Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? | Page 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 19, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,758
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa inawezekana kabisa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe na watupu!, uwezo wa kufikiri kwa kina (deep thinking) hatuna!. Uwezo wa kufikiri kwa tafakuri, ("logical thinking"), ni mdogo!, wengi wetu ni sifuri kabisa, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe, au tufanywa mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunadanganyika kwa viahadi vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo. Badala ya kudeal na issue zenyewe ambazo ndicho chanzo, kilichopelekea haya yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi! Tunahangaika na matokeo.

  Hii ignorance ya Watanzania ina cut across section ya society yetu yote na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya bunge letu, serikali yetu na ndani ya cabinet yetu!, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ma ignorants ajabu ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma zenye dhamana kubwa na maisha ya Mtanzania ambao ni ma ignorants ajabu!, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ikiemo mihimili ambao pia ni ma ignotants, na wana jf wengi tuu pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, ninayeandika hapa, Paskali pia ni ignorant tuu!, ila tofauti yangu na wengi wa maignorants wenzetu, wao wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu, tunaionyesha hiyo ignorance yetu wazi wazi kwa ku speak out and expressing our minds, tatizo, ni, in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!. Sorry for this.

  Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura za ushindi, mwaka hadi mwaka, na October 25 tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.

  Hisia za kujiuliza, kama sisi ni ma ignorants au tumelogwa, ni kufuatia kuwa na mtazamo, ya kuwa haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu ajabu kama haya tunayofanyia na CCM lakini bado sisi wale wale tunaichagua tena CCM na kuichagua tena na tena!, na October 25, tutaichagua tena!.

  Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 54 baada ya uhuru, sio tuu, wale maadui wakuu watatu bado wapo, bali ujinga umeongezeka mara dufu, umasikini sasa ni uliotopea, kila siku ni afadhali ya jana!, na maradhi hadi mengine ni janga, vimeongezeka afadhali ya zamani na enzi za mkoloni, bali pia, tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, Escrow etc, etc.

  Tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulidharau capital kwa kudai "pesa sii msingi bali pesa ni matokeo!".

  Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

  Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa October 25, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

  Namalizia kwa kukumbushia hili swali, are we really this ignorant?!, kwa kuchagua tuu ili mradi ni kuchagua, or this time, around tutaonyesha tumeerevuka angalau kidogo, hivyo tutachagua kwa sababu ya kuchagua, yaani kufanya informed decision?!, na sio kujichagulia tuu alimradi tumechagua!.

  Nawatakia Jumamosi Njema.

  Paskali

   
 2. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #121
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,599
  Likes Received: 5,488
  Trophy Points: 280
  CCM out....!!!
  😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨😨  CCM out... !!!
   
 3. georgemwaipungu

  georgemwaipungu JF-Expert Member

  #122
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 2,779
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Nachelea kusema akili hii ni sawa na kinyesi.
  Maana hoja ya kukichagua ccm hapa sijaiona mpaka mwisho wa habari yake.
  Chagua Mabadiliko ya kweli
  Chagua Lowasa
   
 4. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #123
  Sep 19, 2015
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,935
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  Pasco
  Inaelekea unakata tamaa na UKAWA, baada ya kuwa informed juu ya hali ya ndani ya umoja huo.
  Funguka zaidi boss!

  Kuhusu watu kuichagua ccm, huo ni ugonjwa sugu. Mimi nawafahamu watu wengi tu wana maisha duni kweli kweli. Wananing'inia kwenye dala dala kila siku; hawana mlo unaoeleweka kwa siku. Lakini ni ccm damu. Ukiwauliza unaridhika na maisha uliyonayo? Wanajibu ndiyo. Yaani kwao mgao wa umeme sio issue; kutumia maji yasiyo safi na salama sio issue. Na hawa ni wengi, mijini na vijijini.

  Hawajitambui. Ndio mtaji wa ccm.
   
 5. A

  Abel Ndundulu JF-Expert Member

  #124
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 754
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bukoba imetapika leo viwanja vya "Lowassa" hapa,ha ha ha mabadiliko ni lazima!
   
 6. georgemwaipungu

  georgemwaipungu JF-Expert Member

  #125
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 2,779
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Siwezi na sitaweza kukata tamaa leo, kesho wala maisha mimi ni Chadema tena ukawa kweli kweli.
  Na tuna uhakika wa kuchukua Nchi
  Mwaka huu siwezi kutoka huku nikiwa Ulaya nilikuwa mwana Mageuzi siwezi kugeuka.
   
 7. salimkabora

  salimkabora JF-Expert Member

  #126
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 10, 2012
  Messages: 2,465
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Watanzania ni samaki wanavuliwa kwa nyavu zilezile na ndoano zilezile miaka nenda rudi wala hawasituki
   
 8. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #127
  Sep 19, 2015
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Wewe ni mwongo. Hujawachoka na wala hutarajii kuwachoka. Kuwa mwungwana, sema JAPO MMETUCHOKA. Acha kujivika kilemba cha ukoka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #128
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,178
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 160
  Watanzania wakiweka ushabiki pembeni basi Dkt. Magufuli ndie wa kupokea kijiti cha uraisi kutoka kw Dkt JMK.
   
