Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? | Page 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 19, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa inawezekana kabisa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe na watupu!, uwezo wa kufikiri kwa kina (deep thinking) hatuna!. Uwezo wa kufikiri kwa tafakuri, ("logical thinking"), ni mdogo!, wengi wetu ni sifuri kabisa, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe, au tufanywa mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunadanganyika kwa viahadi vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo. Badala ya kudeal na issue zenyewe ambazo ndicho chanzo, kilichopelekea haya yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi! Tunahangaika na matokeo.

  Hii ignorance ya Watanzania ina cut across section ya society yetu yote na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya bunge letu, serikali yetu na ndani ya cabinet yetu!, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ma ignorants ajabu ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma zenye dhamana kubwa na maisha ya Mtanzania ambao ni ma ignorants ajabu!, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ikiemo mihimili ambao pia ni ma ignotants, na wana jf wengi tuu pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, ninayeandika hapa, Paskali pia ni ignorant tuu!, ila tofauti yangu na wengi wa maignorants wenzetu, wao wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu, tunaionyesha hiyo ignorance yetu wazi wazi kwa ku speak out and expressing our minds, tatizo, ni, in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!. Sorry for this.

  Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura za ushindi, mwaka hadi mwaka, na October 25 tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.

  Hisia za kujiuliza, kama sisi ni ma ignorants au tumelogwa, ni kufuatia kuwa na mtazamo, ya kuwa haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu ajabu kama haya tunayofanyia na CCM lakini bado sisi wale wale tunaichagua tena CCM na kuichagua tena na tena!, na October 25, tutaichagua tena!.

  Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 54 baada ya uhuru, sio tuu, wale maadui wakuu watatu bado wapo, bali ujinga umeongezeka mara dufu, umasikini sasa ni uliotopea, kila siku ni afadhali ya jana!, na maradhi hadi mengine ni janga, vimeongezeka afadhali ya zamani na enzi za mkoloni, bali pia, tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, Escrow etc, etc.

  Tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulidharau capital kwa kudai "pesa sii msingi bali pesa ni matokeo!".

  Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

  Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa October 25, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

  Namalizia kwa kukumbushia hili swali, are we really this ignorant?!, kwa kuchagua tuu ili mradi ni kuchagua, or this time, around tutaonyesha tumeerevuka angalau kidogo, hivyo tutachagua kwa sababu ya kuchagua, yaani kufanya informed decision?!, na sio kujichagulia tuu alimradi tumechagua!.

  Nawatakia Jumamosi Njema.

  Paskali

   
 2. S

  Sombeti JF-Expert Member

  #141
  Sep 21, 2015
  Joined: Jun 20, 2015
  Messages: 804
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Pasco :bange: Umeandikaweeeeeee huu muda si bora ungelala ??? fyuuuu
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #142
  Oct 18, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  With just 7 days to come, hakuna kipya cha kuwaambia wanabodi, bali ni kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, nini kinafanyika sasa, na nini kitafanyika hizo siku 7 zijazo, yaani tarehe 25 October, lets not let CCM to fool all the people all the times!.

  Kiukweli kabisa, sioni jinsi yoyote ya CCM kushinda tena!, Chadema inakwenda kuchukua nchi kiulaini kabisa kama imeokota!, yaani CCM inakwenda kuanguka chini kiulani kabisa kama kumsukuma mlevi!.

  Lakini ili hili litimie, ni lazima kila aliyejiandikisha, ajitokeze hiyo tarehe 25, aende kupiga kura na kumchagua Edward Lowassa!, unless it is very true that we are not only ignorants!, but rather stupids!, but are we real this
  ignorants?!.

  If "Together wa can!", and "United we Stand", against this ignorance, then, "Victory is ascertain!"

  Nawatakia Jumapili njema!.

  Pasco   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #143
  Oct 23, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  With just two days to go, there is nothing new to say, yote yameishasemwa, sasa imebaki kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, uchaguzi ndio keshokutwa Jumapili, nini kitafanyika siku hiyo, na baada ya hapo, tukutane tena wiki ijayo, au tupongezane, au tupeane pole!.

  Nchi hii inaweza tuu kubadilishwa kwa watu wenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu, na kusimama wahesabiwe!.

  I'm very proud kuwa ni mmoja wa wapiga kura hiyo Jumapili.

  Haya shime kwa wote waliojiandikisha, tujitokeze kwa wingi, tuitumie haki yetu ya kidemokrasia kujichagulia viongozi wetu,

  We have to choose our leaders and love our choices and live with or without!.

  Pasco
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #144
  Oct 27, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.
  We are real ignorants na tumelogwa vibaya!.
  Pasco
   
 6. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #145
  Oct 27, 2015
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,323
  Likes Received: 1,488
  Trophy Points: 280
  Viva ACT, Zitto for Presidency 2020.
   
 7. m

  mr.robot Member

  #146
  Oct 27, 2015
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkapa hakukosea kutuita malofa, sasa baada ya uchaguz mwendo ni kukaza, mtu asije nililia shida zakeee
   
 8. Dereva wa Kirikuu

  Dereva wa Kirikuu JF-Expert Member

  #147
  Oct 27, 2015
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 401
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 60
  Mkuu Pasco..
  Maneno yako ni ukweli mtupu Tanzania ni maskini na tutaendelea kua maskini sababu wananchi wake wanaupenda sana umaskini..
  Ndomana maskini hufa maskini..

  tumelogwa..
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #148
  Oct 29, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Hili swali bado valid, kiukweli sisi Watanzania ni ma ignorants mpaka basi!.

  Pasco
   
 10. S

  Singo JF-Expert Member

  #149
  Oct 29, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Watanzania wamefanya maamuzi sahihi,NEC imepuuza matakwa ya wananchi. kwa hiyo si sahihi kuendelea kuwaita watanzania ignorants kisa NEC imelazimisha kumtangaza asiye ndiye ndiye asiye
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #150
  Mar 22, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Kama walivyofanya Watanzania Bara, na Watanzania-Zanzibar, au Wazanzibari nao wameamua kwa kauli moja kuirudisha CCM.

  Hongereni Wanzanzibari, tumeushuhudia uchaguzi, ulikuwa huru na wa haki, utulivu na amani,

  Sasa uchaguzi umekwisha, tusonge mbele!.

  Pasco
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #151
  Apr 13, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Nimeikuta hli mahli humu jf, nikaguswa nimeomba kulitumia bandiko hili kuboresha bandiko langu hili.

  Pasco
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #152
  Sep 5, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Anachofanya rais Magufuli ni kuutumia udikiteta kuondoa ujinga na umasikini!, tumuunge mkono!.

  Pasco
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #153
  Nov 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Ushindi wa CCM kwenye udiwani, umenifanya nitafakari haya mabandiko kuhusu CCM, jinsi sasa inavyopendwa na watu na kuchaguliwa kwa kishindo!.

  Paskali
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #154
  Jan 18, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Mkuu pili pili kichaa, bandiko lako linasadifu hapa, sisi ndio tunaowachagua hawa ma ignorants kwa sababu wengi wetu ni ma ignorants.

  P
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #155
  Feb 13, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Nafanya tuu rejea hoja za bandiko hili na uchaguzi wa marudio wa majimbo ya Kinondoni na Siha ni Jumamosi hii. Sitashangaa kama majimbo yote mawili, CCM itashinda kwa kishindo!.
  Hivi ndivyo Watanzania tulivyo.
  P.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...