Watanzania Ni wavivu kunywa maziwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
KWA UFUPI
Meneja wa Mradi wa Kuboresha Ng'ombe wa Maziwa Afrika ya Mashariki (EADD II), Mark Txoso alisema hayo alipoutambulisha mradi huo utakaotekelezwa katika halmashauri tisa za mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya.


Mbeya. Kila Mtanzania anatakiwa kunywa lita 200 za maziwa na siyo 46 za sasa kwa mwaka mmoja ili kuondoa sumu mwilini na kujenga afya imara, ilielezwa.

Meneja wa Mradi wa Kuboresha Ng'ombe wa Maziwa Afrika ya Mashariki (EADD II), Mark Txoso alisema hayo alipoutambulisha mradi huo utakaotekelezwa katika halmashauri tisa za mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya.

Mradi huo unakwenda sambamba na mradi kama huo ulioko katika nchi za Kenya na Uganda.

Txoso alisema Mashirika ya Kimataifa ya Chakula na Kilimo (Fao) na Afya (WHO) yalishaweka viwango vya kila mtu duniani kunywa walau lita 200 za maziwa kwa mwaka ili kuuweka mwili katika afya bora, lakini Watanzania wanakunywa kiasi kidogo zaidi cha maziwa ikilinganishwa na nchi nyingine.

"Watanzania wengi hawanyi maziwa au wanakunywa kidogo. Hali ni mbaya kwa sababu, wengi hawafikishi lita 200 kwa mwaka kama ushauri unavyoelekeza," alisema.

Alisema mradi wa EADD II unalenga kuboresha ufugaji wa ng'ombe wa maziwa katika Halmashauri za Kilolo, Iringa Vijijini na Mufindi mkoani Iringa, wakati Halmashauri za Njombe ni Wanging'ombe, Njombe Vijijini na Njombe Mjini na Mkoa wa Mbeya ni Rungwe, Mbozi na Mbeya Vijijini.

Alisema mradi utalenga kuboresha mifugo inayotoa lita 5-7 kufikia lita 18-20 kwa mkupuo na kwamba pia utaboresha malisho na aina ya ng'ombe.

"Kila halmashauri mkoani humo italazimika kufungua kituo kimoja cha kushughulikia maziwa na mipango mingine na wafugaji 35,000 wanatarajiwa kuanza katka mradi huo," alisema.

Chanzo
: mwananchi.co.tz






 
Kisa mnataka kuuza maziwa!!
Hivi watoto wanaonyonyeshwa na mama zao kwa miaka miwili mliwahesabu?
 
Back
Top Bottom