Watanzania ni lazima tufikirie kwanza jinsi ya kutatua matatizo kabla ya kusingizia pesa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Watanzania tumekuwa watu wa kulalamikia pesa kila siku lakini ukweli ni kwamba pesa hatuna na ni wakati wa kufikiria pesa ifanye nini kwa jamii na iende wapi. Mfano nilimsikia Zitto akisema walimu wapandishie mishahara lakini hakueleza pesa itataka wapi! vilevile tutataka madaktari waongezewe mishahara lakini hatusemi pesa itatoka wapi?

Polisi na jeshi nao watataka kuongezewa mishahara na makundi mengine yanayotegemea serikali. Sisi Watanzania tuna wajibu wa kuja na jinsi ya kuweza kukuza uchumi ili kuongeza kipato na vilevile kupunguza shughuli na vitu serikali inavyofanya ili serikali iweze kuongeza mishahara na kushughulikia shughuli muhimu tu za jamii.

Hatuwezi kutaka serikali iendelee kujihusisha na vitu vya biashara na kupoteza pesa halafu tutegemee wafanya kazi wa serikali wawe na mishahara na mafao zaidi. Mfano serikali ingeweza kujitoa kwenye Tanesco, ATC, TRC n.k ambavyo vinachukua pesa za serikali nyingi bila kuongeza unafuu, kazi au ufanisi wa mashirika haya kwa jamii. Kwahiyo walimu wakitaka kuongezewa pesa ukweli ni kwamba pesa ya serikali imeenda Tanesco na ATC! huwezi kupata vyote.

Kwahiyo badala ya kulalamikia rushwa pekee ni lazima Watanzania tukubaliane kwamba serikali imejihusisha kwenye vitu vingi sana ambavyo si vya lazima kwa serikali kufanya na hatuwezi kuongeza ukubwa wa serikali na kuongeza mafao wakati huohuo.Matatizo ya Tanzania hayataweza kutatuliwa na serikali pekee bali serikali inatakiwa kuweka mazingira tu na Watanzania wenyewe watatatua matatizo yao.

Huwezi kufanikiwa kwenye mfumo huu wa sasa wa kibepari kwa kuwa na serikali kubwa kwani serikali kubwa inaleta rushwa, inadumisha ufanisi na vilevile haileti ugunduzi.

Swali langu.
1. Je Tanzania ifanye nini kuongeza kiwango cha elimu na kuongeza mafao ya walimu bila kuongeza Budget ya elimu?
2. Tanzania ifanye nini kuboresha sekta ya Afya na kuongeza mafao ya madaktari bila kuongeza budget?
3. Je Tanzania itaweza vitu kuongeza ufanisi wa Bank kwenye uchumi wetu wa Tanzania?

Tutaongeza maswali topic inavyoenda.
 
Kuongeza mishahara si suluhisho lazima tujiulize kwanini mishahara haitoshi.Wachumi wanadai kwa sababu ya mfumuko wa bei.Swali nini kinasababisha mfumkowa wa bei majibu ya haraka haraka ni bei ya mafuta na chakula?

Serikali inatakiwa kuhakikisha mafuta yanauzwa kwa bei nafuu kwa kufufua kiwanda cha TIPPER ili kiweze kusafisha mafuta kwani mafuta ghafi ni bei nafuu na ni pia tukisafisha tutafaidika na kupata mafuta ya taa lami na bidhaa nyinginezo.Kurudisha maghala ya chakula yaliyouzwa kujenga mengine na serikali kuwa mnunuzi mkuu wa chakula.

Serikali haipaswi kuwaachia wafanyabiashara binafsi kazi ya kununua chakula kwani wafanyabiashara hao wananunua kwa wingi wakati wa mavuno tena kwa bei ya kutupa halafu wanahifadhi chakula ili wakiuze kwa bei wanayotaka pale kunapokuwa na uhaba wa chakula serikali ikiwa mnunuzi mkuu ihahakikishe wakati wa kukiuza kinauzwa sokoni kwa bei nzuri ambayo wananchi wengi wataimudu.Serikali iwekeze kwenye shirika la reli hii itafanya bidhaa zisafirishwe kwa bei nafuu.

Jambo jingine kama serikali haina pesa iwe kwa kada zote kwani sasa kada kama za siasa yaani wabunge wamekuwa wakilipwa mshahara mnono na bado wamekuwa wakiongezewa kwa kiasi kikubwa lakini tunaona kada nyingine zikiomba kuongezewa pesa tunaambiwa hamna pesa.

Kuongeza mikoa na wilaya kumeongeza gharama kubwa kwa serikali.Kushindwa kusimamia rasilimali leo ndio tunafikiria tuanze kuhifadhi dhahabu zetu wakati hicho kitu tulipaswa kufanya muda mrefu hayo ni baadhi ya mambo machache tunayoweza kufanya lakini yapo mengi kwa nchii hii
 
Mimi nafahamu uchumi sana! Naona bado hamjajua kinachopelekea watu kudai mishahara. Mfumo wa mishahara na posho uliopo Tanzania ndio unaofanya watu wadai mishahara.
Mshahara wa mhitimu ngazi ya CHETI ya mifugo ni takribani sawa na wa mhitimu wa SHAHADA ya ualimu.
Je hizo hela za kuwalipa hao wengine zinatoka wapi?
TUFIKIRI CHANZO KWANZA, KISHA TUTAPATA SULUHU YA KUDUMU.
 
Back
Top Bottom