku kitakapokua na kukomaa muziki wake hawatauweza...!! Hivi Jeshi la Polisi wako maelfu mangapi haya unganisha na JWTZ na TISS dhidi ya Watz milioni 50 nani atawazuia???
 
Kwenye kampeni Dotto aliahidi mengi kwa wa Tz tena kwa lugha ya upole na unyenyekevu kama tulivyo wa Tz .Dotto aliweza kupiga pushup, alionge karibu lugha zote za makabila Tz. Aliahidi kufanya kazi na chama chochote, Aliwapa matumaini mapya Waja wake. Sasa huyo Kulwa sijui walimpata wapi. Yeye akawa tofauti sana na Dotto, kuongea kwa upole, makashkash, na kuwaombea waja wake waishi kama mashetani, ghafla wapizani ni adui wa Taifa , na hapo ........hapana hili la matukio niliache kwanza. Ila kwa kinachotokea naelewa Kulwa alichosema kwamba ALISUKUMIZIWA tu huko baada ya kubeep.....

Kwahiyo Kaka ndo matokeo yake hayo uliyochambua.
Ninaimani Dotto atakuja tena 2020 kwa lugha ya upole zaidi maana ataona nguvu ya waja wake, baada kuona alichokifanya Kulwa Kimewachukiza baadhi yao aliowapa matumaini akiwa jukwaani 2015
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom