Watanzania na nidhamu ya uoga.tunasema sana vitendo hakuna!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania na nidhamu ya uoga.tunasema sana vitendo hakuna!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Slave, Jan 3, 2011.

 1. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ndg zangu katika JF Napenda nianze kwa kuomba msamaha kabla sijakosea ili ikitokea nimekosea basi ndg zangu msiniadhibu kwa maneno makali. Ndugu zangu mimi nimekuwa nikijiuliza maswali ya kwanini tanzania umasikini,maradhi,ujinga,rushwa,ufisadi bado vinatusumbua?tatizo lipo wapi?mbona ukimuuliza mtu mmoja mmoja kwamba analichukuliaje hili janga?bila shaka watu wengi watasema hawapendi tanzania iendelee kuzumgukwa na hao maadui.hapo hapo ukamuuliza tena tatizo lipo wapi? Bila shaka anaweza akatupia lawama zake serikalini na uongozi kwa ujumla.pia anaweza akakufafanulia katika kutetea majibu yake mpaka ukakubari.ukiwa sasa umelidhika na kufahamu nani chanzo cha matatizo unaweza kushusha pumzi na kuuliza tena kwa mala ya mwisho.nini kifanyike? Majibu ya hapa ndo huwa hayaeleweki.nasema hayaeleweki kwa sababu hapo ndo tiba ya hayo matatizo ilipo.kama watanzania tukifahamu NINI KIFANYIKE bila shaka tutakuwa tumepiga hatua moja mbele. Mfano kuna magazeti kama mawili ambayo ninayafahamu mimi m**h**i na *....a...mw.....a kusema kweli magazeti haya binafsi nayapenda sana kutokana na makala zake zenye uchambuzi hasa zile makala zinazohusu maadui wa taifa hili. Pamoja na wao ukiwauliza nini kifanyike pia hawana jibu linaloleta matumaini. Hivyo basi kutokana na mtazamo wangu eti ninadhani wa tz tuna nidhamu ya uoga.maana kila unalotaka kufanya kwanza tunaangalia usalama wetu. NIDHAMU YA UOGA IMETAWALA SIDHANI KAMA ITAKUJAKUISHA mfano mwingine hapa jf kuna watu wasomi wengi tena nao wazima sana katika kuchambua maslahi ya taifa hawa nao wanaishia kuongea tu njia hawatoi ya nini kifanyike. NDIYO SABABU IMENIFANYA NIKUULIZE WEWE MWANA JF,NINI KIFANYIKE?
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wewe mwenyewe una nidhamu ya woga. Umeanza thread yako kwa kuomba msamaha kabla hata hujakosea ili ikitokea umekosea basi usiadhibiwe kwa maneno makali. Kama huu sio woga ni nini? Pia ume-mention magazeti mawili ambayo unayafahamu "m**h**i na *....a...mw.....a" na umesena unayapenda sana hayo magazeti kutokana na makala zake zenye uchambuzi hasa zile makala zinazohusu maadui wa taifa hili. Sasa kwa nini usiweke majina ya hayo magazeti kama yalivyo? Yaani unaogopa hata kuyataja magazeti ambayo unamini yanachambua habari kwa kina na ukweli? Kama sio woga nini?
   
 3. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nikweli kabisa!Nidhamu ya uoga imetawala.ndio maana nikasema janga hili halitoisha.why? Kwasababu nidham ya uoga imezaa mtoto anaeitwa AMANI hata mimi ni mtanzania nipo tanzania nchi ya amani ninaishi kufutana na mila na desturi nilizozikuta hapa duniani.
   
 4. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tumeshajua kama watanzania ni waoga sasa tujitahidi tuondokane na uoga, tuanze na wewe Slave nini kifanyike?
   
 5. m

  mzambia JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kijumla kila mtz ni mwoga ndo maana hata maandamano ya kuanzia kwa wasomi wetu au wanasiasa wakiona tu ffu basi kazi imekwisha wanatimua mbio.
   
