Kupanga ni kuchagua. Hakuna haja ya kulaumu tena kwamba maisha ni magumu. Adhabu tumeitaka wenyewe. Kwa hapa Marekani, Chama kinachosababisha umaskini kwa namna yoyote ile, kinanyimwa uongozi wa nchi hata kwa miaka 20. Sasa Tanzania ni kinyume. Haiingii akilini kwa mfano: watu wa Singida ambao vijumba vyao ni mithili ya vichuguu wanampa kura Kikwete! Poleni! Ni miaka mingine mitano ni taabu, mahangaiko, umaskini na huzuni. Hakuna tena kunufaika kwa madini. Ni balaa! Nani wa kulaumiwa? Maana hata kama kura zimeibiwa mbona vyama vya siasa, viongozi wa dini, taasisi mbalimbali hakuna aliyesimama kupinga kwa maandamano? Baadala yake viongozi wa dini wamehudhuria kuapishwa kwa Kikwete. Hakuna nabii miongoni mwao? Siasa tunaifanya kama ushabiki wa Yanga na Simba bila kuangalia uhalisia wa maisha. Tujiandae sasa kwa mfumuko wa bei na ufisadi uliokithiri. Ufukara sasa ndio jadi ya watanzania! Poleni.