Watanzania na watawala wetu: Wawekezaji aina ya ACACIA watufungue macho na tubadili dynamics zetu kwenye uwekezaji

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Juzi nilikuwa nasoma kutoka tovuti ya IKULU na kukutana na nukuu ya baba wa Taifa. Naomba ku-copy na kui-paste hapa jukwaani…

“Intellectuals have a special contribution to make to the development of our nation, and to Africa. And I am asking that their knowledge, and the greater understanding that they should possess, should be used for the benefit of the society of which we are all members."

Kwa muktadha wa alichosema Mwl. Nyerere baba wa taifa letu, kuna mengi ya kujifunza na kuchukua hatua za haraka na makusudi ili MAARIFA na UFAHAMU mkubwa wa “Intellectuals” uwe na faida kubwa kwa jamii ambayo sisi wananchi wa Tanzania na Afrika tunaishi.

Alichokisema Mwl. Nyerere, kinanipa kukumbuka nukuu ya mmoja wa wazungumzaji katika kombano la the GLOBAL LEADERSHIP SUMMIT mwaka huu aitwae, Danielle Strickland; ambae alisema “How we use power is the measure of our leadership. Great leaders, use power to empower other people”

Kwa namna gani tunatumia mamlaka yetu, ni kipimo cha uongozi wetu. Viongozi wakubwa, wanatumia mamlaka kuwajengea uwezo watu wengine.

Tanzania ili itoke hapa kiuchumi tuna wajibu wa kuja na “Marshall Plan” yetu ambayo ni inajumuisha mambo yote.

Tujikumbushe kwa muhtasari malengo Mahsusi ya Marshall Plan

  • Kuweka na mfumo wa makazi bora kwa wasio na makazi, kuhakikisha kuna chakula cha kutosha na kuondoka ukosefu wa ajira kwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi.
  • Kudhibiti mfumuko wa bei ili wenye fedha waweza kumudu gharama za bidhaa na huduma; Kuhakikisha viwanda, barabara, reli, madaraja mifumo ya umemena maji inarejeshwa (kama ambavyo jPM anafanya)
  • Wakulima “waliopigika” kutokana na ukame wanajengewa uwezo ili wawe na uhakika wa kuzalisha kwa mfumo wa umwagilaji ikiwemo kuzalisha chakula kwa wingi na gharama nafuu ili jamii imudu kununua. (Tanzania mvua zikinyesha za kutosha, uhakika wa chakula kama mahindi, mtama, mchele unakuwa very automatic… mvua ikipotea tokana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, wote tunajua nini huwa kinatukumba kama Taifa mvua ikipotea msimu mmoja tu)
  • Kuweka mfumo thabiti wa mitaji ili kuruhusu biashara na huduma zishamiri ilijulikana kama Project financing. (Tanzania hapo, tunasubiri mitaji ya wawekezaji na je kuna juhudi za makusudi kutoka hapa)
Kuna nyakati kuna faida kuwategemea wawekezaji wanaokuja na mitaji yao. Ila pia kuna changamoto iliyopo. Wengi wao huwa ni wakwepa kodi na huwa wanahamisha mitaji kurudi kwako wakipata faida tokana na uwekezaji wanaofanya, jambo ambalo sio dhanmbi.

Tuikumbuke Zimbabwe. Ilikuwa poa sana kiuchumi. Rais Mugabe “alipozinguana” na wazungu wawekezaji; haoo…wakasepa na mitaji yao. Zimbabwe ilianguka kichumi mpaka leo haijasimama. Driving force ya uchumi wao na biashara hawakuwa akina Masanja, Mayalla au Wambura,walikuwa ni wale “wakuja”.

South Africa mpaka sasa, uchumi wao mkubwa sio wa akina “Rugakingira”, “Massawe” au “Mafimbo”, wanaomiliki mfumo wa biashara ni akina “Debeers”, “Mark Fish” na watu kama hao.

Kuna maeneo mengine Tanzania yetu hii, ndugu zetu wazawa wenye asili ya “Asia” hasa India na Pakistani huwa wanawekeza. Wakipiga hela na “Balance sheet” za kampuni zikasoma vizuri, hao wanakimbilia UK na Canada. Mfano wakati huu ninapoandika makala hii, kuna kampuni moja kubwa hapa Mwanza ni ya “Wazawa”. Famila nzima ambayo ina-hold (top managemenent positions) imekwenda India, sijui kufanya nini. Na sitaki kujua, maana kila mwaka miezi kama hii huwa wanakwenda.

Tukumbuke, ndugu zetu hawa, nyakati za chaguzi mkuu wengi huwa (hasa kama tunabadili ma-rais), huwa wanafunga biashara na kwenda “kusikilizia” hali ikoje. Mambo yakitulia wanarejea. Tukumbuke 1995, 2005 na hata 2015. Hawa ni wenzetu kweli kwenye kupigana kwa njia ya uwekezaji Tanzania isogee mbele. Binafsi nina wasiwasi nao, ila niko tayari kukosolewa kama sina macho ya kuona sawasawa. Achilia mbali ni wazuri kupiga deal na wakubwa. Kumbukeni kashfa ya Zuma kuondolewa kwenye umakamu wa Rais kwa kashfa ya wizi wa hela alisababishiwa na Schabir Shaik (wa kule kule). Badae Zuma akajiweka sawa akawa Rais, (mara hii akina Gupta na haooo wakapiga nae madili) Hapa bongo, nikae kimya wenye macho ya kutazama wanajua.

Tukirejea kwenye Marshall Plan, ndani ya miaka 4 toka iwe implemented, ilitoa matokeo tarajiwa kwa zaidi ya asilimia zaidi ya 30 kwa nchi za Ulaya 17 zikiwamo Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Austria n.k. Aidha kuna wafaidika wengine kama Ugiriki na Uturuki walijijenga kiuchumi kwa msaada kama huo.

Swali la msingi kwetu, sisi kama Tanzania, je tuna mkakati wa kutafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali vikwemo vya ndani ili kukuza ujenzi wa viwanda kwa soko letu na kwengineko ili kutengeneza surplus katika balance of trade?

Kufanya kazi na “wakuja” kama “ACACIA” ambao baba yao Barrick alikiri wazi kuwa walituingiza chaka na kutuibia kwelikweli. Tutemee wao kutupaka matope, au kuna nyakati wakisimamisha uzalishaji na ikitokea ndiyo hivyo tunalia ajira kupungua. Tabu tupu.

Ushauri kwa watawala/viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Wakati tukiendelea kujenga uwezo na kuwabembeleza wakezaji waje, tuna wajibu wa kutengeneza mfuko wa uwezeshaji (project investment funding) kwa biashara za kati. Akitokea Mtanzania mwenye akili yake akopeshwe kwa msingi ya equipment finance purchase/machinery finance ili kwa yale ambayo Watanzania tunaweza tufanye biashara na kurejesha mkopo. Mzunguko wake utalipa tu. Tusiogope sana risk, kuidhibiti riski isitokee na kama ikitokea kuwa na recovery, basi tuongeze risk absorption base kwa kwa kuwa na policies za kinga kupitia kampuni zetu za bima. Tukubaliane tu, kuna haja ya wenye biashara hizi kuwa under supervision ya wataalamu kwenye kila stage kuanzia andiko la mradi, kuanzisha biashara mpaka kuikuza kwa kupanua katika line hiyohiyo au ku-deversify.

Nitoe mfano wa wazi kabisa kuonesha hela zipo. Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambao wana akili zao wanapopata udahili wa vyuo vikuu, kwa kutambua famila haina uwezo wa kulipa ada, wanakopeshwa na serikali. Juzi nimesikia taarifa ya bodi ya mikopo ya vyuo vikuu kuna billion 88 kwa mwaka huu zimetengwa wa kwanza tu. By assumption tunaweza kuwa tunawekeza zaidi ya bilioni 400 kwenye mikopo ya elimu tu. Mrejesho wa haya mabilioni uko subject getting jobs au establishing a business which can ensure the pay back. Bado kuna wanafunzi wengine wanakuwa “discontinued” so hela zinapotea, kuna wengine wanakufa hela hizo hela nazo zinapotea na kuna wengine wanachelewa kupata kazi, hivyo kupelekea urejeshaji nao unakawia.

Tukijenga vizuri “Small and Medium Industrial funding basket”, urejeshaji wake ukiwa kwa say asilimia 70, maana yake mzunguko wake utakuwa promising kwa lengo la kupanua biashara pia kwa hao wanaliokopa kwanza na kurejesha ili na wengine wakope, hii itakuza mzunguko. Tutaongeza mzunguko wa fedha, spending capacity ya biashara kwa kununua bidhaa na huduma, kodi itapatikana kwa wingi kwa kuwa miamala inafanyika kwa wingi kuliko sasa. Mifuko ya Pesheni itaongeza wanachama na tukiwa na hala kwanini tusipande “bombardier ya Dreamliner” mara moja moja. Tunavisapoti vya kwetu kwa kuwa sehemu ya Wateja.

Ni uzalendo wa hali ya juu serikali kuwa-support intellectuals ambao ni wazawa ili ukuaji wa uchumi katika sekta binafsi (biashara na hudumu) ushikiliwe kwa nguvu na akina Misoji Enterprises, Manka Ltd, Kabula Investment, Wegesa Group Ltd au Nyangeta General Merchandise.

Wapo Watanzania ukiambia haya wanasema sisi hayo ya kuwekeza kwenye biashara na viwanda hatuwezi. Mimi huwa nawaza tofauti kwa swali, kama hatuwezi; Mbona vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama (JWTZ, Polisi, Magereza, Umahiaji, PCCB, Unti-Drug Abuse na TISS) hawategemei “wawekezaji wakuja” ambao ni ngozi nyeupe iwe toka Ulaya au Asia?. Kama ni uwezo, maarifa na ujuzi hata katika biashara, Watanzania wataingia kama “recruit” na wanapanda kimaarifa, kiufahamu na uzoefu huku wakikua mpaka wana-head directorates?

Tunaweza kuwekeza kama tutaamua kuwajengea watu wetu uwezo (training, skills development, enhancement and adoption of right technology), kuwa-supervse na kuwa-mentor ili wakue kwa kutoa matokeo tunayotaka.

Ili mbegu bora na sio bora mbegu ya uwekezaji katika biashara itupe matokeo tunayotaka, tuandae shamba letu, tuipande sasa mbegu bora, tuweke mazingira rafiki ya (unyevunyevu na mbolea ili ardhi iwe na rutuba) ili mmea ukue na kuzaa sana (provided Oxygen na hali-joto Mungu ashatupa).

Muandishi wa kitabu cha “As a Man Thinketh” James Allen alisema “Men will always gravitate towards that they most secretly want”

Sisi tunachotaka ni nini? Toka mwaka 1997 wakati Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inaasisiwa mpaka leo maiak 11 baadae, nadhani tuko nyuma kwa viashria vya matokeo tarajiwa. Kuna mahala tunakosea, sio dhambi kubadili methodologies, strategies na tactics since we are navigating towards the known goals by taking down poverty with all it takes.

Asalam Aleykum
 
Muarabu na Mhindi unayemuona Tanzania halafu akakuambia mimi ni mtanzania nawewe ukamuamini na kumfanya mtanzania mwenzio imekula kwako,kifupi hawa watu sio watanzania hata kama wamezaliwa kusoma na kukulia hapa, kigezo cha kujifanya ndugu zetu ni wao kupata urahisi wa kuishi na kuingia kwenye mifumo na matumizi ya rasimali zetu kwa kigezo cha uzawa na hii ni siri kweli wanaijua wenyewe na wenzao waliopo India na kwingineko Uarabuni.

Uchumi lazima ushikwe na akina shomvi/kokuleba/Mayala/Maduhu nk ndipo utasema tuko salama na uchumi uko mikononi mwa wazawa, lazima akili zetu ziamua sawa ili mwisho wa siku uchumi kweli uwe kwenye mikono ya weusi wa kyela, Dar, Njombe, Geita nk na heka izungushwe kwenye mipaka yetu na hata ukiita top ten za matajiri basi waje weusi na sio watanzania wenye asili ya wapi sijui.
 
Wawekezaji hawana shida mkuu, shida ni makaratasi na njaa ya viongozi wetu, na usiri uliopitiliza, hata umelete mungu, watu watapiga kiaina
 
Back
Top Bottom