Uchaguzi 2020 Watanzania, ni wakati mwafaka wa kuchagua nuru au kuendelea kuwa gizani

Abubakary Shacou

JF-Expert Member
Aug 31, 2014
392
305
Huu ni uchaguzi wa kimkakati sana kwa kila mpiga kura!

Ni either uchaguwe haki au dhuluma!

Au uchague mtetezi wa kweli wa wanyonge ama uchague mzalishaji wa wanyonge, shida na mataabiko ya watu.

Wapiga kura tumepewa mtihani mkubwa na mwepesi mbele za Muumba wetu. Kabla ya kupiga kura yako tafakali maumivu ya jamii nzima na kisha amua kwa haki na siyo usikilize tumbo lako tu.

Mungu alishamaliza kazi yake ya kumukomboa mkombozi wa Watanzania, pale alipomunusuru na kifo baada ya kumiminiwa utitiri wa risasi Mh. Lissu. Mungu aliona ni vema watu wake awaachie mtetezi wao wa kweli na wao watetewa ibaki kazi moja tu ya kumthibitisha kuwa kweli yeye ni mtu wa haki. Hatuna haja ya kuletewa au kuoneshwa muujiza zaidi ya huu wa Lisu kuwa hai na kuibukia kusaka ukombozi wa nchi.

Kama tukiamua kinyume na mapenzi ya Mungu tumeisha na tutaangamia kwa ujinga na kukoswa maarifa kidogo ya kutambua mapenzi ya Mungu juu ya taifa lake.

Tusikubali kuchaguwa utapeli wa ndege, madaraja na viwanja vya ndege tusivyojuwa mahesabu yake na ninani kahakiki husahihi wa pesa na thamani halisi ya ya miradi hii! Lakini pia miradi hii inawezekana isiwe kipaumbele kwa Watanzania tulio wengi.
 
Mwaka tuliokuwa tukiusubiri umewadia, mwezi na siku tuliokuwa tunazisubiri zimejongea. Siku ya kuamua hatma yetu watanzania tuendelee na dhiki, unyonge, umasikini unaoendelea kuota mizizi, haki za raia zikikanyagwa, uhuru wa vyombo vya habari vikiendelea kusiginwa, watu wakiendelea kupotea na wengine kuokotwa kwenye viroba kwenye fukwe za bahari, wazazi na wanawake wakiendelea kudharilishwa na wenye hoja za mabadiriko nchini wakiendelea kukamatwa na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha AU mabadiriko ya kimfumo, usawa kwa wote, utawala wa haki na sheria, malipo kwa walionyanyaswa; kubomolewa nyumba zao bila stahiki zao, wastaafu pension zao, maendeleo ya uwiano kati ya vitu na watu KWA MIAKA MITANO IJAYO.

Watanzania wenzangu siku hiyo tupige kura kwakuangalia umoja wetu na si matumbo yetu. Wewe waweza usiwe unateseka lakini mama ako, shangazi zako, dada zako na kaka zako wanateseka kwa mfumo dharimu uliokuwepo. Ni muda muafaka wa kuyapata maendeleo ya kweli, kugawana keki ya taifa kwa pamoja na si kikundi flani.
 
Back
Top Bottom