Watanzania ni lazima waambiwe na wajue, hakuna tusichokuwa nacho ili kuiletea nchi yetu maendeleo

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,037
2,000
Watu wa kwanza wanaotakiwa kulifahamu hili ni viongozi wetu, na wao ndio wawe mstari wa mbele kuhimiza kila mtu ajibidishe kujiletea maendeleo na kwa kufanya hivyo kuipatia nchi yetu maendeeo inayoyatafuta.

Hii ndio kazi ya kwanza muhimu kwa viongozi wetu.

Hatutegemei wawe watu wa kuzunguka dunia wakilialia kwa niaba yetu kutafuta watu wengine waje hapa kutuletea maendeleo.

Kusema hivyo haina maana hatutaki mashirikiano na watu wengine, au hatutaki wawekezaji waje hapa kuunga juhudi zetu, kwa maelewano nasi za kuiendeleza Tanzania.

Hawa wanapokuja hapa, hawaji kwa hisani, wanakuja kwa sababu wanaona kuna fursa kwao pia; hawaji hapa kutoa sadaka.

Tutawawekea mazingira ya kufanya kazi zao, lakini isiwe ni mazingira yanayofifisha juhudi zetu za kujiendeleza.

Wananchi wetu wanahitaji tu uongozi mzuri utakaosimamia juhudi tunazofanya ili zilete tija kwetu. Wasimamie vyema mipango yetu ya maendeleo na kuhakikisha kwamba tunafikia malengo tunayojiwekea katika muda maalum.

Mali asili tulizo nazo, hata kama hatuna uwezo wa kuzivuna sasa ili zichangie kwenye maendeleo yetu, zisifanywe kuwa ndizo sadaka za kuwapa/kuwavutia wanaopenda kuja hapa kuzivuna. Ni lazima zitufaidishe, na wao wakipata faida ya uwekezaji wao.

Kwa hiyo, tuwakumbushe hawa viongozi waliopo sasa, kuvutia uwekezaji, hasa wa ndani ni muhimu zaidi, lakini hata tunalazimika kuwavuta wa nje, lengo letu liwe ni moja tu, manufaa ya nchi yetu na wananchi wake.

Kamwe, haitatusaidia chochote kudhani kwamba uwekezaji wa holela kutoka kwa yeyote toka nje ndio utakaotuwezesha kupata maendeleo ya haraka kwa nchi yetu.
 

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,022
2,000
Mfano wa uongozi bora ni Speaker kukanyaga katiba na kujimwafay kuwa hawezi kushtakiwa popote pale.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,800
2,000
1. Watu wamekuwa wakifanya kazi na kujibidishaa tangu uhuru. Bahati mbaya sana maendeleo hayaji kwa kufanya kazi kama punda kitu ambacho jiwe alifanikiwa sana kuwaaminisha wafuasi wake katik kipindi chake.

Maendeleo yangekuwa yanakuja kwa kufanya kazi kama punda katika hii miaka ungewaona wasukuma mikokoteni, makuli, wamachinga, mama ntilie, bodaboda, watembeza ukwaju/maji, wakulima wengi, n.k wakiwa wameondokana na umaskini.

2. Wawekezaji wa ndani unaowazungumzia ni wapi? Bakhresa, MO, Sayona, Manji, Rostam? Kama ni hao, wengi wao wanataka kuuza juice, ice cream, tambi, bodaboda, mchele, mafuta.

Tunzania inahitaji wawekezaji wakubwa kabisa aina ya Dangote katika kila sekta ili ijitoe mikononi mwa makucha ya umaskini.Wawekezaji wa haina hii ndio watakaotoa ajira na kodi za maana na kuleta tija kwa rasilimali tulizo nazo.

Huu wimbo wa kuendelea kukalia rasilimali unaoimbwa tangu enzi za Nyerere kusubiri watoto wetu waje kupata ujuzi wa kuzivuna umepitwa na wakati. 60 damn years!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom