Watanzania na Visa ya UK

Kuntakinte

JF-Expert Member
May 26, 2007
702
28
Jamani wakubwa Heshima zenu!

Kuna kitu mimi sijakipatia jibu maana sielewi kuna umakusudi au watanzani wenye tuu ndio magumashi kwenye suala la kupata Visa.

Majuzi nina jamaa yangu alienda kuomba Visa ya UK kwaajili ya kwenda shule kusoma na kwa jinsi ilivyokuwa na kulingana na muongozo wa British commission requirement jamaa alitimiza kila kitu kilichohitajika na kupeleka pale mishale ya saa 3 asubuhi.

Kwa vile alijaza form Online haikuwa tabu kuingia pale kwa reception na kwenda kufanya submission na kuambiwa arudi saa 8:30 mchana.

Kazi ikaja pale aliporudi na kuona ameandikiwa refusal na huku akihamaki kuona kati ya watu 71 walioomba siku ile ni 4 tuuu ndio waliopata. Sasa kwa mshangao na kutomwamini msela nikajaribu kuuliza kwa watu tofauti na marafiki wakasema hayo ni ya kweli na haya kijiba.

Kwa upande wa pili, inakuwaaje kunakuwa na ugumu sana kwenye Visa ya UK hapa Bongo na nchi kama NIGERIA na GHANA na nyingine kma South Africa wanapata tena bila hata ya migegeseko ya kama Bongo.

Nani mchawi hapa Mwananchi, Wafanyakazi wa British Commission au UK wenyewe hawawataki WATANZANIA?

Naomba msaada wenu ndugu zanguni maana Kuuliza Sio Ujinga wala Ugonjwa? Why? Kwaniniiiiiiiiii?
 
Swali zuri sana, hapana shaka kuna tatizo hapo, aidha ingependeza iwapo mada hii ukaipeleka kule kwenye maswali(Nauliza hivi)
 
Suala hapa sio bongo tu, ni balozi zao zote!
Visa za UK ni issue sana kuzipata, yaani hadi kero.
Mie katika kuihangaikia, nilijikuta nina karatasi za A4 kama 35 hivi mkononi ambazo niliwapa, na bado nilipofika kukawa na maswali kibao, wenyeji wangu akapigiwa simu na kuulizwa kama ana taarifa za ujio wangu nk! Na huo mlolongo unatokana na matukio ya kigaidi ambayo yaliwakumba miaka michache iliyopita, hivyo kunakuwa na ugumu wa kuwaruhusu wageni kwenda kwao.
Likewise, nilimsikia Kikwete akiteta mwaka jana na wabongo walio UK kwamba, hadi mwaka 1995 wabongo walikuwa wanatinga UK bila visa wala kokoro za namna yoyote. Sasa ilipotokea mitafaruku ya kisiasa kule Zenji, wale wenzetu wakatumia mwanya huo "kuhamia" Uk kwa makundi, na hivyo Waingereza wakashtuka na kuanzisha viza.
Sasa mpaka hapa nani alaumiwe?
Mwenye ufafanuzi tunauomba tafadhali!
 
Kuna jamaa mmoja namfahamu alitoswa hapo Bongo mara mbili lakini alikwenda kuombea Botswana akapata.Kuna wabongo wengi wanakwenda kuombea South Africa, na huko nasikia ni pesa yako tu, unaweza hata kutumia ma agents(Sijui kama hii ni kweli??). Mimi naona uchumi wa nchi unayoombea ukiwa bomba na zengwe nalo linapungua, kama unatokea nchi maskini wanaona kuna possibility kubwa ya wewe kutorudi.
Nipeni urais 2010, nitakuza kauchumi kenu hadi waingereza na wamarekani wawafutie visa!!
 
hapa kuna kitu kimoja ambacho ni muhimu kukijua ni kuwa uamuzi wa mwisho ni wa yule anayekuhoji akupe au akunyime,hata kama unakila sababu ya kuomba hiyo viza.
 
Wakubwa nimewapata na heshima sana mchango wenu kwenye hili ila nimesikia mengi leo hii hii kwamba pale British Commission kuna MAMA WA KIHINDI ndio maombi mengi yanapita kwake na yeye ndio mwenye kukubali au kukataa au anakufanyia utaratibu wa Interview sasa sijui kama hili nalo lina ukweli wowote maana inasemekana sina ushahidi ila lisemwalo lipo na kama halipo..... wahindi wengi wanapata VISA hapa Bongo. Kitu Kingine mbona WANAIGERIA wanapeta sana ina maana wao wako vipi?
 
Wakubwa nimewapata na heshima sana mchango wenu kwenye hili ila nimesikia mengi leo hii hii kwamba pale British Commission kuna MAMA WA KIHINDI ndio maombi mengi yanapita kwake na yeye ndio mwenye kukubali au kukataa au anakufanyia utaratibu wa Interview sasa sijui kama hili nalo lina ukweli wowote maana inasemekana sina ushahidi ila lisemwalo lipo na kama halipo..... wahindi wengi wanapata VISA hapa Bongo. Kitu Kingine mbona WANAIGERIA wanapeta sana ina maana wao wako vipi?
duh balaa hili kila kona wameteka magabachori kaka'ke RA anakula BOT yeye anabana kwenye Visa
 
Nadhani hiyo inaweza kuwa "unofficial policy" ya Uingereza katika suala zima la immigration.Kimsingi,suala hili limekuwa likiwaumiza vichwa sana jamaa wa chama tawala cha Labour.Chama pinzani cha Conservatives,kikisaidiwa na right-wing newspapers eg The Sun/News of The World,The Daily Express,The Telegraph,na kianra wao,the Daily Mail,zimekuwa ni force kubwa za kuisukuma Labour kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti kile "racists" hao wanachodai udhaifu wa Labour katika kudhibiti uhamiaji" (note: "uhamiaji" hapa unamaanisha wageni wote wanaoingia nchi hii,iwe kwa masomo,kutembelea ndugu,nk).Pengine kwa shingo upande,Labour ambao kimsingi ni wana mrengo wa kushoto-kati (ambao tofauti na mrengo wa kulia/kulia-kati,kwa kawaida hauna upinzani mkubwa kuhusu suala la uhamiaji)wanajikuta hawana jinsi bali kuzima kelele za wapinzani na wakosoaji kwa kufanya kitu flani (do something).

Ukitaka kuelewa vizuri mawazo yangu,jaribu kuya-monitor magazeti hayo niliyoyataja angalau kwa wiki tu,na kwa hakika utaona kelele zao dhidi ya wageni zinavyoweza kusikuma serikali yoyote ile kuchukua hatua flani.

In fact,wapinzani wa uhamiaji wamekuwa wakitaka kuwepo utaratibu kama wa Australia ambako idadi ya watu wanaoingia nchini humo iko ktk mfumo wa quota.Yaani kwa mfano,kwa mwaka ni watu kadhaa tu.Nasisitiza kwamba sijawahi kusoma au kusikia mahala popote kwamba Labour au Home Office wameweka limit ya wageni,lakini wakati mwingine policies za namna hiyo huwa zinakuwa za kimyakimya.

Ukiangalia mwenendo wa mambo ulivyo hapa UK,ni rahisi kutabiri kwamba kwenye mika kadhaa ijayo kupata visa ya kuingia hapa inaweza kuwa ngumu kuliko kushinda ubunge huko nyumbani (unless uwe na hela ya kuhonga)....sheria mpya kila siku na wanatafuta kila namna ya ku-discourage wageni waliopo hapa kuendela kukaa ardhi hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom