Watanzania ni Wakarimu, Nitarudi Tena ' - Busta Rhymes | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ni Wakarimu, Nitarudi Tena ' - Busta Rhymes

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Nov 24, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Busta Rhymes akichengua wabongo kwenye Fiesta Tuesday, November 24, 2009 8:00 AM
  MSANII mkongwe wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes amesema kuwa ameridhishwa na ukarimu wa Watanzania hali inayomfanya afikirie kuitangaza Tanzania kwa wasanii wenzake wa nje kuja nchini. MSANII mkongwe wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes amesema kuwa ameridhishwa na ukarimu wa Watanzania hali inayomfanya afikirie kuitangaza Tanzania kwa wasanii wenzake wa nje kuja nchini.

  Busta Rhymes alikuwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mwaliko wa kuwa moja ya wasanii wa kutumbuiza katika tamasha la Fiesta la mwaka huu lililofanyika jumamosi katika viwanja vya Chuo cha Posta.

  Mara baada ya kupanda jukwaani na kutakiwa azungumze kidogo, Mwanahip hop huyo maarufu duniani alisema "Sikutegemea kuwa Watanzania wanapenda muziki, ni wakarimu, na hii inanifanya niwakumbuke zaidi na zaidi nikirejea Marekani".

  Alisema, atafanya kila analoliweza kuitangaza Tanzania kimuziki, na hata kuwavutia wanamuziki wenzake wakubwa, wakiwemo 50 Cent na Jay Z kuja kwa ajili ya onyesho, ikiwezekana katika onyesho lijalo la Fiesta.

  Licha ya msanii huyo kuchelewa kupanda jukwaani, aliweza kutumbuiza zaidi ya saa moja huku akiwa na wasaidizi wake na kuufanya umati uliofika hapo kumshangilia kwa nguvu.

  Busta alishangiliwa zaidi pale alipoimba vibao vyake ambavyo vimezoeleka katika masikio ya wapenda muziki kama `Make it Clap` na `Arab money'.

  Mbali na nyota huyo kutoka Marekani, onyesho hilo pia lilipambwa na wasanii mbalimbali wa hapa nchini.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3606326&&Cat=8
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  He..this is a NEWS to me!
  Watanzania ni Wakarimu, not because he got all his due in full?
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,348
  Likes Received: 22,196
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kusikia mtu kaenda ugenini kisha akasema hapa ni pabaya sana na nyie ni wakatili kabisa sirudi ng'oooo
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nenda Somalia au Afghanistan ndio utajua kama upasifie wakarimu au la.
   
 6. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  wee mwanangu usimshauri mtu hivyo atafariki bure....

  Ila mwisho wa siku kweli bado waTZ ni wakarimu sana...Nchi nyingine hata

  kumpa hi mtu barabarani ni isue, hata kuongea na mtu kwenye daladala sio

  kawaida yani mnaanza safari mpaka mwisho kama mabubu, hata kitendo

  cha kusimama kwenye daladala ili kumpisha mtu mzima anapoingia ni nadra

  sana kutokea nchi nyingine, hata kitendo cha watu kuudhuria msiba na

  kufil kama sehemu ya yale matatizo

  watusaidie waliotembea nchi nyingi.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli huwezi kwenda mahali ukasema eti nyie wabaya na sirudi tena hiyo ni fact, ingawa moyoni anajua ukweli! Nadhani dada zetu walimkarimu pia....nakumbuka Etoo, alitamani kutorudi Barcelona!
   
 8. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hiyooo!!
   
 9. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii,lakini niliwahi sikia kuwa kuna kipindi ze late Wacko Jacko alikuja bongo na kudai kuwa eti bongo kunastink,ikamlead kutembea na mask mpaka mwisho wa dhiara yake!!
   
 10. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Salam.

  Watanzania ni wakarimu kwa wageni, mgeni akija unampa vilivyo bora, wenyeji mnabakia kula, au kulala kwenye sehemu zisizo bora, mtamchinja kuku hata kama ndiye aliyebakia kuwa wa mbegu. Pia hatuna tabia ya kuwaeleza wageni wanaotuudhi kuwa wametuudhi. Niliwahi kuwa na urafiki na wanaafrika mashariki wengine, walikuwa wanadhani kuwa Watanzania ni wanafiki kwa kuwa tunavumilia sana kuudhiwa na watu wengine.

  Kwa maoni yangu huu ''ukarimu'' umetusababishia kutawaliwa na wakoloni wa zamani na hata wa mamboleo. How can you explain a chinese Konda? ( mgonga debe kwenye daladala) We do not have the guts to say he he he do not do the kind of jobs that can be done by our youth. If you are a foreigner please do the jobs that we are not yet able to do like the technical stuff.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa milele ntamkumbuka na huu wimbo wake hapa chini. Umekaa ki-ajabu sana ila ndiyo ulimfanya ATESE dunia nzima na kuwa anafahamika. Pia ni moja ya watu walioanza kutumia Video Camera with FISH-EYE LENS.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=AiVpSSkwPU4&feature=related[/ame]
   
 12. B

  Babuji Senior Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo mzee umenena pointi
   
 13. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Akienda kenya atasema hivyo hivyo , akienda Uganda atasema hivyo hivyo kote akienda atasema Nchi nzuri , wakarimu na wanawake wao wazuri .
  Sehemu yeyote ukiwa mgeni unakarimiwa bwana . Nakumbuka mara ya kwanza nafika USA , kila jirani kwenye neighborhood yetu alikuja kutukaribisha kwa kutuletea matunda na mazagazaga kibao nikasema kumbe wazungu ni wakarimu .Ngoja huyu Busta ange haribikiwa gari mtaani halafu aone wabongo wangemsachi kinamna gani .

  Michael Jackson hakusema kua Bongo inanuka, ila alivaa ile surgical mask ambayo ilifanya watu wadhani kua anaona harufu mbaya .

  Kiukweli ni kwamba Kulikua kunanuka shombo ya samaki kutoka ferry maana ilikua maeneo ya Kilimanjaro hotel , Kama una bisha hakunukio nenda Kempinsky level 8 toka kwa nje pale halafu sikilizia hiyo shombo.

  Halafu hawa clouds mbona sijaona nani kashinda gari? au ilikua longo longongo?
   
 14. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Ni una Naive tulionao kwa watu wa mataifa ya nje ukichangiwa na umasikini hakuna jengine .

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=lPT_3PEjnsE[/ame]
   
 15. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi olalalalalala
  Ila ni ahah haha haha haha aha aha aha ah
  Aisee wapunguze
   
 16. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Wengine husema kwa matendo, kama yule aliyeshika pua yake mara baada ya kutua JK N international airport
   
 17. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hana lolote ameshakuwa played out anafurahia mshiko aliolipwa.
   
 18. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu hayo mapokezi ya shangwe na vigeregere ni Marekani hii hii au South America? State gani hiyo na wengine waende japo kutembea!
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  huyu kaonjeshwa milupo ya CORNER BAR anatoa ukarimu kwa watanzania wote tungempeleka GARDEN BISTOL Si angeomba na uraia kabisa..ngozi za bongo noma
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Labda woooooote mliopinga hapo juu mlitaka labda mchizi asemeje? Sisi kwa kukosoa hata angesema chochote tungelalamika tu, nafikiri duniani sisi ndio tunaongoza kwa kulalamika.
   
Loading...