 10. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #129
  Sep 19, 2015
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  lowasa sio mwizi. Hajawahi kuiba chochote. Naona umeridhika na wsifu wa makomeo.
   
 11. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #130
  Sep 19, 2015
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  CCM ndio hawaaminiki kwa ajili ya kila aina ya ufisadi waliowafanyia Watanzania kwa miongo hii mitano.
   
 12. u

  utali JF-Expert Member

  #131
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 323
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli tutaendelea kuwa "ignorants" na mazuzu Kama mleta uzi alivyoandika.
  Hivi lakini tunajiuliza ni mabadiliko gani hasa sisi waTz tunayataka?? Je ni nini hasa tatizo/kiini cha matatizo yetu? Hivi ni chama/mfumo ndivyo vyenye matatizo au nini hasa?
  Tuna haja ya kukaa chini na kujiuliza maswali ambayo kwayo ndio sababu kuu ya sisi kuendelea kuwa hivi tulivyo. Lakini vile vile tujiulize uhalisia ni upi katika hili tunalolilia wakati wote,
  Mawazo yangu:
  1. Ni lazima fikra zetu zibadilike sana
  2. Tujitambue, mitizamo iwe chanya
  3. Uwajibikaji, maadili na kuipenda nchi yetu vitutawale.
   
 13. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #132
  Sep 19, 2015
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,957
  Likes Received: 1,403
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco kula TANO. Umeongea maneno mazima sana na umechambua kwa kina nini tunatakiwa kufanya, tumeanguka wapi na ni kwanini. Haya uliyosema tutayapinga kwa sababu bado hatujielewi. Tutayapinga kwa sababu tumekaririshwa fikra fulani mfu vichwani mwetu. Hatutayakubali kwa sababu yamesemwa na Pasco ambae si mwenzetu!!! HAPO NDIPO AKILI ZETU ZILIPOKOMA.

  HAKIKA WEWE NI MTANZANIA WA KWELI KULIKO WENGI TUNAOJIITA WATANZANIA HUKU NGUO YENYE KIRAKA TUKIITA MPYA!!! TUKIFUATA FIKRA MFU HUKU TUNAZISIFIA...

  AH POLE TANZANIA.
   
 14. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #133
  Sep 19, 2015
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,891
  Likes Received: 24,284
  Trophy Points: 280
  Absolutely.....
  Miss you my dear,nafurahi kukuona tena.
   
 15. Diva Beyonce

  Diva Beyonce JF-Expert Member

  #134
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 12,953
  Likes Received: 6,064
  Trophy Points: 280
  Am glad to see you ulipotea bibie nikawaza sijui umepatwa na nini, kwahyo kukuona nikajua umerudi
   
 16. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #135
  Sep 20, 2015
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,891
  Likes Received: 24,284
  Trophy Points: 280
  Mimi sio mjinga,nitadhihiridha hilo hapo October 25 nitakapoenda kuipigia kura Chadema.
  Serikali ya CCM inayayomaliza muda wake sikuwahi kuhusika kivyovyote kuiweka madarakani....nina maana ya kwamba huu ndio uchaguzi wangu wa kwanza na ninakwenda kushiriki kuiondoa CCM madarakani,raha sana.
   
 17. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #136
  Sep 20, 2015
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,891
  Likes Received: 24,284
  Trophy Points: 280
  Nakuambia acha tu,kikubwa uzima mumy....tuendelee na safari yetu ya mabadiliko maana naona imepamba moto sio mchezo!
   
 18. Diva Beyonce

  Diva Beyonce JF-Expert Member

  #137
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 12,953
  Likes Received: 6,064
  Trophy Points: 280
  Yani uzima ni kila kitu mpaka October ifike napenda changes balaa kupiga kura kwa Mara ya kwanza nataka iwe na positive impact ya changes.
   
 19. m

  makuhaba JF-Expert Member

  #138
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 231
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko tuu a
   
 20. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #139
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 5,033
  Likes Received: 1,476
  Trophy Points: 280
  kuna swali,ulishaacha kumshabikia luwassa.
  Watanzania ni malofa na mafala COPY BEN.
   
 21. Z

  Zuphora Senior Member

  #140
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 137
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani hata mseme nini mimi ni CCM tu kwani siwezi kuweka nchi rehani kwa watu ambao wamekosa dira wala muelekeo.Chama kisichoaminika na kubadilikabadilika kama Kinyonga kwakweli pamoja na madhaifu yooooote ya CCM sijaona nani wa kumuamini. Kumchukua Lowassa na kutugeuka watu tuliowaamini ni usaliti ambao upinzani umefanya wanakosa uwezo wa kuinyooshea ccm vidole
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...