Watanzania na Tanzania

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Sisi ni watu wa ajabu sana. Kwa sisi namaanisha watanzania. Najiuliza;

Dowans! Tumesahau!

Radar! Tumesahau!

Epa! Tumesahau!

Migodi! Haituhusu!

Iptl! Tumesahau!

Mafuta! Tumesahau!

Wizi wa wanyama! Tutasahau!

Jairo! Tunasukuma gari lake! Tunamwimbia na kumsifu!

Pinda! Amedhalilishwa! Tunamuhurumia!

Halafu kila siku ukisalimia 'habari ya asubuhi' unajibu 'salama kabisa Mungu anasaidia' wakati umekaa kwenye foleni three hours, hujapasi shati au gauni hakuna umeme, ada ya mtoto ya shule hujalipa, kodi unadaiwa nk! Bado tunaona ni sawa tu na ni mipango ya Mungu!

Wimbo wetu wa taifa 'eti nikienda safarini sitasahau...' Nchi ya neema! Asali na maziwa!

Nyumbu wana akili sana!

Mbona hata wewe unaonekana kulalamikalalamika tu na UMESAHAU kuchukua hatua zinazoeleweka.

Nadhani hatujasahau hata moja, kuna mengine wewe ndiye umesahau kwani hayaonekani kwenye list. Lakini, kama wewe ni mtanzania basi unawakilisha maelfu kwa maelfu ya watanzania wanaoyakumbuka uliyoorodhesha.

Usitarajie UPINZANI ukusaidie, au eti serikali iamke na kuyakumbuka, timiza wajibu wako, achana na mikwara ya Jairo ati ukitoa siri utakiona cha mtema kuni....

.......wanaosema tumechukua hatua gani nadhani na wao wamesahau kwamba mfumo uliopo hautoi nafasi kwa any actions

au na hilo tumesahau??

Tuna Imani na Jairo oya oya oya Yeleleeeeeee Baba baba baba, Baba huyo baba baba baba huyoo baba baba huyooo Libaba Hilo. Sijui nani ameturoga Walah

Mbona hata wewe unaonekana kulalamikalalamika tu na UMESAHAU kuchukua hatua zinazoeleweka.
Hatua zinazoeleweka ni kuiondoa serikali ya chama cha magamba madarakani, Vinginevyo tutaendelea kulalamika siku zote.

.......wanaosema tumechukua hatua gani nadhani na wao wamesahau kwamba mfumo uliopo hautoi nafasi kwa any actions

au na hilo tumesahau??

Tusitegemee mifumo itupe nafasi...fursa inabidi tuzitengeneze wenyewe wananchi. Wamisri walitinga Tahrir square....

Nadhani hatujasahau hata moja, kuna mengine wewe ndiye umesahau kwani hayaonekani kwenye list. Lakini, kama wewe ni mtanzania basi unawakilisha maelfu kwa maelfu ya watanzania wanaoyakumbuka uliyoorodhesha.

Usitarajie UPINZANI ukusaidie, au eti serikali iamke na kuyakumbuka, timiza wajibu wako, achana na mikwara ya Jairo ati ukitoa siri utakiona cha mtema kuni....

mkuu kama unasema usititarajie upinzani ukusaidie wala serikali umetoa wazo zuri,naomba ueleze zaidi hapo kwenye red

Mbona hata wewe unaonekana kulalamikalalamika tu na UMESAHAU kuchukua hatua zinazoeleweka.

tena issue ya wanyama kutoroshwa kama sikoei mleta mada kwanza ni mwanasheria a pili imetokea ukanda amabao anahusika nao kikazi kwa namna mojaau nyingine na tatu kamasikosei ana madaraka kisiasa Diwani yanayoweza kufanya asikike na kusikilizwa

. Au na yeye kasahau kuw anataiwa kuhakikisha sheria zinafuatwa ?

Watanzania ndio sisi bana inadidi tuanze kuexport wanasiasa. kwa nchi nyingine za afrika ili ziwe na amani na umoja teh teh teh teh

Hatua zinazoeleweka ni kuiondoa serikali ya chama cha magamba madarakani, Vinginevyo tutaendelea kulalamika siku zote.
Kuthubutu kuiondoa CCM madarakani ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe. Hao wapinzani wa kuirithi CCM wako wapi?

mkuu kama unasema usititarajie upinzani ukusaidie wala serikali umetoa wazo zuri,naomba ueleze zaidi hapo kwenye red
Tanzania ni ya watanzania, hivyo tukiwaachia wengine ndio wailinde Tanzania ilhali tunawaona wakiihujumu tutakuwa hatuitendei haki nchi yetu. Ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha analisaidia taifa lake kwa namna anayoweza kulisaidia kuepukana na janga lolote.

Tuna Imani na Jairo oya oya oya Yeleleeeeeee Baba baba baba, Baba huyo baba baba baba huyoo baba baba huyooo Libaba Hilo. Sijui nani ameturoga Walah

Albedo nilitamani kulia! Niliwaangalia wale wafanyakazi moyo ukaniuma sana! Kweli tumelogwa! Na aliyetuloga alienda Libya!

tena issue ya wanyama kutoroshwa kama sikoei mleta mada kwanza ni mwanasheria a pili imetokea ukanda amabao anahusika nao kikazi kwa namna mojaau nyingine na tatu kamasikosei ana madaraka kisiasa Diwani yanayoweza kufanya asikike na kusikilizwa

. Au na yeye kasahau kuw anataiwa kuhakikisha sheria zinafuatwa ?

Watanzania ndio sisi bana inadidi tuanze kuexport wanasiasa. kwa nchi nyingine za afrika ili ziwe na amani na umoja teh teh teh teh

Zing polisi wenyewe na barrier zote kutoka arusha mpaka kia walishindwa kuzuia! Jeshi hawakujua uwepo wa ndege ya Qatar! Idara ya wanyama hawakujua kuhusu wanyama hao! Waziri na Raisi hawajui walipelekwa wapi! Mwanasheria Mkuu hajui lolote! Sasa Diwani na mwanasheria atajua kweli! Nakubaliana nawe hii ndio
Tanzania kamanda!

Mashariki na magharibi, Tanzania tajiri, Watanzania maskini, Tanzania imebarikiwa WaTZ wamelogwa, Tz ina neema, waTZ wamebanwa na hawawajibiki hata wenye nafac, Tanzania imelowa maji, WaTZ wamekauka km kuni, Tz sasa inachakaa, waTZ wachache sana wana neemeka, Wengi wa waTZ utadhani wamekuja kusalimia, kwao wapi? Cjui, Tz, watanzania,Somaaa weee hata shule umalize zote kama ujawa mwongo (mwanasiasa) utoki, Ushirikina sn, uganga kila kona, Ooh! Mungu we2 tz hii mbona umeiweka kwenye holly books? Nn makusudi yako??

Ni vigumu sana kuibadilisha nyeusi kuwa nyeupe na ni rahisi sana kuibadilisha nyeupe kuwa nyeusi na ndio maana kila siku mi naamini kuwa rafiki wa adui yangu ni adui yangu pia.

Kuthubutu kuiondoa CCM madarakani ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe. Hao wapinzani wa kuirithi CCM wako wapi?

Mwita naomba kujua hii maana niichukue ka ilivo au ndo usha maanisha zaidi ya hapo??

Back
Top Bottom