Watanzania ndiyo wadhaifu na wanafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ndiyo wadhaifu na wanafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Jun 30, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika tafakari yangu nimegundua kuwa Kikwete yeye si dhaifu ispokuwa sisi watanzania ndo tunapaswa kjilaumu kwa udhaifu na unafiki wetu Nasema hivi kwa maana hii; awamu ya kwanza ya uongozi wake tuliona kuwa kashindwa lakini baada ya uchaguzi mkuu awamu ya pili tukamchagua tena. wengi watasema alichakachua mimi nashindwa kuelewa kuwa wengi tusingempigia kura basi hata uchakachuaji ungekwam. Lakini udhaifu wetu ni pamoja na kusifia mafisadi, fisadi anaonekana shujaa kwa kumsifia, kumwalika kwenye harambee,nk. Fisadi mwenye pesa huonekana bora kuliko mzalendo wa kweli. Ni siku nane tangu madaktari kugoma watanzania tupo kimya hata kuandamana kupinga udhalimu huu wa serikali kushindwa kukaa na madaktari sisi tunalaumu tu kwa mdomo. Tunashindwa hata kuonyesha hisia zetu. Kikwete anatuenjoy sana baadaye atawaita wale rafiki zake kwa madai wazee wa daresalaam na kutukoga kulaani wanaharakati, ndipo utasikia eti watu wanaandamana kuunga hotuba ya rais UNAFIKI NA UDHAIFU!!!!! Walimu wanataka kugoma baadhi ya watu wanawasema vibaya mara vilaza licha ya umuhimu wao, kama si udhaifu na unafiki ninini? Dr. Ulimboka yupo mahututi hakuna hata kuandamana kuonyesha hisia zetu UDHAIFU MKUBWA, wanaharakati mbona kimya, wapinzani mbona kimya, spika anafanya madudu kwa kuzuia mijadala isivyo halali tunamchekea utafikiri mazuzu kwa nini tusiandamane kupinga ubabe wa yule mama Watanzania sisi ndiyo dhaifu! Kikwete yupo kimya licha ya matatizo ya madaktari sisi tupo kimya. Wanaiba mali zetu, wanatibiwa nje, wanasomesha watoto nje sie Kimya AIBU, SISI NDIYO WADHAIFU WALA SI KIKWETE TUUNGANE KUUKATAA UDHAIFU HUU NA UNAFIKI!!!!!
   
Loading...