Watanzania ni watalii mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi duniani-viena austria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ni watalii mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi duniani-viena austria

Discussion in 'Jamii Photos' started by BabaK, Jul 19, 2010.

 1. BabaK

  BabaK Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wakati lengo la mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi duniani likiwa ni kujadili na kuonana maendeleo na mafanikio katika nchi mbalimbali Tazania tukiwa wamoja wao lakini banda letu limekuwa kama vile hakuna kitu kinachoendelea kuhusu masuala hayo.
  tz.jpg
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mambo ya wabong utayaweza ndugu yangu?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kigezo cha kutalii hapo kiko wapi?
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndio maana nakubaliana na wanaosema HIV AIDS is an industry. Labda mleta mada tuambie kwenya banda la tanzania tulitakiwa tuonyeshe nini.?

  Reaerches za kisayani nyingi za tanzania tunashirikiana na mataifa au vyuo vya nje inawezekana hatuna hata hatimiliki ya matokeo ya tafiti hizi

  Labda kwenye mabanda haya wachaguliwe waheshimiwa waathirika wachachache wenye HIV watumike kuombea misaada ya ARV zaidi. waongee na wafadhili kuwa afya zao zimeboreka na tuombe ARV zaidi. na ikiwezakana tuombe hata condoms ndogo ndogo kwa ajili ya vijana wa primary. teh teh teh
   
 5. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nimeshiriki mkutano wa Toronto mwaka 2006 na mkutano wa Mexico 2008 nimekosa huu mkutano, lakini ni kweli kuwa watanzania huwa hawatulii kwenye vipindi/seminars/workshops/presentation/discussion/prenary wanakuwa wanapuyanga mitaani kufanya shopping hata kununua malaya kwa mapesa ya allowance wanayolipwa. Kwa mfano wawakilishi wa serikali hulamba zaidi ya $ 300 PDM, mkutano ni wa siku tano lakini unakuta ana ticket ya siku 10 maana yake anawahi siku mbili kabla na kuchelewa siku tatu juu kwa kisingizio cha kuwa ndege zilikuwa zimejaa. Tanzania kila sehemu ni wizi wizi. UKIMWI unaambukizwa na kuturudisha sana nyuma kimaendeleo lakini kuna watu wanatamani UKIMWI usiishe leo wala kesho maana WANAFAIDI, kwao ni Biashara.
   
 6. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KWELI KABISA KAMA HAPAKUANDIKWA KITU BILA HATA KUWA NA BANGO INA MAANA HATUKUSHIRIKI,..BY the WAY Tanzania tuna tafifiti za ukimwi kweli au ndio,...sisi ni questionnaires and data collectors kama sivyo natumaini zile data za mapolisi waliokubaki kuwa MA SUBJECT wa ukimwi zingekuwepo na picha za hali zao,...Otherwise Ni mambo yale yale ya MEJA GENERAL HERMAN LUPOGO KUONGOZA mapambano ya ukimwi kwenye TACAIDS,MWANAJESHI AMBAYE HAJUI NINI MAANA HATA YA ASPIRIN....
  Na kutumia WAALIMU KUGAWA CHANJO YA UGONJWA WA KICHOCHO,...wanafunzi waliopata madhara baada ya kutumia hizo dawa walikuwa wanakimbizwa hospitalini,...na kwenye zahanati za vijijini ambako hakukuwa na mkakati angalizo,...ya kujiandaa na madhara ya dawa hizo[side effects],...basi matokeo yake yalikuwa ,.
  ni kumbiza watoto hospitalini tu ,..huku wahusika wakikazana kujitetea hamna mtoto aliye kufa,..
  Bado nashindwa kuelewa,huwa inakuwaje kuamua kuendesha shughuli fulani bila kuwahusisha wadau husika katika kuprogram kitu,.au kukisimamia????

   
 7. h

  housta Senior Member

  #7
  Jul 20, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maybe he mean't to say wamealikwa lakini hawajatokea.Or wamealikwa,wamekwenda(na kula pesa za kujikimu) LAKINI hawana muda wa kuonyesha chochote kwenye banda lao.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Jamani...labda tuangalie kidogo mpangilo wa hii mikutano.
  Mikutano hii ya kimataifa, siyo kama mkutano wa wanachama wa club ya...... mpangilio wake ni tofauti sana.Inakuwa kama hivi:
  1. Plenary - hili ni jumuiko kubwa la waliohudhuria mkutano na wanaweza kuwa kwa mamia kama siyo maelfu.Kwa kawaida hapa ndio utaona watu kama viongozi wa msafara ( mawaziri au viongozi wengine wa taasisi mbalimbali including NGOs), wataalamu wengine nk wakitoa speech zao, na statements na kutoa mada zilizopangwa kwenye ratiba
  2. Side meetings/Caucuses/workshops - hii ni mikutano inayoendeshwa sambamba na mkutano mkuu. Mara nyingi hii huwa na themes mbalimbali na watu huchagua wanataka kuhudhuria ipi.
  3. Maonyesho/exhibitions - haya maonyesho hufanywa na washiriki kuonyesha mambo mbalimbali ikiwemo machapisho, n.k.

  NB: Ni vigumu sana kuweza kujua kama Tanzania tumeshiriki vipi katika kila level maana hii hutegemeana na ukubwa wa delegation iliyoenda huko.Ninafahamu kwa mfano Tanzania tuna washiriki kutoka Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na nje ya nchi.Na najua baadhi wako kwenye ratiba ya kutoa mada katika maeneo mbalimbali.

  Kuhusu kufanya shopping wakati mkutano unaendelea, hili siyo tatizo la watanzania peke yao. Hata washiriki kutoka nchi nyingine na siyo za kiafrika tu hapa za ulaya hufanya hivi japo wazungu siyo sana kama waafrika. Mjue kuna kitu kinaitwa " conference tourism' hii ni fursa mtu huipata kuona nchi nyingine akiwa anahudhuria mkutano ughaibuni na kwa wale walioko kwenye tasnia ya utalii watanielewa naongelea nini. Ni kama WC ilipokuwa inaendelea ( japo havifanani sana) mtu anaenda kuona mechi lakini hapo hapo anachukua fursa ya kuwepo huko kuona vivutio vingine ikiwemo kufanya shopping.
  Huko Vienna ni zaidi ya AIDS CONFERENCE 2010 - NI BIASHARA KUBWA inaendelea - madukani, mahotelini nk na ndio maana nchi hugombea ku host mikutano maana ni njia moja wapo ya kufanya biashara na kuingiza pato.
   
 9. Salha

  Salha Senior Member

  #9
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh!
   
Loading...