Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,448
- 1,003
Katika hotuba yake miongoni mwakauli zilizozua utata katika kikao kile ni pale Rais Samia Suluhu Hassan alipowaambia viongozi hao kuwa, " Lazima kila mtu ale kwa Urefu wa kamba yake "
Kauli hii imetafsiriwa na wengi hasa wasiofahamu maana za methali za kiswahili kuwa ni sawa na Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu Mawaziri kutafuna pesa ya Umma,
Nini maana halisi ya methali hii " Kila Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake "
Kwanza, maana yake kinadharia ni kwamba Mbuzi akifungwa kamba hawezi kula zaidi ya urefu wa ile kamba mpaka kamba ikatike,
Pili, Maana ya kimantiki ni kwamba kila kitu/mtu hufanya kile kilichopo kwenye uwezo wake au ruhusa yake au Mamlaka yake tu,
RAIS SAMIA ALIMAANISHA NINI?
Rais Samia Suluhu Hassan alipotoa kauli hii alilenga kuwafunda Mawaziri na Manaibu Mawaziri wasichote pesa ya Umma hata senti moja,
Ila waridhike na wachukue kile tu wanachostahili kama Posho za Safari na marupurupu mengine yaliyoanishwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi wa Umma kwa nchi yetu,
Sikia, Kila mtu kula kwa urefu wa kamba yake sio kauli inayoruhusu " Wizi au Ufisadi " ila ni kauli inayolenga kuwarudisha watu|Viongozi kuwa na hofu ya Mungu na kutambua dhamana walizonazo ipo siku watajibu walizitumiaje kwa Mungu,
Dunia hii kila mtu ni mwizi ndio sababu pakawepo na controls|Utaratibu au kwa lugha rahisi kama aliyoitumia Rais Samia Suluhu yaani " Kamba "
" Kula tu unachostahili, kula chako tu "
#Sasa kama kuna Waziri hafahamu kiswahili fasihi aguse pesa ya Umma ndio ataelewa Rais Samia Suluhu Hassan alimaanisha nini,