MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,748
- 48,371
Humu JF sisi ni watani, na hata nje ya JF huwa watani wa jadi, tunaringishiana maendeleo ila kwa nia njema, pamoja na haya matani ila binafsi huwa sina kinyongo na Watanzania na wengi ni marafiki zangu, kunao hata leo nina ukaribu nao hata kuzidi ndugu zangu, yaani tunaweza kupigiana simu na kusaidiana hata hela, ila hili la UNSC limenishtua sana, sikujua inawezekana mkawa na chuki kiasi hiki, sitaki kuamini na mpaka itolewe taarifa rasmi sitaamini.
Jameni acheni kuwa serious kwamba hamkutupigia kura, yaani mataifa yote ya SADC na EAC yatupigie kura nyie mbaki na waarabu huko pekee yenu, kama hii kweli itakua aliyekwenda kupiga kura kajichanganya, sitaki kuamini Magufuli na uongozi wake wote waliidhinisha kitu kama hiki, siamini na sitaamini mpaka taarifa rasmi zitoke.
Jameni turingishiane mazuri, tupige biashara na kushindana lakini tusifike mpaka wa kuoneana wivu kiasi hiki, nitachukia sana nikizingatia kwamba nina jamaa zangu wa karibu sana huko Tanzania, hivi tulifikia kiasi hiki lini na ilianza vipi, waziri wenu bwana Kabudi tena namheshimu sana maana ni kichwaa, mwenyewe aliahidi mtatupigia kura.
Bado naomboleza kwa hili, sitaki kuamini.