Watanzania na mfano wa samaki anayeishi majini na kuhisi kiu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania na mfano wa samaki anayeishi majini na kuhisi kiu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Deogratius Mosha, Aug 10, 2012.

 1. D

  Deogratius Mosha Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania wenzangu, sio nia yangu kuandika mada hii ila naaminini ni siasa mbovu zilizo tupatia viongozi wabovu ndizo zilizotufikisha hapa tulipo. Hivyo awali ya yote ni kitambua kwamba maissha ya shukrani ni maisha ya fadhila nianze na kumshukuru Mungu kwa zawadi kubwa ya uzima aliyonijalia. Ndugu watanzania wenzangu huwa ninakaa na kutafakari kwa kina UPENDO mkubwa wa mwenyezi MUNGU kwa taifa hili zuri alilotupatia na utajiri aliouweka karibu sehemu kubwa ya nchi hii.

  Ndugu zangu ninajiuliza maswali mengi sana tena sana, na kukosa majibu, kwa mfano;
  1. Kwanini Mwenyezi Mungu alipenda, madini pekee duniani ya tanzanite yawepo katika ardhi hii???
  2. Kwanini MUNGU alikusudia ziwa victoria lililo ziwa la pili kwa ukubwa duniani liwepo Tanzania??????
  3. Kwanini huyu Mungu alipenda mlima mkubwa kuliko milima yote Africa na mlima wa pili kwa ukubwa duniani uwe hapa Tanzania?????
  4. Kwanini Mungu huyu alipenda rasilimali nyinginezo kama, dhahabu, almasi, gesi, makaa ya mawe, uranium na mbuga za wa nyama kama, Ngorongoro, mikumi, Tarangire, Arusha National Park, Seluu, Ruaha national park, kilimanjaro national park, na Serengeti, kwa kutaja chache tu ziwepo hapa Tanzanzania???????
  Kwa maswali hayo yote, majibu yake ni dhahiri kwamba huyu Mungu aliipenda na anaipenda sana Tanzania tena anaipenda UPEO. Masikitiko yangu ni kwamba, viongozi wetu wakuu katika nchi hii iliyopewa upendeleo mkubwa na Mungu kwa nyakati tofauti na kauli za kufanana, wanaulizwa kwanini watanzania ni masikini na neema hii Mungu amewapa bure?? Majibu yao yamekuwa ya kufanana hata kiasi cha kusema ata wao wenyewe hawajui kwanini watanzania ni masikini??? Nikiwa kama muumini wa ukweli nilisikitishwa sana tena sana na kauli hizi za viongozi tena viongozi wakuu wa nchi, na kujiuliza, inawezekana Ndugu Kikwete na Pinda wanapotoka kwenye majumba yao ya kifahari, wanadhani na watanzania nao wanaishi maisha kama ya kwao. Leo hii miaka hamsin ya uhuru, taifa lenye utajiri kama tanzania, watu wanakufa na njaa, wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ajira zimekuwa tabu, wasomi wanaongezeka, wanazagaa mitahani hawana la kufanya, bado viongozi wetu hawajui kwanini watanzania ni masikini.

  Ndugu zangu, tatizo hapa sio rasilimali tulizonazo kwani Mungu alishapenda rasilimali hizo ziwaneemeshe watanzania, tatizo sugu ni viongozi wetu, ambao wanakiuka maadili ya uongozi na badala ya kulitumikia taifa wanatumikia familia zao kwa kujilimbikizia mali, kuuza rasilimali hizi kwa wageni (wawekezaji)na kuwaacha watanzania wakibaki hoehae.

  Wapendwa kwa wkristu wenzangu tunatambua safari ya ukombozi ya wana waisraeli kutoka utumwani misri mpaka nchi ya ahadi aliyowaaidia Mungu "KANAANI". Nchi hii ni nchi iliyojaa maziwa na asali, hakuna kusikia kiu na neema za kutosha ambaya kwa sasa sina budi kuifananisha na Tanzania ya leo.

  MUHIMU: Ninawasihi watanzania wenzangu tuakisi katika mabadiliko ya kweli, na MUNGU akitusimamia kwa dua zetu na sala kumwomba mungu atupatie viongozi wakutufikisa katika nchi ya ahadi iliyojaa asali na maziwa, na kutoka huku utumwani tuliko leo na viongozi wasioweza kutufikisha huko.

  MWISHO: "Ukimwana samaki ndani ya maji na anasikia kiu, samaki huyu anaitaji serious professional cancelling" Tafakari chukua hatua!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...