Watanzania ni wavivu sana kazini tubadilike!!

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,093
1,894
Salaamu kwenu,

Nimejikuta nikiandika uzi huu mfupi, nikiwa nasikitishwa sana na taabia mbovu na uvivu/utegeaji mkubwa wa vijana wakitanzania katika shughuli mbali mbali za kujiongezea kipato.

Binafsi nina Biashara inayoniingizia kipato na nimeajiri vijana wawili kwa kazi hiyo. Mmoja binti na mwingine mvulana.
Watu hawa wanekuwa kero hasa inapotokea nipo safarini.
Kila ahsubuhi nikuomba udhuru, mara naumwa naomba kwenda hospital, mara nitachelewa kidogo.
Mara naenda kanisani, mara misiba.... na sababu chungumzima. Leo huyu kesho yule.
Wakati wa kuomba kazi wanatia huruma kabisa, wakianza kazi wanaanza mazoea.

Hivi najiuliza watanzania tuna matatizo gani? Japo naamini si wote ila hawa wanawakilisha asilimia kubwa ya tabia zetu.

Ofsn pia naona jinsi watu wanavyofanyakazi kwa mazoea, kuna kundi la wachelewaji na kuwahi kutoka ofsn.
Kuna kundi la wanaowahi ofsn na kuanza kupiga soga, saa mbili mpk saa nne wapo kanteen kwenye chai ️, kusema wenzao wanaochelewa huku wao wakiwahi na hakuna la maana wanalofanya kwa muda mwingi.

Huduma kwa wateja wa nje ni mbovu sana hapa kwetu Tanzania katika sehemu nyingi, mtu anaongea na simu au kuchat huku mbele yake kukiwa na mteja. Katikati ya maongezi na mteja anatokea shosti wanaanza kuongea na kukatiza mazungumzo na mteja mara kwa mara tena story zisizohusiana na kazi.
Mara mtu kanuna bila sababu na hakujui. Unahudumiwa mfano huduma za kifedha, fedha ni zako lakini unahudumiwa kama vile unapatiwa msaada.
Unapiga simu za huduma kwa wateja hazipokelewi!

Najiuliza sana, kwa nini mambo haya!

Inasikitisha sana .
 
Naunga mkono hoja yako. Tuambiane ukweli tusaidiane. Inakera sana.
Kazi ya kumaliza juma moja inakaa mwezi. Na kila siku watu wanaamka wanaenda kazini asubuhi.
 
Mkuu umenena ukweli mtupu,nadhani ni hulks ambayo ipo ndani ya damu ya watanzania walio wengi!

Tena kwenye taasisi za umma ndiyo kabisaaa,nilifika taasisi moja nikakuta kuna watu 2 wanasubiri huduma,(mimi wa tatu) nawauliza mbona hamuingii kupata huduma naambiwa "tumeambiwa ngoja tuongezeke,tuwe wengi wengi),nikaingia kwa lazima ndani na kuwauliza jamani mbona hamtupi huduma,wakanambia tutaanza kutoa huduma mkiongezeka ongezeka!!(khaaaaa!!)

Nikawauliza kama wengine wasipokuja je? Eti watakuja tu,halafu hata hawashtuki,wanapiga soga na kuonyeshana simu!!!

Nikawaambia huo ni utaratibu wenu wa kazi au mumejiamulia wenyewe!!??
Akatika mmoja na kuniambia " njoo nikuhudumie uende"

Hao ndiyo watanzania sasa!!!!
 
Huu ni moja ugonjwa unaishambulia kwa kasi miongoni mwetu na haswa vijana, hii hali isipodhibitiwa kuna hatari kubwa mno mbele yetu kama taifa.
Simu au mitandao ya kijamii, ulevi , soga kipindi cha kazi vimekuwa ni adui mkubwa sana, pia betting nayo imewafanya vijana wengi kuwa wajinga na wavivu kupindukia
Tubadilike.
 
Naunga mkono hoja yako. Tuambiane ukweli tusaidiane. Inakera sana.
Kazi ya kumaliza juma moja inakaa mwezi. Na kila siku watu wanaamka wanaenda kazini asubuhi.

Inakera sana sana, kila mtu yupo ofsn ila majuma yanakatika tu bila chochote kufanyika
 
Muda wote ni kununa nuna wanawaza kila mtu anataka kuwatongoza, tabia moja hovyo sana
Tena ukiwauliza chochote wanakua wajeuri sana hawakawii kukujibu vibaya wanaona kama unawasumbua na kuwapotezea muda.
 
Naunga mkono hoja, sasa ukitaka ukorofishane na mmoja wao mwambie ukweli "timiza wajibu wako" mh
 
Nikuunge mkona mtoa hoja

Mimi kazini kwangu hamna kazi kabisa japokuwa nakaa naangalia muvi na muziki. Swala linapokuja ni kwamba hakuna mikakati ya kufanya na malengo ya tunataka kwenda wapi

Kumbuka kama hujui unapotaka kwenda huwezi potea na tatizo letu watanzania hatufundishwagi kuwa wawajibikaji kabisa na hii inatokana na malengo tunayojiwekea mfano ya muda mfupi na muda mrefu. Wewe shangaa kwenye serikali yetu mpaka kiongozi ndo agundue kwamba mambo hayaendi sawa ndo aanze kuleta siasa na akiondoka basi tena ni kama moto wa kiberiti
 
Wengi kwenye biashara huajiri foreigners. Ukimueeka Mrundi au Mmalawi hakuna kuomba ruhusa za kwenda msibani. Anahesabu hela yake baada ya miezi sita atafanya nini.
 
Tumepata malezi Malaya, malezi yasiyothamini uwajibikaji sehemu ya kazi.
Tatizo ni kubwa kwenye mashirika ya huduma kama Tanesco, DAWASCO nk ingawa wapo pia wafanyakazi wanaowajibika na kuheshimu kazi zao
 
Ila kuna baadhi ya taasisi hakuna kazi kabisa week nzima.so unachofanya ni kutimiza wajibu tu wakufika ofisini.

Naukifika kwa sababu hakuna kazi ndo kamahivyo. Simu na mitandao ya kijamii na kuangalia movie ndo kazi yangu sasa nifanye nini zaidi ya hapo
 
Kiongozi hapo hulaumiwi, lakini kuna ambao kazi zipo lakini hawataki kuwajibika, ilhali utakuta kazi hiyo aliisotea kwa muda mrefu akibembeleza kwa rushwa, maneno mengi na ahadi kemkem za utendaji bora, lakini akipewa kazi baada ya muda mfupi anajisahau, ikitokea kapigwa chini basi atahangaika kwa kila mganga aroge ili arudishwe kazini!.
 
Back
Top Bottom