Watanzania ni watu wa amani, Tanzania sio ya amani

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,569
2,000
Nimetafakari sana visa vingi vinavyofanywa na vilivyowahi kufanywa na watawala kwa wananchi wa Tanzania.

Vuta picha askari polisi wanavyonyanyasa raia katika mambo mbalimbali halafu hawarushiwi hata jiwe wala nyumba zao hazipati shida wakati tunaishi nao huku mitaani.

Fikiria maamuzi ya kukurupuka yanayotolewa na yaliyowahi kutolewa na viongozi bila sababu za msingi halafu linganisha na reaction ya wananchi ilivyokuwa simple tu.

Hili la Jana la Simba na Yanga ni sehemu ya kuonesha namna Watanzania walivyo watu wa amani.

Haiwezekani nchi nyingine raia wengine watoe kiingilio, wapoteze nauli, muda na kuacha shughuli zao halafu waishie kufukuzwa kwa mabomu kwa barua ya TFF ambayo haikueleza sababu ya mechi kusogezwa mbele.

Mashabiki wa mpira ni watu wa hisia sana na wako wengi sana. Kwa umoja wao wanaweza kuamua lolote ndani ya dk1 na kuleta madhara makubwa sana hivyo ni muhimu kutenda kwa tahadhari kubwa sana unapoamua jambo linalowahusu. Hii ya Jana haikuwa na tahadhari yoyote na lolote baya lingeweza kutokea.

Viongozi ni jambo la msingi sana kuacha kupima kina cha maji kwa kuyakanyaga ipo siku mtazama.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,246
2,000
Bi Mkubwa kavuruga sanaaaa. Kiatu cha JPM ni dhahiri shahiri hakimtoshi katu.

#Mtanikumbuka kwa mazuri.
 

kifukumkunyi

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
207
250
Ni kweli kabisa ulivyoongea, kuna matukio mengi ambayo Tanzania yametokea kama ni nchi nyengine basi watu wangeingia barabarani , lakini sisi kazi yetu kubwa nikurikodi video halafu kurushiana kwenye mitandao tu. Sijui ni amani au ni nidhamu ya woga.
 

Zogoo da khama

JF-Expert Member
May 20, 2013
597
1,000
Kaka sie sio watu wa amani, woga,hofu na kutojitambua haki zetu za msingi ndo zao la haya yote.

Issue ya jana wengi wanaagalia Simba na Yanga nani yupo sahihi basi lakini hawaangalia upande wetu tuliojitokeza uwanjani, muda wetu, pesa yetu, gharama za usafiri nani atatulipa?

Kuna raia wametoka sehemu mbalimbali kwa mabasi, ndege, usafiri binafsi na mwengine alitembea toka Kigoma hadi Dar je nani alimfikiria, Yanga kuamua kutoa timu kwa kusimamia kanuni wapo sahihi lakini vipi upande wa wanachama wao? Simba walikubali kanuni ivunjwe ili kuwaridhisha wapenzi wao je kuna kosa hapo?

Leo hii ukisimama ukasema tususie kwenda uwajani kwa michezo yote iliyobaki, wangapi wataunga mkono hoja hiyo?

Binafsi nimeumia sana, kulipa kiingilio harafu mpira usichezwe, mwisho tunapigwa mabomu ya machozi kama wahalifu, je ndo fadhila tuliyostahili? Tafakari chukua hatua!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom