Watanzania ni watu wa matukio, Joka ni CCM tuliuwe haraka sana

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Inaonekana tumezoea kuwa watu wa matukio kila kunakucha na huhamishwa mawazo na fikra kuelekezwa kwenye jambo na hufurahia na kushangilia yanayojiri bila ya kujua chanzo ni kitu gani ? Chanzo cha yote hayo ni nini ?

Tunabakia watu tuliogubikwa na mijadala mirefu na mwisho wake unafanana na matukio yaliopita. Inakuwa tunaendeshwa nchi yetu kwa matukio ,Raisi anachagua wengine.

Tunakaa na kuulizana baada ya mambo yamekwishatokea ,tukutane bungeni ,tukutane kwenye mijadala ,inakuwaje jambo likishatokea ndio tuulizane ? Hivi haya mambo hayana chanzo ,hivi yalifanywa kwa kutumia intelijinsia kubwa kiasi gani ? Haikuwa hivyo ila udhibiti wa mambo ya nchi ni dhaifu,mifumo iliyopo ni dhaifu ,leo ndio Stanbik wanasema uwekaji hela haukufuata taratibu halikadhalika utoaji nao pia haukufuata taratibu na ufungwaji hesabu nao haukufuata taratibu ,hivi hapa nani wa kuwajibika ?

Yote haya ni ubovu wa katiba tuliyonayo na tunayotaka kuwekewa na miccm, Katika ulimwengu wa leo utaratibu wa kuenenda katika jamii na Taifa lolote lile ni Katiba na sisi tumeamua kuandika Katiba Mpya na Bora. Ni Katiba Mpya na Bora ndiyo pekee inaweza kuwa silaha ya mwisho kuliangamiza liccm, ikatae katiba iliyopitishwa na ccm kwa hali yeyote ile.

CCM ni joka ambalo limekuwa likitaga mayai kama vile Epa, Majengo ya Benki Kuu, Richmond na haya ni mayai ambayo tumeyaokota mchana kweupe ,kesho na keshokutwa baada ya joka kuona mayai yake yanaokotwa mchana kweupe litatafuta njia nyingine ambayo itakuwa ngumu kuyaona mayai haya..
 
Back
Top Bottom