 6. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kaka medy ndio maana nimeamua kuanika hapa jamvini ili wajuvi watupe njia ya nini kifanyike.mimi binafsi mwisho wangu wa kufikiri umefika mwisho.
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mimi najaribu kuuangalia huu uoga kwa upande wa pili wa shilingi.
  Huyu mtoto amani ambaye tuna mlea kwa misingi ya woga nadhani ni bora tuendelee hivyo hivyo kumlea kwa msingi huo maana naamini bado hatuja fikia hatua ya kumtosa mtoto amani.
  Kwanini bado hatujafikia hatua hiyo?. kimsingi woga unaotajwa sana kuwa tunao ni kutokufanya kama walivyofanya ndugu zetu kenya hasa pale tunapo 'hisi' tumeonewa.
  Hiki tunacho dhania tunatakiwa tuwe nacho 'ujasiri' tujaribu kujiuliza kama tunajua faida na hasara zake.
  Hakuna mchezo mchafu kama siasa, wanasiasa wanauwezo mkubwa wa kujaza watu ujinga na kufanya watu kupata 'ujasiri' na ikatokea fujo na mauaji ya kutisha kwa kudhani tu wengine kufa ili baadhi waingie madarakani ndio 'ujasiri'.
  Kenya walijipanga wakamtoa KANU kwa amani lakini sasa hao waliodhaniwa kuwa wakombozi ndio walikuja kuwa wababe kuliko hata kanu,
  Lazima tutambue kuwa ipo njia sahihi ya kupata tunacho hitaji na si lazima kumtosa mtoto amani na kuwa wajasiri ili kupata tukitakacho.
  Kama wananchi wote watakuwa na utayari na kuamua kusema no kwa watawala kwa njia ya kura, hata wafanye nini hawataweza kuzuia wala kuiba kura zote hizo.
  Lakini kama tunaenda ktk chaguzi hatuko strong, hatujajipanga wala kushawishi wapiga kura vya kutosha tutabaki kutafuta 'ujasiri' tukidhani ndio njia sahihi ya kumtoa mtawala tusie mtaka.
  Moja ya gharama ya uchaguzi wa demokrasia ni kuwa haijalishi umemchoka kiasi gani mtawala ili kumuondoa ni lazima kura zipigwe na ashindwe, na hili linawezekana kabisa na mifano ipo mingi ikiwemo jirani zetu kenya,zambia,malawi nk, hawa walishinda kwakuwa walijipanga na wananchi waliamua na tume na wasimamia dola wote walikua wa serikali iliopo madarakani.
  Kwa maoni yangu hatuitaji huo 'ujasiri', tunahitaji kujipanga na kuamua, hao unao wauliza na kukosa suluhisho ndio kutokujipanga kwenyewe.
  Kutamka tu mdomoni kuwa tumechoka ufisadi,umaskini,mikataba mibovu nk haitoshi, kura ndio suluhisho tukiaamua wote na watawala wachakachue hata dunia nzima itajua kuwa tumeibiwa kama ilivyo iveri kosti na si kutakana tuwe 'majasiri' kwa kuhisi tumeibiwa kwakuwa tu mimi na wewe tumewachoka watawala.
  Ukiwa nayo amani huwezi jua uzuri wake lakini pindi itakapo toweka tutatalia na kujuta.

  paulss
   
 8. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  @mzambia unadhani haya matatizo yanayo tuzunguka yataisha? Maana kweli majasusi wa tanzania wapo kuangalia nani kakosa nidhamu. ENDELEA KUCHANGIA MKUU.
   
 9. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kaka medy ndio maana nimeamua kuanika hapa jamvini ili wajuvi watupe njia ya nini kifanyike.mimi binafsi mwisho wangu wa kufikiri umefika mwisho.
   
 10. P

  Paul S.S Verified User

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu zanzibar walikufa watu 23 kwa mambo kama haya, je huo ndio ujasiri unaoutaka tuwe nao?
   
 11. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Paulss umenitoa tongo tongo machoni pangu.kitu muhimu nimejifunza kutoka kwako ni kutumia nguvu ya kura.ila pamoja na hayo hapa kila mtu anaeingia kuogoza nchi huwa anakuta muongo upo.namaanisha katiba hivyo hawezi kufanya lolote kinyume cha katiba. Mfano katiba inasema ukiiba utafungwa.kisha tukachagu mtu ambae tunaamini atatusaidi wakati nae akiingia lazima afuate muongozo.hapo imekaaje?
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hilo nalo neno mkuu.
  Wakati mwingine nikifikiria sana siasa na mustakabali wa nchi hii wakati wa jioni, basi naishia kukamata kili bariiiiiiidi kupotezea
   
 13. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kaka naunga mkono hoja yako 100 % [​IMG] wengi wetu tumekuwa watu wa kulaumu na kuongea majungu chini chini bila vitendo...Watanzania wananung'unikia midomoni tu, wanaibiwa rasilimali zao, bei za bidhaa zinaongezeka kila kukicha pasipo maelezo ya kina, leo kodi ya umeme imepanda, tumeambiwa tulipe Dowans tumeanza kulipa, tunadanganywa waziwazi kwa ahadi za uongo zisizotekelezeka, yote haya na mengineyo hayana maelezo ya kina lakini Watanzania tumeishia kuzungumza chini chini.
  Kuhusu NINI KIFANYIKE mkuu nadhani Watanzania hawako tayari kukombolewa ndio maana leo hii wanatii kama kondoo kila jambo wanaloambiwa au kufanyiwa, na wewe ukipata nafasi itumie, 'KULA' kwa urefu wa kamba yako hii ni nchi ya asali na maziwa watu kutoka nje wanaitafuna nchi hii kitakatifu nasi tunawakarimu na kuwakaribisha tena na tena (rejea makampuni ya kigeni)wazawa tunawapongeza kwa kuiuza nchi na kuwachagua tena na tena kushika nafasi kutuongoza. Kaka ukipata nafasi 'ITAFUNE' nchi hii ni tamu huku ukitupaka mafuta Wadanganyika kwa mgongo wa chupa...
  Nawasilisha.
   
 14. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #14
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo mtoto Amani unayemuongelea ni yupi kwa watanzania waliojaa umaskini ndani ya nchi iliyojaa utajiri na kuliwa na wachache?
   
 15. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #15
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF hawamo kwenye kundi hilo la waoga
   
 16. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  sana tu kaka afadhari ya kujipa no sweat na moja moto moja baridi kuliko kuifikilia hii nchi. Unaweza ukawa mwehu.
   
 17. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  bro paulss zanzibar walikufa zaidi ya watu 23. Yaani hao 23 ni wale tuliotangaziwa na vyombo vya habari.lakini pamoja na hayo leo hii kuna unafuu flani uliopatikana kutokana damu yao 1 serikali xa mseto pia ninaimani kuna mengine mengi tu.mkuu naomba ujikumbushie historia ya mkombozi yesu alivyo kufa kwa ajili yetu.na ulinganishe na ukristo ulivyo imara leo. Mwanasiasa bob marley alivyo chomwa sindano ya sumu mpaka kupelea umauti wake kwa ajili ya wa south.angali akina mkwawa,mirambo,mangi,na wengine kibao.angalia vita vya kagera watu walivyopoteza maisha kwa ajili ya nchi yao.vipi unaonaje jinsi watu walivyokuwa na jinsi gani wameleta unafuu.MKUBWA SONGA NAO MADA......
   
 18. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  umeona udom? Wote mbio!!
   
 19. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  ila ninawasiwasi CUF Nao wakipewa hili gari waliendeshe nao watakuta kiti kile kile stering ile ile na safari ya gari inaenda kule kule kwenye shimo kubwa.pengine hili gari limekaribia kufika mwisho wa safari yake.
   
 20. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  umeona udom? Wote mbio!!
   
Loading...